Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Kinshasa, DRC Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Kinshasa, DRC 

DRC:Maaskofu walaani mashambulizi dhidi ya Kardinali Ambongo

Serikali inatakiwa kuchukua mambo mikononi mwao,kutambua na kuwaadhibu vikali wale waliohusika kwa sababu ya mashambulio yote dhidi ya Kanisa na ili yasirudiwe tena.Ni ombi kutoka Baraza la Maaskofu nchini Congo DRC baada ya mashambulizi ya vijana dhidi makazi ya Kardinali Ambongo,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Kishansa na matukio mengine dhidi ya Kanisa nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Maaskofu  wa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)wanaelezea kwa masikitiko na hasira kuhusu mashambulizi yaliyofanywa katika miezi hii kwa Kanisa katika Nchi yao. Hata hivyo Dominika tarehe Mosi Agosti 2021, makazi ya Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Kishasa yalilengwa na kikundi cha vijana wasiojulikana ambao walimdhiaki kadinali huyo kwa kauli mbaya za matusi na siku iliyokuwa imetanguliwa pia kulikuwa na shutuma za kukera kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Demokrasia na Maendeleo ya Jamii, Bwana Augustin Kabuya.  

Pamoja na mambo mengine, kiongozi wa kisiasa wa chama tawala alikuwa amewashutumu Kardinali Ambongo, pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu DRC (Cenco), Padre Donatien Nshole, kuwa wanataka kulifanya Kanisa liwe la kisiasa. Mashambulizi  hayo dhidi yanapaswa kuhusishwa na tofauti juu ya upangaji upya wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (Ceni) kwa kuzingatia uchaguzi wa urais wa 2023 ambao Kanisa lingetaka kujitegemea kisiasa na kujieleza kwa asasi za kiraia kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo.

Katika taarifa iliyoripotiwa na Redio Okapi, Baraza la Maaskofu wa Congo (Cenco) linazungumza juu ya tabia isiyowajibika huku wakiwaalika waamini kuwa makini sana na sio kushawishiwa na mtu yeyote. Baraza la Maaskofu (Cenco) pia linaonesha kusikitishwa na vitendo vya mara kwa mara vya uharibifu na wizi wa vitu vitakatifu ambavyo vimetokea katika miezi minne iliyopita dhidi ya makanisa na maeneo ya ibada (kwa jumla12) katika majimbo ya Mbuji-Mayi, katika Kasaï Mashariki.

Mashambulizi hayo yalilaaniwa kwa wa eneo hilo na askofu Bernard-Emmanuel Kasanda ambaye katika barua ya kichungaji iliyotolewa tarehe 26Julai 2021 anazungumza juu ya vitendo vibaya  na uhalifu mbaya ambao unastahili adhabu ya wakati unaofaa na ya kuwa mfano. Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu DRC (Cenco), vurugu hizi zisizokubalika za kushambulia uhuru wa dini na kujieleza, lakini pia ni ukiukwaji wa demokrasia. Ni hatua kubwa kurudi kwenye njia kuelekea sheria ambayo watu wa Congo wanatamani, wanasema, na kwa maana hiyo ndipo ombi la ombi lililoelekezwa kwa Serikali kuchukua mambo mikononi mwao, kutambua na kuwaadhibu vikali wale waliohusika kwa sababu ya mashambulio haya na ili yasirudiwe tena”.

03 August 2021, 15:25