Economy of francesco:lengo ni  kutoa roho mpya kwa ajili ya uchumi kwa kutengeneza michakato ya ujumuishaji. Economy of francesco:lengo ni kutoa roho mpya kwa ajili ya uchumi kwa kutengeneza michakato ya ujumuishaji. 

Italia:Uchumi wa Francisko ni kutoka katika ‘umimi’na kuingia wa'pamoja'

Shule ya kiangazi ya 'Economy of Francesco' huko Gubio iliyoanza tarehe 29 Agosti iliyopita ilihitimishwa Jumamosi tarehe 4 Septemba 2021 ambayo imeongozwa na kauli mbiu ile ile ya“kufikiria kwa upya uchumi mpya inaoshirikisha kuanzia na mali ya pamoja”.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni neno sisi ambalo kwa namna fulani limeonekana kufupisha njia ambayo ‘The Economy of Francesco’, yaani ‘Uchumi wa Francisko’ unafuata ambayo ni harakati iliyoundwa na wajasiriamali vijana na wachumi, lenye lengo la kutoa roho mpya kwa ajili ya uchumi kwa kutengeneza michakato ya ujumuishaji. Papa pia alisema haya wazi kwenye ujumbe kwa njia ya video wakati wa tukio la mkutano wa kimataifa mnamo Novemba iliyopita kwamba “kwa baadhi kuna upendeleo wa kuona mbingu hatimaye hakuna wengine bali mimi tu na kumbe ni vema tujifunze kukomaa ule mtindo wa maisha ambao tunajua kusema sisi yaani kwa pamoja”. Hili ndilo hata hivyo Neno ambalo limejirudia mara kadhaa katika mahojiano na mmoja wa washiriki katika Shule ya kiangazi iliowaona washiriki wapatao 35 kutoka nchi 14 ulimwenguni, huko Gubbio nchini Italia kuaniza tarehe tarehe 29Agosti na kuhitimisha tarehe 4 Septemba 2021. Tukio hilo ni mojawapo ya mikutano inayofanyika katika maeneo makubwa yenye kukaribisha mikutano na mipango ya Uchumi wa Francesco.

Valentina Brandi, mwenye umri wa miaka 32, ameolewa na familia ya watoto 2 mwenye elimu ya (PhD) ya uchumi, ameelezea uzoefu mzuri sana aliouishi kwa kipindi hicho cha shule ya kiangazi. Katika maelezo yake amebainisha jisni ambavyo siku hizo zinaoneshwa na nyakati rasmi na zisizo rasmi, wakati ambao uzoefu na maoni ya mtu yameweza kupitishwa.  Uzi mwekundu wa shule ya kiangazi ambao umeonesha ni kwa jinsi gani inawezakana kutoka katika utamaduni wa umimi, wa shughuli za kiuchumi zinazohamasisha masilahi ya kibinafsi, hadi kupitisha zile shughuli za utamaduni wa sisi yaani wa umoja na ambao ndiyo uchaguzi wa kiuchumi wa kushirikisha.

Kuwa na washiriki wa kozi hiyo kutoka sehemu mbali mbali za nchi ni mojawapo ya mambo muhimu ambayo Valentina Brandi aliangazia kwa dhati. Utajiri pia ulitokana na ukweli kwamba mtu hawezi kujilinganisha kwa hoja zake za kinadahari tu, lakini zaidi ya yote ni juu ya uwezekano wa kubadilishana maoni ya mtu mwingine juu ya mada ambazo ziliangaliwa kama vile za ustawi wa pamoja, mali kama wema wa uhusiano na hali ya uaminifu. Vile vile katika shule ya kiangazai walishughulikia kupitia mihadhara na kazi za kikundi na ndiyo maana ya kuwa sehemu ya ushiriki. Kulikuwa na mambo mengi sana hasa ya utafiti, kwa mfano katika uchumi wa kitabia, “behavioral economics”, utafiti umesonga mbele juu ya nyanja ya akili ya uchumi na ukweli kwamba kimuundo, katika njia ya maisha ya kuuona ulimwengu, unaokuwa na mwelekeo wa kuhisi kama ‘sisi’ badala ya ‘mimi’. Kipengele hiki kimechukuliwa na uchumi wa familia hasa katika uhusiano wa mama na mtoto, kwa mfano, mtoto mchanga ni kitu kimoja na mama mwanzoni, lakini polepole kadiri anavyokuwa yeye hugundua kuwa naye anao ubinafsi wake. Kwa mfano huo, Bi Brand pamoja na wezake amethibitishwa kuwa waligundua umuhimu wa 'kuhisi kufanya kuwa sehemu ya' katika kushiriki pamoja kwa sababu bila 'kuhisi kuwa sehemu ya ushiriki', chaguzi kadhaa za kushirikishana haziwezi kufanyika kamwe.

Bi Brand kuhusiana na mapendekezo halisi ameelezea kwamba Shule ya kiangazi iliundwa kutoa nafasi za kushiriki kwenye utamaduni wa kuwa ‘sisi’ katika kiwango cha uchaguzi wa kiuchumi. Moja ya mantiki ambayo inapaswa kuendelezwa katika maisha ya kila siku, katika uhusiano tunaouanzisha kama wachumi, wafanyakazi, wafanyabiashara na wengine. Kwa maana hiyo lazima kufanya kazi katika mipango kadhaa iliyo juu. Uchumi wa Francisko, kiukweli, unalishwa na nyakati mbili, wa kwanza ni ule wa kutafakari na mwingine niwa matendo ambao unakwenda sambamba. Kwa kutoa mfano, Dk, Brandi alisimulia juu ya mchango anaoutoa katika sekta ya afya, hasa katika uwanja wa huduma za kijamii na afya, ili wawe karibu na uraia na inawezekana kutoka kwenye wazo la hali ya ustawi kibinafsi kwenda wazo la ustawi wa jumuiya nzima kwa kuwashirikisha raia katika huduma zenyewe na kwa ajili ya wa wenyewe.

06 September 2021, 15:54