Papa Francisko anaendelea kuombea wagonjwa wa virusi vya Corona na wahudumu wote wa afya katika misa mubashara kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican Papa Francisko anaendelea kuombea wagonjwa wa virusi vya Corona na wahudumu wote wa afya katika misa mubashara kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican  

Papa:wachungaji wawe karibu na watu:Wakati mwingine hatua kali siyo nzuri!

Katika Misa ya Papa Francisko kwenye Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 13 Machi sambamba na kukumbuka mwaka wa 7 tangu kuchaguliwa kuwa Papa ameendelea kusali kwa ajili ya wagonjwa lakini hata kwa upande wa wachungaji kwa sababu waweze kuchukua hatua ambazo hawaachi watu wa Mungu peke yao na wawasindikize kwa nguvu ya Neno la Mungu, sakramenti na sala.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika misa takatifu ya tano ikiwa kwa njia ya mubashara katika Kanisa La Mtakatifu Marta mjini Vatican, na ikiangukia katika siku ambayo ni mwaka wa saba tangu kuchaguliwa kwa Papa Francisko katika kiti cha Khalifu wa Mtume Petro. , bado ameendelea kusali kwa ajili ya wagonjwa wa virusi vya corona, lakini pia wazo kuu limewaandea kusali kwa ajili ya wachugaji wa Kanisa. Papa

Katika siku hizi tuungani kwa pamoja na wagonjwa, familia ambao wanateseka kutokana na janga hili. Ninapendelea kusali leo kwa ajili ya wachungaji ambao wanapaswa kuwasindikiza watu wa Mungu katika kipeo hiki. Bwana aweze kuwapa nguvu na  uwezo wa kufanya mang’amuzi bora ya kuweza kuwasaidia. Hatua kali wakati mwingine siyo nzuri kila wakati na kwa maana hiyo tusali kwa Roho Mtakatifu aweze kuwajalia wachungaji ule uwezo na mang’amuzi kichungaji ili waweze kutafuta hatua ambazo haziwaachi watu watakatifu waamini wa Mungu. Watu wa Mungu waweze kuhisi kisindikizwa na wachungaji na kutiwa nguvu na Neno la Mungu, sakramenti na sala.

Kwa hakika Papa Francisko hasemi kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali kwa kuzuia maambukizi na  kuzuia mikusanyiko ya umma, bali anawageukia wachungaji ili waweze kuzingatia mahitaji ya waamini ambao wanahitaji kusindikizwa kiroho katika wakati huo mgumu. Katika mahubiri ya Papa Francisko kwa kutazama masomo ya siku  kwa namna ya pekee kuhusu mfano uliotolewa na Yesu katika Injili wa mtu mwenye nyumba, aliyepanda shamba la mizabibu, na kawapangisha wakulima, na kusafiri, Papa anafafanua kwamba inazungumza kuhusu ukosefu wa uaminifu wa yule anayepewa zawadi ya Mungu na ambayo ni utajiri; uwazi na baraka na kuufungia katika mafundisho (Mt 21, 33-43.45). 

“Masomo yote mawili yana utabiri wa Mateso ya Bwana. Yusufu aliuzwa kama mtumwa kwa vipande vya fedha ishirini na kumkabidhi kwa wapagani. Mfano wa Yesu kwa kwa huo huko wazi kwa maana unazungumza ishara ya kuuawa kwa Mtoto. Historia ya mtu mwenye nyumba, ambaye alipanda shamba la mizabibu, alikuwa na utunzaji mwema akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, alikuwa amefanya vizuri sana. Baadaye akapangisha wakulima, akasafiri kwenda mbali. Hawa ndiyo watu wa Mungu. Bwana analiwachagua watu wale, kwa maana kuna uchaguzi wa watu hao. Ni watu wateule. Kuna hata ahadi anawaagiza kwamba  endeleeni mbele. “Ninyi ni watu wangu”, ahadi aliyopewa Ibrahimu. Kuna hata agano lililopewa kwa watu wa Sinai. Watu wanatakiwa daima kutunza katika kumbu kumbu ya uteule  ya kwamba ni watu wateule, waliopewa ahadi ya ktazama mbele kwa matumaini na agano la kuuishi uaminifu huo kila siku. Lakini katika msema huu panatoke jambo jingine inapofikia wakati wa mavuno ya matunda ulipokaribia watu hawa walikuwa wamesahau ya kuwa  wao siyo mabwana. “Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vile vile

Kwa hakika Papa ameendelea kusema:  Yesu anataka tuone anavyozungumzia walimu wa sharia, kama vile waandishi wa sharia walivyowafanya manabii. “Hatimaye akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua”.Waliiba urithi ambao ulikuwa ni wa mwingine. Historia hii inahusu ukosefu wa uaminifu, kutokuwa mwaminifu wa uteule, ukosefu wa uaminifu wa ahadi, ukosefu wa uaminifu wa agano ambalo ni zawadi. Wamekosa uaminifu wa zawadi ya Mungu. Hawakutambua kama ilikuwa ni zawadi na wakaifanya kama vile ni mali binafsi. Watu hawa walijibinafsisha zawadi hiyo na wakaichukua mbali kuwa zawadi na kuibadili kuwa mali binafsi “ yangu”.  Zawadi ambayo ilikuwa ni utajiri ,uwazi, na baraka waliifunga ndani ya mafundisho ya sheria nyingi. Ilibadilishwa katika itikadi na kwa maana hiyo zawadi ikapoteza maumbile na dthamani yake kama zawadi na kuisha katika itikadi.  Hasa katika itikadi ya maadili iliyojaa maagizo, hata kuchekesha kwa sababu iliingia katika masomo kwa kila kitu. Hawa walijibinafsisha zawadi.

Hii ni dhambi kubwa. Ni dhambi ya kusahau kuwa Mungu amejifanya zawadi yake mwenyewe kwa ajili yetu na ambayo Mungu alitupatia kama zawadi na kusahau hilo kwa kugueka mabwana. Ahadi siyo tena ahadi na uteule siyo tena uteule. Agano lazima litafsiriwe kwa mijibu wa mawazo yangu ya kiitikadi. Papa amebainish na kuendelea kufafanua zaidi kwamba: hapa, katika mtazamo huu, ninaona labda mwanzo, katika Injili, ya ukikuhani ambayo ni njia ya upotovu, ambao kila wakati unakanusha uteule  wa bure wa Mungu, agano la bure la Mungu, ahadi ya Mungu ya bure. Anasahau ufunuo, wa bure ambao Mungu alijidhihirisha kama zawadi, akajifanyia zawadi kwa ajili yetu na sisi lazima tuitoe, kuifanya ionekane kwa wengine kama zawadi, lakini siyo kama milki yetu. Ukikuhani siyo jambo moja tu la siku hizi, kuwa na ugumu siyo jambo moja la siku hizi, ulikuwa tayari upo katika kipindi cha Yesu. Baadaye Yesu aliendelea mbele kuelezea mifano hiyo katika sura ya 21 hadi  23 na kwa kuhukumu, mahali ambapo palionekana hata hasira ya Mungu dhidi ya wale ambao wanamiliki zawadi na kuipunguza utajiri wake kutokana na ufedhuri wa itakadi katika akili zao. Na kwa kuhitimisha anasema: Tuombe Bwana neema ya kupokea zawadi kama zawadi na kuionyesha zawadi kama zawadi isiyo mali binafsi na isiwe kama ya njia za madhehebu yaibukayo yenye mtindo mgumu na tabia za ukikuhani.

PAPA:MAHUBIRI
13 March 2020, 12:16
Soma yote >