UFUNGUZI WA MKUTANO  XX WA  AMECEA, KATIKA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA DSM TANZANIA– 10 JULAI 2022. UFUNGUZI WA MKUTANO XX WA AMECEA, KATIKA UWANJA WA BENJAMINI MKAPA DSM TANZANIA– 10 JULAI 2022. 

EMECEA:Sr.Rosalia Sakayombo,ACWECA na AMECEA ni ndugu kushirikiana bega kwa bega

Rais wa Umoja wa Watawa Afrika Mashariki na Kati ACWECA alipongeza AMECEA kwa ushirikiano katika majumu yao.ACWECA inathamini na inaendelea kushirikiana na AMECEA katika mipango kadhaa hasa akataja miwili:kutekeleza Mpango wa Kutunza Watoto wakatoliki (CCC).Mpango huu unahamasisha mgawanyo wa majukumu katika kulea watoto katika Kanda yao.Pili ni Mchakato wa maandalizi ya Sinodi ya 2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hivi Karibuni, umefanyika mkutano Mkuu wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Masharishi AMECEA, kati ya wengi waliopata kuzungumza mbele ya ushiriki mkubwa alikuwa ni Rais wa Umoja wa Watawa katika Afrika Mashariki, (ACWECA)Sr. Rosalia Sakayombo, RSHS. Katika ujumbe wake wa mshikamano alionesha furaha na heshima kwake kuhutubia ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano huo mkuu wa AMECEA uliofanyika katika jiji zuri la Dar es Salaam Tanzania.  Alitoa salamu za amani na mshikamano kutoka kwa ACWECA.  Sr Rosalia alielezea jinsi ambavyo ACWECA inawakilisha  na Masista zaidi ya 30,000 wakatoliki walioenea katika nchi 10 zinazozungumza Kiingereza za Afrika Mashariki na Kati. Nchi hizi ni: Eritrea, Ethiopia, Kenya; Malawi; Sudan Kusini; Sudan; Tanzania; Uganda; Zambia na Zimbabwe. Kwa wale ambao hawakuwa wanaifahamu ACWECA, alisema ni jinsi gani mara moja wangegundua kuwa mbali na Zimbabwe ambayo ni mwanachama mshirika, nchi nyingine zote ni nchi za AMECEA na ndivyo walivyo hata watawa wa AMECEA.

WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA
WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA

Kwa hakika ndilo jina walijulikana kwa mara ya kwanza kama Masista wa AMECEA, kwa vile ilikuwa nje ya Mkutano Mkuu wa AMECEA mnamo 1973 na ndipo wajumbe hao walipokuja na wazo la kuwa na bodi ya kikanda ya Matawa wakatoliki, na mnamo mwaka 1974 wakazaliwa. Tangu wakati huo, ACWECA inashirikiana kwa karibu na AMECEA katika shughuli na programu zake mbalimbali za kichungaji zinazolenga kuimarisha uwezo wa Masista Wakatoliki kufikia maono yake ya kuwawezesha wanawake waliowekwa wakfu kwa ajili ya uinjilishaji wa kina katika kanda zao, zote zikiratibiwa kutoka katika Sekretarieti yake yenye makao yake makuu Jimbo la Ngong kilometa chache nje ya jiji la Nairobi nchini Kenya. Sr Rosalia alionesha furaha kuwapo hapo kushuhudia mkutano wa kihistoria wa AMECEA na kwamba matunda ya AMECEA yanajieleza yenyewe hasa kwa “Kuzaliwa kwa Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo; Kuimarika kwa ubora wa Elimu; kuimarishwa kwa huduma za Kichungaji na afya katika Kanda yao, kwa kutaja machache tu”.

WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA
WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA

