Papua Guinea Mpya Papua Guinea Mpya 

Papua New Guinea:Matumaini ndiyo kitovu cha tamasha la kimataifa

Matumaini yamekuwa ni kitovu cha Filamu fupi kimataifa 2021 huko Papua New Guinea.Tamasha za Filamu fupi zimekusudiwa kama rasilimali ya kichungaji na zinaweza kutumika shuleni,parokia,taasisi na vikundi vya vijana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Limekuwa ni tumaini, ambalo linabaki hai hata wakati wa janga la UVIKO-19, ambalo limekuwa ni mada kuu ya Tamasha la Kimataifa la Filamu Fupi la 2021, ambalo lilifanyika tarehe 7 Agosti 7 iliyopita huko Papua New Guinea, katika mji wa Vision. Mbele ya Balozi wa Kitume nchini humo, Askofu Mkuu Giorgio Licini na wawakilishi wa sekta ya mawasiliano na elimu, hafla hiyo ilihudhuriwa na vijana wengi na ikiwakilisha kilele cha Semina za Elimu ya Vyombo vya Habari 2021, zilizofanyika katika miezi ya hivi karibuni. Shule na taasisi nane katoliki zimeonesha umoja na ubunifu mkubwa. Kilichojitokeza, kwa mujibu wa wataarifa hiyo ni kwamba “mawasiliano sio tu kutuma picha au kuwa na mtindo wa hivi karibuni wa simu za mikono, lakini ni zana yenye nguvu ambayo, ikiwa inatumiwa vizuri, inaweza kubadilisha maisha ya watu”.

Katika siku zote kuna hata kesho

Kila filamu fupi katika mashindano iliwasilisha kwa nguvu na uwazi kwamba “siku zote kuna kesho, ambayo ni, matumaini hata wakati mgumu, uliowekwa na umasikini, ukosefu wa ajira, vurugu, mizozo ya familia, kuomboleza, maumivu, mateso ya  akili”. Je ni kitu gani ambacho kinachoweza kuwa muhimu zaidi kwa vijana wetu katika ulimwengu wa leo ambacho ukuza akili inayokosoa na ambayo ni wepesi kugundua ukweli na haraka wa kutupilia mbali uwongo uliojaa, hasa, kwenye mitandao ya kijamii na katika ulimwengu wa matangazo?

Matumaini yamo kwa kila mmoja

Kwa sababu hiyo, alisema Padri Ambrose Pereira, Katibu wa Mawasiliano Jamii ya Baraza la Maaskofu wa Papua New Guinea kuwa  mawasiliano ni muhimu kwa sababu yanajumuisha kushiriki ujumbe wa matumaini na inawakilisha fursa ya kuinjilisha. “Matumaini yamo ndani ya kila mmoja, amesema mwanafunzi mmoja na kwamba lazima washirikishane na wengine na kufanya matumizi ya majukaa ya mitandao ya kijamii kuyaeneza.

Filamu fupi ni rasilimali ya kichungaji katika shule, parokia, vikundi vya vijana

Tamasha za Filamu fupi zimekusudiwa kama rasilimali ya kichungaji na zinaweza kutumika shuleni, parokia, taasisi na vikundi vya vijana. Kusudi lao ni kukuza kufikiria wazi na akili muhimu katika ulimwengu wa habari za kughushi na habari potofu.

10 August 2021, 15:36