Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa AMECEA kuanzia tarehe 10 hadi 18 Julai 2022. Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa AMECEA kuanzia tarehe 10 hadi 18 Julai 2022. 

Tanzania ni mwenyeji wa Mkutano wa XX wa AMECEA 10-18 Julai 2022

Misa ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa AMECEA itafanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar Esa Salaam Tanzania mnmo Dominika tarehe 10 Julai 2022 na kuhitimishwa na misa katika viwanja vya Kituo cha Msimbazi,tarehe 17 Julai 2022.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baada ya miaka ishirini tangu Baraza la Maaskofu Tanzania, (TEC), kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA), kamati ya maandalizi jijini Dar Es Salaam Tanzania inafuraha na kuwahakikishia wajumbe wote kuwa wako tayari kukaribishwa washiriki wote katika  mkutano wa XX wa AMECEA. Mkutano mkuu umepangwa kufanyika Dar es Salaam,  kuanzia tarehe 10 hadi 18 Julai 2022 ambapo utafunguliwa kwa Ibada ya Misa Takatifu ambapo waamini wote wanaalikwa kuudhuria misa hiyo. Ingawa viwango vya UVIKO-19  vimepungua duniani kote hasa katika kanda nzima ikiwamo Tanzania, kamati ya maandalizi inayo  umakini kuhusu hitaji la kumbi kubwa kwa ajili ya kufungua na kufunga sherehe za Ekaristi Takatifu zitakazofanyika katika Viwanja vya Benjamin Mkapa,  Madhabau ya  Pugu na Msimbazi.

Mada ya mkutano Mkuu ni kuhusu utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja

Mkutano Mkuu  utakaoongozwa na Mada juu ya Utunzaji wa Mazingira  Nyumba yetu ya pamoja na athari zake kwa ajili ya  Maendeleo ya Binadamu  utafanyika katika Kituo cha Mikutano Kimataifa cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 11-13 Julai 2022. Wakati shughuli zinazohusiana na masuala mengine  ya maaskofu zitafanyika katika  Kituo cha Wakapuchini, Msimbazi, kuanzia tarehe 15 hadi 17 Julai 2022. Kulingana na ripoti zilizotolewa mapema na kamati ndogo zote ambazo ni pamoja na liturujia, vifaa, usafiri, ukarimu, ulinzi na upishi, vyote vimepangwa kwa ajili ya tukio hilo.

Mahitaji ya kufika kwenye mkutano huo wa AMECEA TANZANIA

Nchi zote wanachama wa AMECEA hazihitaji visa isipokuwa nchini Ethiopia, Sudan, Eritrea na Djibouti kwani Tanzania ni mwanachama wa COMESA na SADC. Hata hivyo, wale wanaokuja kutoka nchi za nje ya eneo hilo wanahimizwa kuangalia mtandaoni ili kujua ikiwa wanahitaji kutuma ombi kabla ya kusafiri au ikiwa Visa inaweza kutolewa wanapowasili.

Makaribisho na Hali ya hewa

Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi pia inapanga kuweka dawati maalum kwa ajili ya kuwakaribisha wajumbe mara tu watakapowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambaragwe Nyerere kwa lengo la kufuatilia kwa haraka michakato yoyote inayohusu Visa na usafiri wa kwenda wanapotakiwa. Pia, wajumbe hao wanahimizwa kutambua kuwa hali ya hewa ya Dar es Salaam ambayo kwa nyakati hizi ni ya joto kiasi, inaweza kushuka hadi nyuzi joto 18-24 katika mwezi wa Julai. Kwa njia hiyo inatakiwa kuhakikisha kuwa umesasishwa na chanjo za UVIKO -19 kabla ya kusafiri. Kufuatilia mahitaji yote ya ndege na waendeshaji usafiri pamoja na mahitaji yoyote katika  sehemu ambayo unakwenda ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, uthibitisho wa chanjo, upimaji, au kuweka karantini kwa mujibu wa maelezo ya kukaribisha.

Jimbo Kuu Katoliki kuwapokea wageni kuanzia tarehe 8 Julai

Katika taarifa ya awali, pia ilithibitisha kwamba Kansela wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padre  Vincent Mpwaji alisema kwamba Jimbo Kuu  Katoliki linatarajia kuanza kuwapokea maaskofu hao na wajumbe wengine kuanzia tarehe 8 Julai 2022. Aliyasema hayo katika kikao ambacho pia kilifanyika katika viwanja vya Kituo cha Msimbazi jijini Dar es Salaam ambacho kiliwaona Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu, viongozi wa parokia na wakuu wote wa maparokia, wakijadiliana kuhusu mipango ya Jimbo Kuu ikiwa ni pamoja na maandalizi ya kuelekea Mkutano wa AMECEA. Padre  Mpwaji wakati huo  alisema kuwa kila Parokia ndani ya Jimbo Kuu hilo ilibidi ijiandae kikamilifu kuwapokea wageni hao na kuwasindikiza katika kipindi chao cha kukaa Dar es salaam hadi siku ya kuondoka kwao.

Katibu Mkuu wa AMECEA

Naye Padre Anthony Makunde, Katibu Mkuu wa AMECEA, aliyekutana na Kamati ya Maandalizi kwenye Kituo cha Msimbazi, mnamo tarehe 27 Mei 2022, alikuwa ameshukuru kamati ya maandalizi kwa kujitolea kwao, kwamba mkutano huo ni wa kuwaleta pamoja Makardinali, Maaskofu, kaka na dada kutoka nchi tisa ambazo zinajumuisha wanachama wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA), lakini pia wajumbe Umoja wa Mashirika ya Kitawa (ACWECA )kukusanyika pamoja japokuwa wakafanya mkutano wao kwa njia ya Mtandao.

Mikutano mingine ya hivi karibuni iliyotangulia huko Malawi na Ethiopia

Tanzania ndiyo yenye Baraza kubwa zaidi la maaskofu katika ukanda wa AMECEA, lenye majimbo 34. Malawi ambayo ni ndogo yenye majimbo 8 ilikaribisha Mkutano  kama wa aina hiyo mnamo 2014 na mnamo 2018, mkutano mwingine ulifanikiwa nchini Ethiopia, yenye  majimbo  12  tu. Kwa hiyo Padre Makuenda alikuwa akitaka kusisitiza kwamba watu wengi wana matarajio makubwa kwa Tanzania kuandaa na kufanya vizuri zaidi, na wakati huo huo alizitaka kamati hizo kufanya kazi kwa bidii zaidi katika wiki zilizokuwa zikisalia. Hatimaye tuko katika wiki ya mwisho wa maandalizi na mapokezi!

Shirikisho la mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki la nchi nane za Afrika Mashariki ambazo ni Ethiopia (1979), Eritrea (1993), Kenya (1961), Malawi (1961), Tanzania (1961), Zambia (1961), Sudan (1979), Uganda (1961), na wakati Somalia (1995) na Jibuti (2002) wanakaribishwa. Makao yake makuu ya shirikisho hilo yapo Nairobi.  Shirikisho hilo lilianzishwa mnamo mwaka 1961 ambapo 2021 ilifanya Jubilei ya kutimiza miaka 50 ya kiungo hiki kikuu na  sherehe iliadhimishwa huko Uganda; Pamoja na mengine Shirikisho hili linaundwa ndani ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM).

Mkutano Mkuu wa AMECEA Tanzania 10-18 Julai 2022
WIMBO WA AMECEA KUHUSU MADA YA MAZINGIRA
05 July 2022, 12:15