Vatican News
Katika Misa ya Papa Francisko Kanisa la Mtakatifu Marta walikuwapo mapare kutoka Eritrea wanaotoa huduma yao Italia na watawa wa Cottolengo kwa fursa ya miaka 50 ya utawa Katika Misa ya Papa Francisko Kanisa la Mtakatifu Marta walikuwapo mapare kutoka Eritrea wanaotoa huduma yao Italia na watawa wa Cottolengo kwa fursa ya miaka 50 ya utawa  (ANSA)

Papa:Paulo alikuwa ni mpenda sheria lakini mpole!

Katika Misa Baba Mtakatifu Francisko asubuhi tarehe 10 Mei 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican kwa kuongozwa na somo kutoka Matendo ya Mitume juu ya uongofu wa Paulo akiwa njia ya Damasko amefafanua juu ya thamani ya upole na ufunguzi wazi wa moyo katika kusikiliza sauti ya Mungu.

Na Sr- Angela Rwezaula- Vatican

Uongofu wa Mtakatifu Paulo akiwa katika njia ya Damasko, kwa kuitwa na sauti ya Bwana ni kuonesha kugeuza ukurasa mpya wa historia ya Wokovu katika kuwawezesha ufunguzi wazi wa  wapagani, yaani  wale ambao hawakuwa ni waisraeli. Na kwa neno moja ni kutaka kusema kwamba ilikuwa ni ufunguzi wa milango wazi kwa Kanisa zima la ulimwengu, ambapo ni ahadi ya Bwana na ambayo ni muhimu. Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 10 Mei 2019 amewakilisha kwa waamini somo linalojulikana sana la Matendo ya mitume ambapo anasisitiza kuwa linatokana  na uchaguzi wa Yesu kwa kubadili maisha ya mtu ambaye hadi wakati ule alikuwa ni mtesi wa Wakristo….

Baba Mtakatifu katika kiini cha mahubiri hayo, anasema ni sura ya Mtume wa Watu na ambaye anageuka kuwa kipofu kwa siku tatu bila kula wala kunywa, hadi anafika Anania aliyetumwa na Bwana ili aweze kumrudishia uwezekano wa kuona na kuanza safari ya uongofu na kutangaza neno akiwa amejazwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo Baba Mtakatifu anaonesha  hatua mbili hasa kwa kuwageukia kikundi cha watawa wa Cottolengo waliokuwapo katika Misa hiyo wakiwa na fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu wafunge nadhiri zao  na baadhi ya mapadre wa Eritrea wanaojikita kutoa huduma  yao kichungaji katika nchi ya Italia.

Paulo alikuwa wa dhati na mpenda kufuata sheria

Kwa kufafanua  juu ya Paulo  anasema, alikuwa ni mtu mwenye nguvu na anayependa sheria, wa Mungu  mtiifu wa sheria, lakini alikuwa mkarimu  na wadhati japokuwa na tabia ngumu aliyokuwa nayo anasisitiza Baba Mtakatifu! Kwanza kabisa ilikuwa thabiti kwa sababu alikuwa mtu wazi kwa Mungu ... Ikiwa yeye alikuwa anawatesa wakristo ni kwa sababu aliamini kuwa Mungu alikuwa anataka hivyo, anabainisha Baba Mtakatifu. Je  kwa nini? Na  kwa sababu gani ?, kwa kujibu anasema : “hakuna kitu”, kwa maana yeye  aliamini hilo tu. Ni bidii aliyokuwa nayo kwa ajili ya usafi wa nyumba ya Mungu, kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Yeye alikuwa na moyo uliokuwa wazi katika sauti ya Bwana. Na alihatarisha, akajihatarisha na kwenda mbele, amesema Baba Mtakatifu.  Na mwelekeo mwingine wa tabia yake ni kwamba, “yeye alikuwa mtu mpole, alikuwa na upole, hakuwa mtu mkaidi”.

Mkaidi, lakini si katika nafsi ya roho

Labda tabia yake ilikuwa ngumu, amefafanua Baba Mtakatifu , lakini si katika nafsi yake rohoni. Paulo alikuwa wazi kwa mapendekezo ya Mungu. Kwa nguvu zote alikuwa akifunga gerezani na kuua Wakristo, lakini mara moja aliposikia sauti ya Bwana akawa kama mtoto, yeye mwenyewe aliacha apelekwe! Akiwa kipofu aliacha apelekwa Yerusalemu, alifunga kwa siku tatu, anasubiri Bwana amwambie … Katika imani zote hizo, yeye alikuwa amebaki kimya, akisubiri sauti ya Bwana: “Nifanye nini, Bwana?”. Na yeye alikuwa anakwenda kwenye mkutano huko Damasko, na kumbe ni katika mkutano wa mtu mwingine mpole na alijiachia apewe mafundisho kama mtoto, alijiruhusu kubatizwa kama mtoto. Na baadaye anapata nguvu, je anafanya nini? Ni mkimya, anasema Baba Mtakatifu.

Alikwenda uarabuni kufanya nini?

“Alikwenda Uarabuni kusali, kwa muda gani, hatujui, labda miaka mingi, hatujui, anasema Baba Mtakatifu. Akifafanua juu ya upole na kujifungua katika sauti ya Mungu na upole anasema, “ni mfano wa maisha yetu, na mimi leo hii ninapenda kuzungumza juu ya hili mbele ya watawa ambao wanaadhimisha miaka 50 ya maisha ya kitawa”. “Asante kwa kusikiliza sauti ya Mungu na asante kwa upole”, Baba Mtakatifu amesema.

Hata hivyo upole wa wanawake wa Cottolengo umemsababisha kuwa na kumbukumbu  ya Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kwanza kwenye miaka  ya 70 ya kutembelea moja ya jengo ambalo  amethibitisha kuwa, kwa roho ya Mtakatifu  Giuseppe Benedetto Cottolengo, alikaribisha  watu wenye ugonjwa wa kiakili na walemavu kutoka ulimwenguni kote. Aidha ameelezea kwa jinsi gani alivyopita  kutoka  chumba kimoja hadi kingine akiongozwa na Mtawa, kama wale walikuwa wanamsikiliza leo hii  katika Nyumba ya Mtakatifu Marta na ambao  amasema “wanatumika katika  maisha yao pale miongoni mwa waliokataliwa”. “Bila uvumilivu wao na upole, isingewezekana kufanya kile wanachofanya”.

Karama ya kikristo kwa mdogo na mkubwa

Kuvumilia ndiyo ishara ya Kanisa. Baba Mtakatifu ametaka kuwashukuru hao wanaume na wanawake ambao wanahatarisha maisha yao na kwenda mbele, hata kwa kutafuta njia mpya za maisha ya Kanisa. Wao wanatafuta njia mpya.  Lakini hiyo baba siyo dhambi?  mmoja anaweza kuuliza. La, siyo dhambi! Baba Mtakatifu amesema na kwamba: “Tunatafuta njia mpya, ili kufanya yote yaliyo mema. Mkristo lazima awe na karama ya udogo na ukubwa” Na hatimaye ndiyo sala anayo mwelekeza Paulo kwa ajili ya kuomba neema ya kuwa na upole katika sauti ya Bwana na kwa ufunguzi wa moyo kwa Bwana ya neema ili tusiogope kutenda mambo makuu na kwenda mbele kwa kutunza yale tuliyo nayo na  kutunza vitu vidogo.

10 May 2019, 13:53
Soma yote >