Vatican News
Ushuhuda wa familia moja kutoka Afrika mbele ya Baba Mtakatifu katika tamasha la Familia kwenye uwanja wa Croke Dublin Ushuhuda wa familia moja kutoka Afrika mbele ya Baba Mtakatifu katika tamasha la Familia kwenye uwanja wa Croke Dublin  (Vatican Media)

Farrell:Kwa mara nyingine Injili inatoa matumaini kwa familia!

Baraza la Kipapa la Walei, familia na maisha wanafuraha kubwa kwa ajili ya Kanisa la Ireland jinsi walivyokubali kupokea na kuanadaa tukio hili kwa ajili ya huduma ya Kanisa zima. Kwa namna hiyo Kardinali Farrell amewasalim makardinali, maaskofu na wawakilishi maalum kutoka nchi mbalimbali wakiwemo, mapadre,watawa, walei na watoa mada wote!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Kabla ya kuwasili Baba Mtakatifu Fransisko, nchini Ireland katika zaiara yake ya Kitume kwenye fursa ya Mkutano wa Familia Dunia, Kardina Kevin  Joseph Farreli Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha wakati kongamano la Kichungaji aliwaambia kuwa, Baba Mtakatifu anakariba kufika katika Mkutano wa 9 wa Familia diniani, Tumkaribishe kwani yeye anayekuja kwa jina la Bwana. Mkutano wa Dublin ni wa dunia kwasababu wawakilishi maalum ni kutoka nchi 140 na namna kubwa ya familia ya dunia nzima ambao wanajadili kwa moyo, mawazo na sala. Familia zote zinazo amini na zile zisizo amini, zilizotengena na zile zilizo ungana, zenye furaha na zile zinazoteseka.

Zaidi wanataka kushukuru Taasisi ya raia ambao kwa namna nyingi wameweza kushirikiana kwa ajili ya tukio hili la Kanisa. Baraza la Kipapa la Walei, familia na maisha wanafuraha kubwa kwa ajili ya Kanisa la Ireland jinsi walivyokubali kupokea na kuanadaa tukio hili kwa ajili ya huduma ya Kanisa zima. Kwa namna hiyo anawasalimu makardinali, maaskofu na wawakilishi maalum kutoka nchi mbalimbali wakiwemo, mapadre, familia watoa mada na washiriki wote zaidi wale wanaotoka mbali.

Injili ya Familia: furaha ya ulimwengu ndiyo mada iliyochaguliwa na Papa kwa ajili ya mkutano huo kama wazo ambalo linafuata Wosia wa kipapa wa Amoris Laettia yaani (Furaha ya upendo ndani ya familia), Waraka ambao unastahili kwa dhati katika kuwajibika kichungaji. Kiini kinachotawaa ni kile cha furaha kwasababu pamoja na hatari na kipeo kinacho hatarisha leo hii familia, Injili inatoa kwa mara nyingine ujumbe wa matumaini na furaha.

 Papa Francisko kwa shukrani kubwa anafurahi kwa kutangaza Injili ya familia na kufanya Sikukuu na familia nyingi mjini Dublin na familia zote ulimwenguni. Uwepo wake unaweza hasa kuwa makini na kuchukuliwa kwa vyomb vya habari na taasisi nyingi katika suala la familia na zaidi kutoa imani na ujasiri kwasababu papa ni shuhuda wa kweli katika kujikita kubeba ndani ya moyo wake familia katika Kanisa na pia kwa Mungu mwenyewe.

Umakini wa Papa Fransisko katika Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia (Furaha ya upendo ndani ya familia) ambo kwa namna ya pekee umekuwa kiini cha Mkutano mjini Dublin katika kongamano na sikukuu ya familia, unajikita zaidi ya mada ya upendo wa kweli kwa wanandoa na familia katika mwanga wa Injili, uzoefu, na tafakari ya pamoja; upendo kwa maana ya kujitoa binafsi kwa ajili ya mwingine, urafiki wa dhati ambao unaunganisha upendo, shauku, tamaa na furaha ya kutoa na kupokea. Mambo hayo yote Kardinali anasema yanahitahi ukomavu, kwa ngazi ya kibinadamu na kikirstu katika machakato wa muda mrefu kwa kipindi ambacho kinajikita kwenye mafunzo ya akili na utashi, wa shauku, upendo na hasa hisia, kwa kutafuta na kushawishi katika mtindo wa wema, ambao unapitia katika sheria za maadili na kujieleza mahitaji yake kwa neema ya sakaramenti ya ndoa

Upo utambuzi wa kuwa familia ni uzoefu wa ulimwengu katika historia ya kibinadamu na ambayo imeomba tangu kizazi hadi kizazi kati ya mwanamke na mwanaume kwenye mahusiano kati yao watu wawili katika kizazi, na kuwa wanazaa watoto. Hata lei hii uchunguzi na takwimu zinaonesha kuwa familia ambayo imeundwa na mama, baba na watoto ndiyo iliyo mstari wa kwanza kwa kuigwa na vijana. Katika Komgamano la kitaalimungu la kichungaji siku hizi mada hii imepata nafasi nzuri katika hotuba nyingi na mafundisho, kadhalika katika meza za mduara, uzoefu na mijadala kwa umakini wake kwa watu, na kusikiliza sifa nyingi kutoka ulimwengu mzima.

Pamoja na hayo tamasha na sikukuu hii itaonesha kwa dhati japokuwa inapita katika mateso na taabu, furaha na matumaini ya familia nyingi. Aidha amesema yeye kama mzaliwa wa Ireland anatambua vema jisni gani imani ya kikristo imetanda mzizi wake wa maisha ya kila siku. Watu wengi wanatambua malezo ya Kardinali Tomás Ó Fiaich (1923-1990), ambaye alikuwa anafananishwa na waamini walei kama jitu kubwa lililolala na ambalo lazima liamshwe.  Kwa njia hiyo yeye binafsi anafikiri na kuona wakati endelevu wa familia, nchini Ireland na Kanisa la Ulimwengu. Kwa pamoja na wakatoliki wa Ireland na kwa jina la Familia yote ya Mungu iliyofika Dublin katika kuwakilisha ulimwangu, tumkaribishe Papa Fransisko “Céad Míle Fáilte”, yaani mara mia elfu!

26 August 2018, 13:45