Waamini wakiudhuria Misa Takatifu Waamini wakiudhuria Misa Takatifu 

Kard.Bassetti:Maria ni kama mwinjili wa kwanza na mwinjilishaji

Katikati ya moyo wa mwezi wa Agosti,Makanisa yote ya Magharibi na Mashariki kwa pamoja wamesherehekea sikukuu ya Kupalizwa kwa Maria Mbinguni,ishara ya Kanisa ya kipekee ambayo inajitambua katika picha halisi ya Mama wa Mungu anayepalizwa Mbinguni.Ni kutoka mahubiri ya Kardinali Bassetti Rais wa Baraza la Maaskofu Italia,tarehe 15 Agosti 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika siku kuu ya Kupalizwa mbinguni kwa Bikira Maria tarehe 15 Agosti 2021, Kardinali Guartieroro Bassetti, rais wa Baraza la Maaskofu Italia CEI akiongoza misa ya siku kuu hiyo ametoa mahubiri yake kuwa Mama Maria anatufundisha kutazama maisha yetu na si visingiti vyenye giza katika ulimwengu huu, lakini ni matarajio na katika peo za Mungu. Sisi tumezaliwa ili kuweza kumfikia Baba na katika dunia hii sisi ni kama waafiri na hatupaswi kushikilia mali za dunia kana kwamba  za umilele. Kama Maria sisi sote tunaalikwa siku moja katika siku kuu ya Mungu, katika amani timilifu ya furaha na si katika katika pumziko milele…

Askofu Mkuu wa Perugia katika mahubiri hayo amesisitiza kwamba tumwombe Mama Maria atusaidie kuwa na imani hadi kufikia kukutana na Mungu kwa furaha, kwa sababu kuwa na imani haina maana ya kuondokana na matatatizo ya dunia hii.  Tupo bado tunateseka na janga, lakini lazima hata kupanua mitazamo yetu. Kama ilivyo katika kipindi hiki ambacho si rahisi kutofikiria nchi ya Afghanistan mahali ambamo Watalebani wanaendelea na mauaji ya wanawake na watoto!  Inawezekanaje usifikirie ndugu zetu wa Haiti ambao wamepata pigo jipya la tetemeko la ardhi? Kwa maana hiyo kuna mateso mengi na sisi tunaalikwa kama Maria kuwa mabalozi wa ndugu zetu wanaoteseka na wale wote ambao wana matatizo ya kibinadamu. Wakati anaanza mahubiri hayo Kardinali Bassetti amekumbusha jinsi ambavyo ameadhimisha misa ya siku kuu  hiyo kwa mara ya 11 nao. Lakini akaongeza kusema kuwa wakati anatoka uasikofuni, alikutana na baadhi ya watu walio mwambia kuwa “ Askofu siku  kuu  njema ya likizo ya mwezi wa nane”( Buon Ferragosto), "kiukweli ninawambia, afadhali wangeniambia heri na siku kuu ya Mpalizwa, ningefurahi zaidi”.

Kardinali Bassetti baadaye kwa kufafanua zaidi akaongeza “hii pia ni ishara ya mawazo ambayo yamekuwa ya kidunia sana, lakini maovu ya jamii yetu, ya maisha yetu, ni tofauti kabisa”. Katika kufafanua juu ya kifungu cha Injili cha Luka , juu ya ziara ya Maria kwa Mtakatifu Elizabeth, Kardinali Bassetti amesema: Katikati ya moyo wa mwezi wa Agosti, Makanisa yote ya Magharibi na Mashariki kwa pamoja wamesherehekea sikukuu ya Kupalizwa kwa Maria Mbinguni, ishara ya Kanisa la kipekee ambalo linajitambua katika picha halisi ya Mama wa Mungu anayepalizwa Mbinguni ... Maria, tunaweza kusema, ndiye mwinjili wa kwanza, ndiye mwinjilishaji wa kwanza, kwa sababu mara tu baada ya kupokea tangazo la Malaika, kwa haraka, mwinjili  Luka abnathibitisha kuwa alianza safari kwa haraka kuelekea mkoa wa milima wa Yudea kwenda kukutana na binamu yake Elizabeth, sio tu kwa tendo la upendo na hisani kwa jamaa  yake mzee, lakini juu ya yoteni  kuleta sababu ya furaha na matumaini yake, ya Yesu Kristo na wokovu wa ulimwengu. Haraka ya Maria katika kuwasiliana na ujumbe mkubwa zaidi, ule wa imani, pia iwe haraka yetu katika kumkaribisha, kumtangaza na kumshuhudia Yesu.

Katika kuzingatia maana ya Kupalizwa Mbinguni, Kardinali amekumbusha kwamba Maria, kama Yesu, yuko Mbinguni katika mwili na roho. Ni sherehe nzuri pia kuangazia wito wetu wa Kikristo. Maria, kwenye safari za kidunia, hakuwahi kujitenga na Yesu, kila wakati alikuwa pembeni mwake ... Na jambo hili pia linahusu maisha yetu, kwa sababu hiyo ndio hatima ya mama na ndio mwisho wa watoto ... Ni fumbo kubwa tunalosherehekea leo, kwa sababu haihusishi maisha yetu tu, kujitoa kwetu Kikristo, utunzaji wa mwili wetu unaotarajia ufufuko”. Kwa sababu hiyo maisha yetu ni matakatifu tangu mwanzo, tangu kutungwa, hadi mwisho. Hakuwezi kuwa na njia za mkato za kufupisha maisha na jinsi umuhimu wa kutafakari juu ya Dhana ya Maria kupalizwa Mbinguni, kwa sababu wanatembea pamoja wale wote ambao wamefungamana maisha yao kwa Mwana wa Mungu. Kwa bahati mbaya tunajisahau mara nyingi kuwa sisi tumefanywa kwa ajili ya mbingu na safari yetu si kwamba haina mwisho: mbingu na dunia, kupitia Maria, vimeingiliana katika kukumbatiana kwa upole”.

Kardinali kwa kuhitimisha amewaalika waamini kusali kwa Mama yetu Maria ili aweze kutusaidia kupata katika maisha yetu nafasi kwa ajili ya ukimya, kwa ajili ya kuabudu, kwa ajili ya tafakari ya moyo, kwa ajili ya kuwa na mshangao na kwa kwa ajili ya kuona maana  hasa katika kuishi kama Mitume ambao walikuwa wanakaa na Yesu. Tunajua kuzungumza sana juu ya Mwana wa Mungu, anasema lakini labda kwa bahati mbaya tunaishi naye kidogo. Siku kuu ya tarehe 15 Agosti utafikiri inataka kutueleza kuwa simama kidogo kabla hujachelewa, ishi na usijiruhusu kuishi tu; ishi kwa vitu vyema na sio kwa utupu na michezo; kutoa maana kwa maisha yako na wakati wako. Maria anatufundisha kutazama maisha yetu sio kutoka vichochoro vya ulimwengu huu, lakini kutoka kwa mitazamo na upeo wa Mungu ”.

MAHUBIRI KARDINALI BASSETTI

 

16 August 2021, 14:26