Siku ya vijana ni shughuli inayowaruhusu vijana kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi kukusanyika pamoja kufurahi katika Bwana. Siku ya vijana ni shughuli inayowaruhusu vijana kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya nchi kukusanyika pamoja kufurahi katika Bwana.  

Ivory Coast:Zaidi ya vijana 3,000 jimbo la Yopougon washiriki siku ya vijana

Kuanzaia tarehe 27 hadi 30 Agosti 2021 katika Parokia ya Mtakatifu Lautent jimbo katoliki la Yopougon nchini Ivory Coast vijana 3,000 wameadhimisha siku ya vijana kijimbo.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Vijana Katoliki wa jimbo la Yopougon nchini Ivory Coast walikusanyika pamoja tangu tarehe 27 hadi 30 Agosti 2021 katika parokia ya Mtakatifu Laurent huko Yopougon Kouté ili kufanya uzoefu wa kiutamaduni kwa ajili ya shughuli ya Siku ya Vijana kijimbo ambapo walishiriki vijana zaidi ya  3,000.

Shughuli ambayo haikuweza kufanywa mwaka jana kwa sababu ya UVIKO-19, lakini ambayo imekuwa ikilenga kuwa mfumo wa mkusanyiko wa karibu na Askofu wao, kwa ajili ya malezi ya kiroho, kwa ajili ya mkutano, kuishi udugu na kwa kubadilishana mawazo na vijana wengine kati yao. Katika  toleo hili la tisa, kaulimbiu iliyochaguliwa kuongoza ilikuwa ni: “Bwana Yesu, aliye kweli katika hema, nisaidie kukuabudu mara nyingi”.

Kwa mujibu wa Padre Franck Hermann Soko, mchungaji wa idara  ya malezi ya vijana ya Jimbo Yopougon nchini Ivory Coast akifafanua tukio hilo alisema kuwa: "Siku ya vijana ni shughuli inayowaruhusu vijana kutoka sehemu mbali mbali na  kukusanyika pamoja kufurahi katika Bwana kwa kufanya uzoefu kubadilishana maoni mbali."

Akiorodhesha shughuli zilizofanyika katikati ya mkutano huo Padre  Soko alisema:“Tumekuwa na shughuli za kiutamaduni kama kufanya mashindano ya 'Miss Bikira' ambayo ni kweli, na mashindano ya 'Miss Esther', ikiwa inataka kuonesha usafi  ambao ni thamani ya Kanisa na jamii. Kuulikuwa pia tamasha ya kidini, walicheza na kupendekeza ujumbe, vile vile tulikuwa na mashindano ya kibiblia ili kuamsha mazoezi ya Biblia pia kuruhusu vijana wote waliopo kukariri maarifa ya kibiblia".

02 September 2021, 15:29