Tuwakumbuke kila siku  watu wanao tusindikiza katika safari ya maisha yetu kwani uwepo wao mara nyingi unageuka kuwa wa kifamilia ambapo ni vema kutoa shukrani au kuomba msamaha kutokana na udhaifu unaojitokeza. Tuwakumbuke kila siku watu wanao tusindikiza katika safari ya maisha yetu kwani uwepo wao mara nyingi unageuka kuwa wa kifamilia ambapo ni vema kutoa shukrani au kuomba msamaha kutokana na udhaifu unaojitokeza.   (� Vatican Media)

Papa Francisko:Tuwakumbuke watu tunaosafiri nao katika maisha yetu!

Katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 14 Februari 2020,amejikita kufafanua juu ya maisha ya kila siku katika nyumba ya Mtakatifu Marta,hasa kwa kutoa shukrani kwa wote wanaofanya kazi kwa upendo mkubwa na kusindikizana katika safari ya maisha.Tafakari hii imetokana na sura ya mfanyakazi katika nyumba hiyo anayestaafu ambapo ametumia fursa ya kumshukuru na kushukuru wote!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mahubiri ya Papa Francisko tarehe 14 Februari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican , amewaalika watu wakumbuke kila siku wale watu wanaowasindikiza katika safari ya maisha yao, kwani uwepo wao mara nyingi unageuka kuwa wa kifamilia ambapo ni vema kutoa shukrani au kuomba msamaha kutokana na udhaifu unaojitokeza. Amesitiza hayo kwa kutazama nyumba ya Mtakatifu Marta ambayo inakuwa  ya familia kubwa yenye mzunguko wa watu ambao wanawasaidia katika safari ya maisha na kila siku wanafanya kazi hapo, kwa kujitoa, utunzaji na kuwasaidia ikiwa mtu anaumwa, wanakuwa na uchungu iwapo mmojawapo anaondoka. Ni sura zenye tabasamu na salam, kwa maana ni mbegu zinazopandwa katika moyo wa kila mmoja. Kwa kufafanua hayo alikuwa anamlenga mama mmoja mfanyakazi Patrizia ambaye ametaafu na hivyo amemshukuru kwa yote na kuomba msamaha iwapo palijitkeza udhaifu fulani.

Papa Francisko katika mahubiri yake ameeleza ukawaida wa nyumba ya Mtakatifu Marta  mjini Vatican kwa kungalia juu ya familia iliyo kubwa ambayo unakuta kuwa siyo baba, mama, mama wadogo, kaka wajomba, bibi, lakini pia ni familia iliyokubwa na ambayo inawasindikizwa na wote waliomo ndani katika maisha ya kila wakati. Baada ya miaka 40 ya kazi, Patriza anastaafu ambaye alikuwa amekuwa kam mwanafamilia aliyewasindikiza kwa kipindi kirefu katika nyumba hiyo na ndiyo maana ya mahubiri yaliyolenga sura kama hiyo. Na hii itakuwa vizuri wote wanaoishi katika nyumba hiyo kufikiria familia ambayo inawasindikiza, na kwa wote wasio ishi hapo kufikirie pia watu wengi ambao wanawasindikiza katika safari ya maisha, walio karibu, marafiki, wafanyakazi wenzao, , katika masomo na wengineo… kamwe sisi sote hatuko peke yetu amebainisha Papa . Bwana anataka watu wake wasindikizwe na hataki ubinafsi, kwa maana ubinafsi ni dhambi.

Katika tafakari hii, Papa amekumbuka ukarimu wa watu wengi wanafanya kazi na ambao wanawasindikiza wagonjwa katika nyumba ya Mtakatifu Marta na kusema kuwa nyuma ya kila jina kuna uwepo wa historia ambayo inabaki kama ishala.  Papa Francisko amkumbuka Luisa , Kristina, bibi wa nyumbani, Sr.  Maria aliyeingia kufanya kazi akiwa kijana na baadaye akajiunga na shirika la kitawa, amesema Papa. Papa katika kukumbuka familia yake kubwa, lakini pia amewakumbuka hata wale ambao hawapo tena wamekwisha eleke kwa Mungu Baba, kwa mfano amekumbuka Miriam aliyefariki akiwa mjamzito, na Elvira aliyekuwa mfano wa kupambania maisha hadi mwisho.   Vile vile amemkumbuka wengine walio staafu au kwenda kufanya kazi mahali pengine . Uwepo wao ambao ni vema kuukumbuka  na wakati mwingine ni vigumu kuwaacha waondoke, amebainisha. “Ni vema leo kuwakumbula na kusema asante Bwana kwa kuwa hukutaacha peke yetu. Ni kweli kwamba daima kuna matatizo, na mahali ambapo kuna watu kuna maneno”.  Papa amebainisha kwamba hata mahali pale maneno hayakosekani. Wanasali lakini pia wanasema sema hivyo, mambo yote mawili yanatendeka na wakati mwingine ni kutenda dhambi dhidi ya upendo, amebaninisha Papa.

Kwa kuhitimisha amesema kutenda dhambi, kukosa uvumilivu na baadaye kuomba msamaha ndivyo vinavyo fanyika katika familia. Kwa maana Papa ametaka kushukuru kwa ajili ya uvumilivu wa watu ambao wanaawasindikiza na kuwaomba  samahani kwa udhaifu  huo. Na kwa wote ambao wanafanya kazi katika nyumba ya Mtakatifu Marta amewashukuru sana  hata kwa Patrizia ambaye anaanza hatua ya pili akimtakia maisha mengine zaidi ya  miaka 40!

14 February 2020, 14:14
Soma yote >