Papa Francisko wakati wa kutoa mahubiri katika Kanisa la Mtakatifu marta Vatican tarehe  14 Januari 2020 Papa Francisko wakati wa kutoa mahubiri katika Kanisa la Mtakatifu marta Vatican tarehe 14 Januari 2020  (Vatican Media)

Ni huzuni kuwa na wakristo wasio na msimamo na ushuhuda!

Ni huzuni kwa wakristo wasiokuwa na msimamo na makuhani wasiojibidisha na na konesha ushuhuda,matokeo ni kwenda mbali na mtindo wa Bwana,uthabiti wake na mamlaka yake.Ndiyo ufunguo wa maneno ya Papa Francisko katika mahubiri yake wakati wa Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta kwa watu wa Mungu tarehe 14 Januari 2020.Anahitimisha kwa maombi kwa Bwana ili watu wapate hekima pamoja na kuwa wavumilivu lakini watambue kujitenga na unafiki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yesu alikuwa nafundisha kama mwenye mamlaka. Injili ya Siku kutoka  Marko 1,21b-28)  inasimulia jinsi Yesu alivyowashangaza watu kwa mafundisho yake hekaluni na hisia za watu kumwona anavyotenda kwa mamlaka tofauti na waandishi wa wakati ule. Ni mlinganisho Papa Francisko uliomsaidia katika kufafanua tofauti zilizopo kati ya kuwa na mamlaka, yaani mamlaka ya undani kama ya Yesu, na lile zoezi la kufanya mamlaka lakini bila kuwa nayo mfano wa waandishi wanaoelezwa katika Injili. Papa Papa Francisko amebainisha hayo wakati wa mahubiri yake kwenye Ibaya ya Misa Jumanne tarehe 14 Januari 2020 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican kwa waamini. Papa anasisitiza kuwa waandishi pamoja na kuwa wataalam wa kufundisha sheria na kusikilizwa na watu, lakini watu hawa walikuwa hawana imani nao.

Mtindo wa Yesu ni wa kifahari

Je Yesu ana mamlaka gani? Papa kwa kujibu amesema, Mtindo wa Bwana tunaweza kusema ni ule wa kifahari, ambao Bwana anazunguka nao huku akifundisha, akiponya na akisikilizwa. Ni mtindo wa kifahari ambao unatoka ndani ya moyo na kuonekana kwa wengi. Je wanaona nini? Watu wanaona msimamo thabiti na uhalisi wa utendaji wake. Utendaji wake wenye msimamo halisi  ndiyo unajifafanua kama mtu mwenye kuwa na mamlaka. Yeye ni mwenye mamlaka  kwa maana anavyo tenda ni uhalisia na kutoa ushuhuda wa kweli. Kwa maana nyingine ni kusema kuwa mamlaka yanaonekana katika matendo ya kweli na utthabiti wa ushuhuda.

Waandishi, wachungaji wasio na msimamo ambao wanasema lakini hawatendi

Papa Francisko akiendelea na ufafanuzi wake zaidi amesema kinyume ni kwamba waandishi hawakuwa na msimamo na Yesu kwa upande mwingine anawaonya watu wafanye kile wanacho wambia, lakini siyo kile wanachofanya. Na kwa upande mwingine Yesu hapotezi fursa ya kuwakaripia dhidi ya tabia hii anasisitiza Papa. Hawa kwa bahati mbaya wameangukia kukosa msimamo wa kichungaji. Wanasema jambo na wanafanya lingine. Papa anabainisha, pia kwamba  katika Injili kuna matukio mengi, ambapo Yesu anaonekana akiwakemea, hata kuwaweka pembeni na wakati mwingine hawapatii hata  jibu lolote na wakati mwingine anawapa  tuzo. Na neno ambalo Yesu anatumia kudhibitisha utangamano huo wa ukosefu wa msimamo ni ‘unafiki’.  Kwa kuongeza amesema “ Ni rosari ya kufuzu!  Kwa ufafanuzi zaidi amesema: “Katika Sura ya 23 ya Matayo, Injili  mara nyingi inasema wanafiki kwa ajili ya hili,… wanafiki kwa ajili ya lile … kwa maana hiyo Yesu anawapa tuzo la ‘unafiki’.” Unafiki ni mtindo wa kutenda  hasa kwa wale ambao wana jukumu kwa watu na katika mktadha huu, ni  wahusika wa kichungaji, kwa maana hawana msimano, hawana ufahari na wala kuwa na mamlaka. Na watu wa Mungu ni wapole na wanavumilia. Wanavumilia wachungaji wengi wanafiki, wachungaji wengi wasio kuwa na msimamo ambao wanasema lakini hawatendi na wala hawana msimamo madhubuti.

Ukosefu wa uthabiti  ukristo ni kashfa

Papa Francisko akiwageukia waamini wa Mungu ambao wanavulimia sana, anajiuliza kama wanatambua kutofautisha nguvu za neema. Amefafanua hili kwa kutumia Somo la Kwanza linaohusu mzee Eli, kuhani, aliyekuwa akiketi kitini pake penye mwino wa hekalu la Bwana(1Sam. 1:9-20). Yeye alikuwa amepoteza mamlaka yote, isipokuwa alibaki na neema ya mpako  na neena hiyo ilibariki na kufanya miujiza kwa Anna ambaye alikuwa na uchungu sana na kusali ili aweze kuwa na mtoto. Na kwa maana hiyo, fikira za Papa zinamsukuma kutazama juu ya watu wa Mungu, hasa wakristo na wachungaji.

Wakristo wanaokwenda misa kila Dominika lakini wanaishi kama wapagani

Papa amesema , watu wa Mungu wanatambua kutofautisha mema kati ya mamlaka ya watu na Neema ya mpako. Ametoa mfano kwa wale ambao wanadhiaki wengine wanaokwenda kuungama. Lakini anatoa ushauri kwamba “tunapaswa kutambua kuwa tunakwenda kuungama kwa Mungu na kwa Yesu  basi na hiyo ndiyo hekima ya watu wetu ambao wanavumilia mambo  mengi ikiwa ni pamoja na  wachungaji wengi wasio kuwa na msimamo, wachungaji kama wale waandishi, hata wakristo ambao wanakwenda kila misa za Dominika lakini wanaishi kama wapagani.

Papa Francisko amebainisha kwamba watu wengine wanasema hiyo haifai na ni kashfa. Na kwa maana hiyo anaongeza kusema “ ni kwa jinsi gani inahumiza kuwa na wakristo wasio kuwa na msimamo na ambao hawaoneshi ushuhuda na wachungaji wasio kuwa madhubuti, msimamo na hawaoneshi ushuhuda wa dhati.” Kwa kuhitimisha anasema: “hii ni fursa njema ya kutafakari na kusali kwa Bwana”. Amewaombea wabatizwa wote ili waweze kuwa na mamlaka ambayo siyo  katika kuamuru na kujifanya wasikike na badala yakewawe madhubuti, kutoa shahidi na kwa maana nyingine amesema kuwa wapagani wa barabarani katika njia  za kuelelea kwa Bwana”.

PAPA-MAHUBIRI 14.01
14 January 2020, 13:05
Soma yote >