Amani ya kweli inatoka ndani ya moyo na hiviyo tuombe Mungu atujalie amani hiyo. Ni maombi ya papa Francisko wakati wa mahubiri ya Ibada ya Misa asubuhi tarehe 9 Januari 2020 Amani ya kweli inatoka ndani ya moyo na hiviyo tuombe Mungu atujalie amani hiyo. Ni maombi ya papa Francisko wakati wa mahubiri ya Ibada ya Misa asubuhi tarehe 9 Januari 2020   (ANSA)

Papa Francisko:Amani ya kweli inatoka ndani ya moyo!

Papa Francisko wakati wa mahubiri yake Alhamisi 9 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican,ametafakari kuhusu Somo la kwanza ambapo Mtakatifu Yohane anaelekeza njia ya kufikia amani.Lazima kubaki na Bwana kwa upendo unaojitambulisha katika mambo madogo.Amani duniani inajengwa kuanzia ndani ya moyo.Tujiulize kama kweli ndani mwetu kuna amani hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Alhamisi, tarehe 9 Januari 2020 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican, Papa Francisko wakati wa mahubiri yake amekazia juu ya suala la amani, ambapo ameomba sala kwa Mungu ili aweze kutujalia amani ya kweli. Papa amesema: “hatuwezi kuwa wakristo ikiwa tunapanda vita ndani ya familia, katika mitaa yetu na katika nafasi zetu za kazi. Na kwa maana hiyo tuombe Bwana ili aweze kutupatia Roho Mtakatifu ili kubaki na Yeye na atufundisha  kupenda na maana rahisi ya kutofanya vita dhidi ya wengine. Katika mahubiri hayo amekumbusha sala ya mwanzo mwa Liturujia ambayo inaomba Mungu ajalie watu wote amani ya kweli. “Tunapozungumza amani, kwa haraka tunafikiria vita na ili duniani isiwe na vita na  kwamba amani ya kweli ni sura inayokujia kila mara na siyo vita, japokuwa nje na katika nchi ile na katika hali ile… Ni kuonesha kwa haraka wakati huu kumekuwapo na moto wa vita unaowaka  na idyo fikra zinakwenda hapo na kumgeukia Bwana ili atujalie amani”. Ni lazima kusali kwa ajili ya amani duniani, lazima kuwa na mtazamo huo mbele yetu wa kuwa na zawadi ya Mungu ambayo ni amani na kumwomba kwa ajili ya watu wote.

Kubaki na Bwana

Papa Francisko ametoa ushauri wakati huo huo kujiuliza “namna gani amani inajionesha  ndani ya nyumbani mwetu na kama  ipo ndani ya mioyo yetu au  kuna wasi wasi na  daima vita, mivutano ya kutaka kuwa na lolote la zaidi, kwa ajili ya madaraka na kutaka sifa ya kusikika”. Amani kwa watu au kwa Taifa, inapaswa ianzie ndani ya moyo amebainisha Papa. Ikiwa sisi tunataka amani moyoni kama tunavyofikiri,  je tunaiomba iweze kutawala duniani? Au kama  kawaida hatufikiri. Somo la siku Mtakatifu Yohane mtume anaonesha njia  ya kufikia amani ya ndani yaani ile ya  kubaki na Bwana, amesema Papa.

Palipo na Bwana kuna amani

“Palipo na Bwana kuna  amani. Ni yeye anayefanya amani”,  ni Roho Mtakatifu ambaye anatumwa na Yeye ili kuleta amani ndani. Ikiwa tutabaki ndani mwa Bwana  mioyoni mwetu tutakuwa na amani; ikiwa tutabaki kama kawaida na Bwana na wakati tukiangukia katika dhambi au kosa lolote, Roho atatuonyesha makosa hayo ya kuanguka”. Amesema Papa. Je ni kwa jinsi gani tuweza kubaki na Bwana? Mtume Yohane ametoa jibu ya kwamba iwapo  “tukipendana sisi kwa sisi”. Na ndilo jibu na ndiyo siri ya amani Papa Francisko amebainisha.

Kishawishi cha ibilisi

Papa Francisko akiendelea amezunguza juu ya upendo wa kweli na siyo ule wa tamthiliya na maonesho, bali ni ule unatusukuma kuzungumza vema juu ya wengine na kinyume chake, iwapo huwezi kufanya hivyo basi ni bora kufunga mdogo, bila kutoa  domo au kusimulia mambo mabaya. Na hiyo ni ka sababu kusema na kusengenya wengine ni vita. Upendo unakufanya utazame mambo madogo madogo kwa sababu ikiwa kuna vita ndani ya moyo wangu,  kutakuwa na vita katika familia yangu, kutakuwa na vita katika mtaa wangu na kutakuwa na vita katika nafasi yangu ya kazi. Wivu, kijicho na masengenyo amebainisha Papa, vinatupelekea kufanya vita dhidi ya wengine na kuwaharibu, ni kama vike uchafu.   Wito wa Papa Francisko kwa mara nyingine tena ni ule wa kutafakari kwamba, ni mara ngapi unazungumza na roho ya amani, na mara ngapi unazungumza na roho ya vita. Ni mara ngapi unasema dhambi za wengie na wakati kila mmoja anazo dhambi zake, mimi lazima nitazame dhambi zangu na zile za wengine watafikiria wao,  kwa maana hiyo ni  kufunga mdomo.

Tuna tabia ya kutaka kuharibu wengine

Hata hivyo kwa kufafanua zaidi Papa amesema kwa kawaida namna yetu ya kutenda ndani ya familia, katika mitaa na nafasi ya kazi ni namna ya kutenda vita, kwa  kumwaribu mwingine, kumchafua mwingine. Lakini hiyo si tabia ya upendo, hiyo siyo tabia ya  amani ya kweli ambayo tunaiomba katika sala. Tunapofanya hivyo hakuna Roho Mtakatifu hasa inapojitokeza katika nafsi ya kila mmoja. Kwa haraka ni tendo la kuhukumu mwingine. Awe mlei, awe kuhani, awe mtawa, askofu, awe Papa ni wote kwa pamoja ndani mwake kuna kishawishi cha ibilisi kwa ajili ya kufanya vita!

Zawadi ya Roho Mtakatifu

Ikiwa ibilisi anafanikiwa kuwezesha vita ndani mwetu na kuwasha ule moto  yeye anafurahi sana kwa sababu hana kazi nyingine ya kufanya. Kaniz hiyo amwaachia sisi wenyewe ili kujiharibi mmoja na mwingine. Ni sisi tunaendeleza vita mbele, uharibifu awali sisi binafsi kwa maana ya kuondoa upendo ndani mwetu na baadaye dhdi ya  wengine.  Na hii Papa Francisko amebainisha, ipo kwa dhati tabia ya kuchafua wengin,  ni mbegu ambayo shetani ameweka ndani mwetu.  Na kwa kuhitimisha Sala ya mwisho amsema ni  kuomba amani ya kweli ambayo ni zawadi ya Roho Mtakatifu huku tukitafuata kubaki na Bwana daima.

MAHUBIRI PAPA
09 January 2020, 12:38
Soma yote >