Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiweka shada la maua katika kumbukizi la waathirika wa bomu la Atomiki la 1945 huko Hiroshima Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga akiweka shada la maua katika kumbukizi la waathirika wa bomu la Atomiki la 1945 huko Hiroshima 

Kumbukizi la Hiroshima na Nagasaki la bomu la atomiki

Kila tarehe 6 na 9 Agosti ya kila mwaka ni Siku ya kumbukizi ya mlipuko wa Bomu la Kinyuklia huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan.Katika afla hiyo,Pax Christ,imetoa wito kwa upya wa kuendeleza kwa haraka saini na kuridhia utekelezaji wa Mkataba mpya wa UN juu ya kupiga marufuku Silaha za Nyuklia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wito mpya umetolewa  wa kuendelea haraka na kutiwa saini, ili kuridhia na kutekeleza Mkataba mpya wa Umoja wa Mataifa juu ya kupiga marufuku Silaha za Nyuklia ambao mataifa 55 sasa yamesaini. Wito huo umezinduliwa na  chama cha 'Pax Christ' kwenye hafla ya kumbukizi la kulipuka kwa mabomu ya atomiki huko Hiroshima na Nagasaki, siku ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 6 na 9 Agosti. Makumi ya mamia elfu ya watu walikutana na kifo tayari wakati wa kulipuka kwa bomu na wengine wengi walikuja kufa baadaye au waliugua sana kutokana na mionzi yake. Wamekumbusha chama cha kitume cha Kimataifa cha ‘Pax Christ’, katika ujumbe wao kwa siku hii. “Kama wanaharakati wa amani, tunachukulia matumizi haya ya kwanza ya silaha za nyuklia kama moja ya hatari mbaya zaidi katika historia na wito wa ngunvu na haraka ya kuamka ambao ubinadamu haupaswi kusahau kamwe!”

Mkataba umeanza kutumika tangu Januari 22 mwaka huu

Kutokana na fursa hii shirika Katoliki, wanathibitisha kuwa mkataba ambao umeanza kutumika tangu Januari 22 mwaka huu na kuhamasishwa na mashuhuda wasiochoka wa waathirika wa mwaka 1945 ni hatua ya kihistoria kuelekea ulimwengu bila silaha za atomiki. Kwa hakika ni hatua muhimu kwamba silaha za kinyuklia hatimaye zinamepigwa marufuku na sheria za kimataifa na hatua muhimu ya kuhakikisha kuwa ukatili huko Japan hautatokea tena”, ujumbe huo unasema. Mkataba huo mpya unaruhusu nchi zote kuwa na fursa ya kuungana ili kumaliza vitisho vya nyuklia ambavyo vimeenea ulimwenguni tangu siku ya mabomu ya atomiki mnamo 1945. Hatua za kwanza za dhati kutokana na mkataba maeneo yaliyochafuliwa na majaribio ya nyuklia. Kwa kuhitimisha wanahizimza kuhakilisha kwamba maadhimisho haya yanawapatia wote nguvu na uvumilivu, pamoja na manusura wa Hibakusha, viongozi wa Kanisa, mashirika ya amani, wanaharakati, viongozi wa kisiasa na watu wengine ulimwenguni kote, kuendelea na kazi yao kupinga silaha za nyuklia na kwa kutafuta haki kwa watu walioathiriwa na majanga ya nyuklia tangu mashambulio ya Hiroshima na Nagasaki.

Askofu Lang: kama Papa 'hakuna kupoteza kumbukumbu ya kile kilichotokea'

Kamwe hakuna kupoteze kumbukumbu yako ya kile kilichotokea na ili isirudiwe hali hiyo. Baba Mtakatifu Francisko alisema hayo wakati alipotembelea eneo la Kumbukumbu ya Amani ya Hiroshima wakati wa hija yake ya kitume nchini  Japan mnamo 2019 na maneno yake yamerudiwa tena  tarehe 6 Agosti katika, kumbukumbu ya miaka 76 ya bomu la nyuklia, na rais wa Idara ya Mambo ya Kimataifa ya Baraza la  Maaskofu wa Uingereza na Wales, Askofu Declan Lang, katika ujumbe wake uliotumwa kwa ajili ya tukio hili.” Wakati watu huko Japan na ulimwenguni kote wanakumbuka bomu la Hiroshima ya mnamo tarehe 6 Agosti 1945, tunakumbuka tena maneno ya Baba Mtakatifu Francisko kwenye eneo la Ukumbusho wa Amani wa Hiroshima na kuungana naye kuombea ulimwengu bila silaha za nyuklia”.

Akiendelea katika   maneno yake yaliripotiwa na wavuti wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Wales  amesema kwamba  baba Mtakatifu wakati wa hija yake ya kitume kwenda Japani alisisitiza umuhimu wa maadili ambayo kamwe yasiruhusu vizazi vya sasa na vijavyo kupoteza kumbukumbu ya kile kilichotokea hapo, akithibitisha kuwa ni kumbukumbu  inayohakikisha na inahimiza ujenzi wa siku za usoni zilizo na haki zaidi na za kindugu. Mwaka jana maaskofu katoliki wa Uingereza, Wales na Uskochi walisherehekea miaka 75 ya bomu kwa kurudia wito kwa Uingereza wa kuachana na silaha zake za nyuklia na mnamo Januari walihimiza serikali kutia saini Mkataba wa Kuzuia Silaha utakapoanza kutumika, amekumbusha. Askofu Declan na Askofu William Kenney pia wameungana  na viongozi wengine wa Kanisa kulaani uamuzi wa Uingereza wa kuongeza akiba ya nyuklia kama hatua ya kurudi nyuma ambayo haitamfanya yeyote kati yetu kuwa salamana wameahidi kufanya kazi pamoja kuelekea kuondoa kabisa silaha za nyuklia.

06 August 2021, 10:18