Papa anaomba ujiuliza swali:je wako ni mgumu na uliofungwa? Je unaacha  moyo wako ukue au unaogopa kukua? Papa anaomba ujiuliza swali:je wako ni mgumu na uliofungwa? Je unaacha moyo wako ukue au unaogopa kukua?   (Vatican Media)

Papa:Mambo mabaya katika maisha ya mkristo ni ugumu wa moyo,ukaidi na udanganyifu!

Hitimisho la tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Januari 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican, anaomba nguvu ya Roho Mtakatifu ili atuangazie na pasiwepo hata mtu yoyote mwenye kuwa na roho ya ugeugeu, moyo mgumu, unyonge;ukaidi ambao unapelekea ukiburi na katika uitikadi; udanganyifu na kuishia katika maisha ya kubahatisha

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hai. Hii ni lugha ngumu na ni ujumbe wa kuhimiza umakini ambapo Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri ya siku katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 17 Januari 2019, ameweza kutafakari Somo la Wahebrania 3,7-14. Ni somo linalojikita kuelezea jumuyia ya kikristo katika mantiki zake zote, kuanzia mapadre, watawa maaskofu, ambapo kwa wote hata leo hii ipo hatari ya kuangukia katika moyo mbovu.

Baba Mtakatifu ameuliza swali, je ushauri  wa barua hiyo ina maana gani?

Kwa kufafanua zaidi ametoa maneno matatu kutoka katika barua ya Somo la siku ili kuweza kusaidia kutambua, na mamaneno hayo ni: ugumu,ukaidi na udanganyifu. Moyo mgumu ni miyo uliofungwa na ambao hautaki kufunguka, unaweka kizingiti na kuufunga kabisa. Katika maisha inawezakana ikatokea kutokana na dhambi nyingi ambazo hijitokeza, kwa mfano  hata uchungu kwa sababu ngozi ya mwili uhisi ngumu Baba Mtakatifu amethibitisha. Kwa kutoa mfano anasema hali hiyo ilijitokeza kwa mitume wa Emau, hata kwa Toma. Na yeyote anayebaki katika hali hiyo ni tabia mbaya na mnyonge wa moyo na kigeugeu.

Tunaweza kujiuliza je moyo wangu ni mgumu na uliofungwa? Je ninaacha moyo wangu ukue? Au ninaogopa kukua? Tunajiuliza hayo kutokana na  kwamba katika maisha ni kukua daima yapo  majaribu na matatizo tangu utoto wetu. Tunajifunza kutembea tangu tukiwa wadogo kwa kuanguka, hata wakati wa kutambaa kabla ya kutembea wakati mwingine ni  kuanguka! Katika hali hiyo ni kuonesha hali ya kukua. Ugumu:Baba Mtakatifu akifafanua juu ya ugumu amesema hata hiyo ni sawasawa na kujifunga. Na kwa kila yoyote anayebaki amefungwa ina maana ni mnyonge wa moyo Na kuwa na unyonge wa moyo nayo ni tabia mbaya ya ukristo, kwa maana anakosa ujasiri wa kuishi hivyo anajufungia katika unyonge wake.

Wakristo wengine ni wakaidi na wenye kiitikadi, kiburi na majivuno

Katika Barua ya Wahebrania pia imeandika kwamba: “Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi”. Kwa kufafanua anasema  ugumu huo ndiyo ulikuwa dhidi ya   ya Mtakatifu Stefano na ambapo baadaye wao walimpiga mawe bila huruma. Ukaidi ni kuwa na kichwa kigumu cha kiroho, moyo wa ukaidi, moyo ulifungwa katika mawazo binafsi , na mboa haufungulii kamwe Roho Mtakatifu. Na ndiyo kielelezo cha kuonesha wenye kuwa na mitindo ya kiitikadi, hata wenye kiburi na majivuno Baba Mtakatifu amesisitiza!  

Itikadi ni ukaidi. Neno la Mungu, ni  Neno la  Roho Mtakatifu  na siyo itikadi. Ni maisha ambayo yanakufanya ukue daima na kwenda mbele hata kwa kujifungulia moyo ishara za Roho na  ishara za nyakati. Lakini ukaidi ni kiburi, ni majivuno. Kuwa na kichwa kigumu ni jambo baya sana, baba Mtakatifu amesisitizana. Kwa maana ni ile tabia ya kujifunga moyo. Ni kusema wenye kuwa na ubaridi ni wale wenye kuwa na itikadi.  Swali la kujiuliza je mimi nina kichwa kigumu? Na kila mmoja ajitafakari: Je ninao uwezo wa kusikiliza wengine? Je ninao uwezo wa kusema kile ninachofikiria; Je ninao uwezo wa kuzungumza? Mara nyingi wenye ukaidi kamwe hawazungumzi na wengine kwa maana hujidanganya kwa kulinda daima mawzao yao , maana ni wenye kiitikadi. Itikadi kama hizi ninawatendea watu wa Mungu vibaya na ni jinsi gani zilivyo mbaya kutokana na kwamba zinafunga shughuli za Roho Mtakatifu, Baba Mtakatifu amesisitiza!

Wakristo wa  kunahatisha, watumwa wa kudanganywa

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari yake ameonesha kwa jinsi gani unaweza kuepuka usiangukie katika hatari za  kuwa na moyo mgumu,  moyo kigeugeu ambao ni udanganyifu. Udanganyifu ni dhambi anasisitiza na kuombeza kuwa ni ambayo ilitendwa na shetani, yaani mlaghai mkuu, mtaalimungu mkuu bila kuwa na imani,  bali aliyejazwa chuki, ambazo anataka kuingia nazo na kutawala katika moyo na kwa dhati yeye anatambua kufanya hivyo. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema  moyo kigeugeu na ambao unajiachia katika udhanganyifu na udanganyifu huo unampelekea mtu  kuwa mkaidi, kujifungia mwenyewe binafsi na mambo mengine mengi.

Katika udanganyifu,huo, unakutaka au uogoke au ubadili maisha na kutafuta mara kuishi kwa kubahatisha, lakini hiyo ni katika kukufanya kwenda hapa na pale na kuishi maisha mchanganyiko au maisha ya mkristo wa aina mbili.  Kwa kutumia neno kubwa Elia aliwambia watu wa Mungu kwamba ninyi mnachechemea kwa miguu miwili. Ni kuchechemea miguu miwili bila kuwa hata mmoja wa kuegemea!

Kwa maana hiyo inahitajika ndiyo kwa Bwana

Maisha yao ni kubahatisha Baba Mtakatifu anasisitiza na kusema kuwa wengine utakuta wanasema kuwa mimi ni mkristo na wanafuta Bwana, lakini hawamruhusu aingie. Ni wenye uvuguvugu na wanakwenda mbele daima kwa kubahatisha tu, hao ndiyo wakristo wa kubahatisha Baba Mtakatifu amebainisha. Hata kama  Bwana anatufanya tutambue njia, hata kwa amri zake, hata kwa njia ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, lakini wengine bado wanapendelea mwambo mengine mengi ya kwenda kutafuta njia mbili wakichechemea miguu yote miwili.

Anahitimisha kwa kusema, Roho Mtakatofu atuangazie ili pasiwepo na mtu mwenye roho ya ugeugeu. Moyo mgumo ambao unapelekea unyonge; moyo wa ukaidi ambao unakupeleka ukiburi na kukupelekea katika uitikadi; moyo unaovutika na kupendelea utumwa wa udanganyifuna ukaishia kuwa mkristo wa kubahatisha.

17 January 2019, 14:09
Soma yote >