Vatican News
Papa Francisko akiwa amepiga magoti ndani ya  Kanisa dogo la kutokea Mama Maria huko Knock nchini Ireland Papa Francisko akiwa amepiga magoti ndani ya Kanisa dogo la kutokea Mama Maria huko Knock nchini Ireland  (Vatican Media)

Mama Maria asaidie katika shughuli za kueneza Ufalme wa Mungu!

Siku ya pili ya Papa Francisko nchini Ireland, katika fursa ya Mkutano wa IX wa Familia Duniani. Tarehe 26 Agosti ametembelea madhabahu ya Bikira Maria wa Knock na kuongoza sala ya malaika ya Bwana mbele ya waamini na mahujaji wapatao 45,000 .

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

“Hakuna mtu yeyote asiye weza kuguswa na historia ya wadogo ambao wameteseka na manyanyaso na ambao wameibiwa udogo wao bila hatia au waliondolewa kwenda mbali na wazazi, kuachwa katika uchungu mkubwa. Hata katika Madhabahu ya Bikira Maria huko Knock kabla ya kusali sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amerudia kuzungumza juu ya janga lililofunguliwa wazi la manyanyaso yaliyo wakumba watoto kutokana na wahusika wa Kanisa la Ireland.

Baba Mtakatifu anasema, tunapaswa kuwa na msimamo halisi wa kutafuta ukweli na haki, ninaomba msamaha kwa Bwana kwa ajili ya dhambi hizi, fedheha, na usaliti ambao umeshitakiwa  na familia nyingi za Mungu. Na  kuthibitisha juu ya kutafuta  suluhisho la pendekezo ya kutoruhusu janga ili lisitukie tena. Baba Mtakatifu ameomba kwa maombezi ya Bikira Maria, kwa ajili ya waathirika na ili wote walio husika waweze kuendelea daima katika haki na kufanya malipizi ya ghasia nyingi zilizotukia.

Familia zichukue hatua ya kusaidia walio wa mwisho.

Katika ziara ya Kitume ya 24 ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Ireland, na ikiwa ni fursa ya Mkutano wa Familia duniani, mara baada ya kufika Knock ameingia  katika Kanisa dogo la Kutokea  kwa Bikira Maria huko  katika Kijiji cha Contea Mayo kinachojulikana duniani kote kutokana na Madhabahu hiyo na kusali.

Alifanya tendo la sala kabla ya kutoa zawadi ya Rosari ya dhahabu kwa Bikira Maria, kama utambuzi wa muhimu wa nchi ya Ireland wa kusali  Rosari kama ilivyo utamaduni wake ndani ya familia. Baba Mtakatifu amesema, kwake Maria anayetambua furaha na ugumu wa uzoefu wa kila kitu katika nyumba, anamkabidhi familia zote dunia, ili Mama Maria uweze kuwasaidia katika shughuli zao za  kueneza Ufalme wa Kristo na kuwatunza wale walio wa mwisho.

Kati ya matukio na dhoruba ambazo zinasonga nyakati hizi, imani ndiyo iwe ngao na wema ambao kwa mujibu wa utamaduni wa taifa, wavumilie kila aina ya chochote ambacho kinataka kupunguza hadhi ya mwanaume na mwanamke walio umbwa kwa mfano wa Mungu, amewaalika katika kushiriki ukuu wa maisha ya milele.

 Amani na maelewano kwa ajili ya Ireland

Kati ya mawazo ya Baba Mtakatifu Fracisko ni kwa ajili ya Ireland ya Kaskazini na ambapo anawahakikishia upendo wake na ukaribu wa sala. “Kwa furaha ya maendeleo ya kiekumene na maana ya kukuza urafiki na ushirikiano kati ya jumuiya za kikristo, Baba Mtakatifu anasisistiza kuwa, anasali ili wafuasi wa Kristo, waweze kupeleka mbele na katika msimamo wa thati zile nguvu kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa amani na ujenzi wa jamii ya maelewano, umoja na haki kwa ajili ya watoto wa sasa”.

Mshikamano wa sala kwa wafungwa katika magereza nchini Ireland:

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa salam maalum kwa wanaume na wanawake ambao wamefungwa katika magereza ya Ireland. Baba Mtakatifu Francisko amsema: Ninawakikishia uwepo na familia zenu ukaribu wangu na sala zangu. Mama Maria wa Huruma akeshe juu yenu na kuwapa nguvu katika imani na katika matumaini.

27 August 2018, 10:30