Sr. Rosalia vilevile alisisitiza  kwamba mkutano huo Mkuu uliikuwa wa kipekee kwa sababu ulifanyika wakati mwafaka wa kihistoria ambapo roho ilimwongoza Mama Kanisa katika maandalizi ya Sinodi ya 2023 kwa ushirika, ushiriki na majadiliano katika roho ya Sinodi kama ilivyoitishwa na Baba Mtakatifu Francisko.  Kwa kufafanua zaidi alielezea kwa  kwa kutazama ukumbi pande zote aliona uthibitisho wa kweli, kwa maana uliowakilisha na Kanisa zima kuanzia na Maaskofu, Mapadre, watawa wa kike na kiume na Walei yaani uwakilishi wa wote uliokuwa ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere. ACWECA na AMECEA ni ndugu kutoka kwa Mama mmoja. Shughuli zao ni za ziada na zinaingia katika utume uleule wa lengo la Kanisa, alisistiza Sr. Rosaria na kwamba ni kuhamasisha kazi ya uinjilishaji katika Kanda. Kwa njia hiyo awe kuhani alisema anaongoza Misa au kutoa Sakramenti zozote za Kanisa; ikiwa sista anafundisha vijana au anatibu watoto katika kituo cha afya; awe Mkatoliki mlei ambaye anakusanya kodi kwa serikali yao au anaendesha biashara ya familia yake; wote ni katika kushiriki ubatizo mmoja na wote wamemeitwa katika majukumu sawa kuhusu kueneza ujumbe wa Injili na kushuhudia tunu za injili katika miito yao mbalimbali katika kanda zao.

WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA
WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA

Na ndiyo maana wao walikaribisha kwa shauku, uteuzi wa kaulimbiu ya Mkutano huo wa 20 wa AMECEA kuhusiana na  Athari za Mazingira kwa ajili ya Maendeleo ya Kibinadamu ambayo inaleta changamoto kwa wote. Sr Rosalia alisema kwamba kauli mbiu hiyo ilikuwa inawakumbusha jinsi ambavyo wote wana wajibu wa pamoja, na kuwaalika kwa kila nafasi zao mbalimbali, kukumbatia utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja , yaani  Mama Dunia; kwa kutambua kwamba kwa hakika Mungu ametupatia sisi sote rasilimali za kushirikishwa na kuwa mawakili ili watoto wote wa Mungu  walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ili waweze kuishi kwa heshima na Amani.  Sr. Rosalia alionesha furaha kubwa kwa ushirikiano ambao AMECEA inautoa kwa ACWECA kwa kadiri ya majukumu yao na kwamba ACWECA inathamini na inaendelea kushirikiana na AMECEA katika mipango kadhaa. Kwa kutaja kidogo alielezea mbili za ushirikiano ambao unapitia mipango.

WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA
WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA

Awali ya yote ACWECA inashirikiana kwa karibu na AMECEA katika kutekeleza Mpango wa Kutunza Watoto wakatoliki (CCC). Mpango huu unahamasisha mgawanyo wa majukumu katika kulea watoto katika Kanda yao. Mpango huu unatambua umuhimu na nafasi ya familia katika juhudi hiyo. Ni katika familia ambapo watoto hulelewa na kufundishwa maadili ambayo hutengeneza tabia ya uhusiano wa mtoto zaidi ya familia. ACWECA na AMECEA zote zimejitolea katika mpango huo ambao wanatarajia kuupanua na kujumuisha nchi zote za Kanda. Kwa sasa mpango huo unahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia na Malawi ni mshiriki mpya katika mpango na mipango mingine  ya kuhamasisha zaidi ya nchi hizo.

WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA
WAJUMBE WA AMECEA 10-18 JULAI 2022 DAR ES SALAAM TANZANIA

Pili ni Mchakato wa Sinodi ambapo Sr Rosalia alifafanua kuwa ni eneo ambalo ACWECA inafanya kazi kwa karibu na AMECEA. Mpango huo unahusisha nchi zote katika Kanda zao na wana shauku kwamba ushirikiano wao katika mchakato wa Sinodi utaimarisha uhusiano wao wa kufanya kazi na kuchangia katika Kanisa lenye ufanisi na uchangamfu zaidi katika Kanda Sr. Rosalia alisema kuwa pamoja na kuseheherekea mkutano huo, hakusahau kuonesha mafanikio ya AMECEA kwa miaka mingi, hasa kupongeza ushirikiano kati ya ACWECA na AMECEA, pamoja na washirika wengine katika Kanda na kwingineko. Kwa njia hiyo walikuwa pamoja ili kuendelea kuwa ishara ya matumaini kwa watu wa Mungu katika Ukanda huo wa AMECEA na kwingineko. Hatimaye Rais wa ACWECA, alipenda kuwakikishia ndugu maaskofu wa AMECEA ili kuendelea kuwaunga mkono na kushirikiana kama washirika katika shamba la mizabibu la Bwana la kana na kama kijiji cha kimataifa katika Laudato Si na kushukuru kama washirika sawa.

UJUMBE WA MSHIKAMANO WA RAIS WA ACWECA KWA AMECEA JULAI 2022
10 August 2022, 15:08