Vatican News
Misa ya baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican Misa ya baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican  (Vatican Media)

Papa anasema moyo mgumu unapoteza uaminifu hadi kufikia kukashifu Bwana

Kusikiliza sauti ya Bwana ili usiwe na moyo mgumu au kukashifu Bwana,ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini wakati wa misa yake Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 28 Machi 2019.Aidha amekumbusha kuwa Mungu ni mwenye huruma ambaye anaendelea kutoa wito ili kumrudia kwa moyo wote

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wito wa  nguvu wa kumrudi Mungu ndiyo umesikika katika tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko ,Alhamisi tarehe  28 Machi 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta Vatican. Tafakari lake limeanzia katika Neno la Liturugia ya siku kwa maana hiyo ametoa angalisho la moyo ambao hausikilizi sauti ya Bwana na kupita siku, miezi hadi miaka na moyo unakuwa ardhi isiyo na maji na kuwa kavu na ngumu.  Aidha baba Mtakatifu anasema, iwapo moyo una jambo ambalo hautaki ni kulikataa na kukashifu Bwana. Katika Injili ya siku Yesu anasema wazi Baba Mtakatifu anabinisha kwamba: “Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu”; na hivyo anaongeza au hana utii na amepoteza uaminifu!

Ipo hatari ya kupoteza uaminifu

Baba Mtakatifu anaendelea kueleza kuwa mara nyingi sisi ni viziwi na hatusikilizi sauti ya Bwana. Kwa kutoa mifano anasema ni rahisi kusikiliza televisheni na masengenyo katika mitaa na hayo ndiyo daima yanasikilizwa. Bwana lakini anatoa ushauri wa kusikiliza sauti na siyo kufanya migumu mioyo. Katika sima la siku kutoka Nabii Yeremiha (Yer 7,23-28), anaelezea kwa dhati uzoefu huu wa Mungu mbele ya watu wenye vichwa vigumu ambao hawataki kusikiliza.Somo hili ya Yeremiha kwa hakika ni kama kusema kwamba  Bwana analalamika Baba Mtakatifu Francisko anaongeza. Bwana anaagiza watu wasikilize sauti yake na kutoa ahadi ya kufungamana naya daima kwamba:  “ninyi mtakuwa watu wangu”.Lakini hawakusikiliza, wala kutega sikio lao, bali walikwenda kwa mashauri yao wenyewe, na kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya, wakaenda nyuma wala si mbele.

Baba Mtakatifu kutokana na somo hili anaongeza kutoa mfano: Bwana ahesabu: yote kwa maana yeye yuko pale anasubiri. Katika Somo la kwanza Mungu kwa dhati anakumbuka: Tokea siku ile baba zenu walipotoka katika nchi ya Misri hata leo, nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu ninyi, nikiamka mapema kila siku na kuwatuma. Lakini hawakunisikiliza, wala kutega sikio lao; bali walifanya shingo yao kuwa ngumu; walitenda mabaya kuliko baba zao. Nawe utawaambia maneno hayo yote; lakini hawatakusikiliza; nawe utawaita; lakini hawatakuitikia. Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya Bwana, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali vinywa vyao. Ni kusema kwamba  hawakuwasikiliza , badala yake walikuwa na kicha kigumu zaidi ya mababu zao. Aliwaeleza yote hayo lakini hawakumsikiliza na kwa maana hiyo anahitimisha akiwa na huzuni kwamba ushuhuhuda wa kifo, kwa  maana uaminifu ulikuwa umetoweka.

Mifano ya mtu kukosa uamaminifu

Watu wasio na uaminifu, ambao wamepoteza maana ya uamanifu, ndiyo swali ambalo Kanisa leo hii linatoa kwa kila mmoja: je mimi nimepoteza uamifu kwa Bwana? Itakuwa vizuri kijiuliza kwa maana Kwaresima inasaidia hili , ili kuweza kuweka moyo sawa. Kusikiliza sauti ya Bwana leo hii ni mwaliko wa Kanisa. Na Yesu anasema Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu. Hayo ndiyo yaliyomtokea Yesu  kwa watu wake, anasema Baba Mtakatifu kwa kutafakari Injili ya Siku ya kutoka Luka 11,14-23, ili kuwafanya waelewe ni nani Bwana. Yesu alikuwa anafanya miujiza, anaponya wagonjwa, kwa kuwafanya waelewe alivyo kuwa na uwezo wa kuponya hata roho za mioyo yote. Lakini hawa waliendelea kuwa na ubishi na kumwambia: “ Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo anaye fukuza pepo”. Baba Mtakatifu anabainisha jinsi ya kumdharau Bwana ilikuwa ndiyo hatua karibu ya mwisho wa kumkataa Bwana. Kwani walikuwa hawasikilizi, hadi mioyo yao ikawa migumu na baadaye kumdharau. Hatua ya mwisho ndiyo inakosa na ambayo hakuna kurudi nyumba na ambayo ni kashifa dhidi ya Roho Mtakatifu nayp inaonekana katika maneo ya Yesu mwisho wa Injili hiyo.

Yesu anajaribu kuwashawishi, lakini hawataki… na mwisho kama alivyo hitimisha Nabii Yeremiha umaminifu imetoweka na Yesu anahitimisha na sentensi ambayo inaweza kutusaidia. Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu.  Ni lazima kufikiria moyoo wetu kama uko kwa Yesu au mbali,ni mwaminfu au wenye utiii au umepoteza imani? Kila mmoja afikiri, katika Ibada ya Misa na wakati wa siku nzima”, amehimiza Baba Mtakatifu. Ni lazima kufikiria kidogo je imani yangu ikoje? Katika kumkataa Bwana natafuta sababu au dharau ya kukataa Bwana? Usipoteze matumaini.  Kwa kufuata maneno mawili ya “ uaminifu umetoweka na Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu yaweze kutoa  matumaini hata kwetu sisi. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena amewaalika waamini wamrudie Bwana kama shangilio lisemavyo "nirudieni mimi kwa moyo wako wote asema Bwana kwa maana mimi ni mwenye huruma na rehema".

Hiki ni kipindi cha Kwaresima, ni kipindi cha rehema ya Bwana, mrudie Yeye

Baba Mtakatifu anasema, ndiyo moyo wako ni mgumu kama jiwe, na mara ninyi umekuwa na dharau na kukataa, lakini bado kuna muda unapewa na Bwana akisema: "Nirudieni kwa moyo wote, anasema Bwana kwa maana mimi ni mwenye heruma na rehema, na wakati huo huo  nitasahau yote" amesisitiza Baba Mtakatifu! aidha ameongeza kusema:la muhimu wewe rudi tu. Ndiyo suala msingi ambalo Bwana anataka kuhimiza, kwa maana anasahau yote yanayobaki. Na hiki ni kipindi cha huruma, ni kipindi cha rehema ya Bwana kwa maana hiyo ni wakati sasa wa kumfungulia miyo ili yeye apate kuja kwetu, amehitimisha Baba Mtakatifu Francisko!

 

28 March 2019, 13:00
Soma yote >