Maaskofu Zimbabwe:Tubaki na umoja na uchaguzi si vita kati ya marafiki na maadui
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Maaskofu wa Zimbabwe katika barua yao ya kichungaji inayojikita kugusia mada ya uchaguzi mkuu, kwa kupiga kura itakayofanyika tarehe 23 Agosti 203 wanabainisha kwamba: “Uchaguzi ujao, unaofafanuliwa kuwa muhimu, wenye msimamo na wenye maamuzi, lazima usitugawanye kama taifa.” Kwa njia hiyo wapiga kura wanaalikwa kumchagua Mkuu wa Nchi, wajumbe wa Baraza na Seneti na wawakilishi wa mashirika ya ndani. Zimbabwe bado inateseka kutokana na urithi mzito wa Rais wa Zamani Robert Mugabe, Baba wa uhuru wa taifa, aliyeondolewa madarakani mnamo mwaka 2017 baada ya miaka 37 ya mamlaka bila kupingwa. Katika nafasi yake mnamo 2018, Rais wa sasa alichaguliwa, Emmerson Mnangagwa, wa chama cha Zanu-PF, ambacho kilikuwa ni chama cha Mugabe, ambacho alikuwa mshirika wake wa zamani. Uchaguzi hata hivyo ulipingwa na upinzani.
Maisha magumu na mifumko ya bei
Nchi hiyo pia inakabiliwa na mzozo wa kiuchumi na kijamii. Kulingana na Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Zimbabwe (ZCTU), ukosefu wa ajira umefikia 90%. Serikali inapingana na idadi hii, ikisema kuwa sehemu kubwa ya watu wanafanya kazi kwa njia isiyo rasmi. Kiwango cha mfumuko wa bei hivi karibuni kimepanda tena hadi 175%. Chama tawala, ambacho msingi wake wa uchaguzi wa vijijini unaonekana kuendelea kuwa waaminifu kwake, kina njia za serikali kuendesha kampeni zake za uchaguzi, huku mamlaka ikiweka vikwazo katika shughuli za uchaguzi za upinzani; Mnamo tarehe 6 Julai, wafuasi wanane wa mgombea urais mkuu wa upinzani, Nelson Chamisa, walikamatwa kwa kushindwa kuzingatia marufuku ya mkutano wa uchaguzi.
Maaskofu Zimbabwe wanatoa mwaliki wa jukumu la kupiga kura
Katika muktadha huo, Maaskofu wa Zimbabwe kwa hiyo wanatoa mwaliko wa kuchukua jukumu la kupiga kura. “Ujasiri! Simama… na uwajibike Hakikisha kuwa sauti yako inasikika kupitia sanduku la kura” wanahimiza. Kwa kuendelea wanabainisha kuwa: “Sote tuwe wananchi wawajibikaji ambao watakumbukwa kuwa wanaume na wanawake wa kizazi hicho ambao walikuwa wamoja kiasi kwamba tofauti zao za kiitikadi haziwezi kuwagawanya. Ikiwa kulikuwa na chochote, walishikamana wakati wa kusherehekea umoja wao katika utofauti.”
Maaskofu wanahimiza kuungana na sio kugawanyika
Maaskofu wa Zimbabwe wanakumbusha wapiga kuwa aidha kuwa “Uchaguzi sio wa vita kati ya marafiki na maadui. Tukiletewa chaguzi, zinatokana na itikadi tofauti zinazoshikiliwa na vyama vya siasa, sio kwa sababu kuna maadui walioapa. Sisi ni watu wamoja, Wazimbabwe, tumegawanyika na hivyo tunaanguka, lakini kwa umoja tunasimama kidete.” Hatimaye, ujumbe wao unatoa mwaliko wa matumizi ya uwajibikaji ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, ili kuepuka hotuba na lugha zinazochochea chuki.