Baraza la Maaskofu  Afrika Kusini Baraza la Maaskofu Afrika Kusini 

Afrika Kusini,Askofu Sipuka:umuhimu wa kuhamasisha misingi ya demokrasia

Umefunguliwa Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Afrika Kusini ambapo Askofu Sipuka Rais wa Baraza hili wakati wa kutoa hotuba ya ufunguzi tarehe 2 Agosti amesema kuwa ni lazima kuhamasisha misingi ya kidemokrasia ya nchi na majukumu badala ya kushikamana na watu fulani na vyama.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kufundisha idadi ya watu juu ya demokrasia na kuwahimiza kupiga kura kwa misingi ya kanuni na majukumu, badala ya hisia na kushikamana na watu fulani na vyama. Haya ndiyo maelekezo kutoka kwa Askofu Sithembele Anton Sipuka, rais wa Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini(Sacbc), iliyotolewa katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Maaskofu. Mkutano umefunguliwa tarehe 2 na utamalizika tarehe 7Agosti, ambao unafanyika kwa njia ya mtandao tu kutokana na janga la Uviko- 19 inayonendelea. Awali ya yote, Askofu amekabiliana na masuala magumu ya vurugu na uporaji ambao katika nyakati za mwisho umewakumba Eswatini na Afrika Kusini yenyewe.  Vile vile eneo lote kwa ujumla limekumbwa na maandamano makali dhidi ya mfalme Mswati III, aliyeko madarakani karibu zaidi ya miaka 30. Maandamano yalikandamizwa na ngumi ya chuma kwa jeshi na kusababisha vifo na majeruhi, Polisi ni wahusika. Katika jambo hili, kupitia Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Afrika kusini (Imbisa) ambalo linajumuisha viongozi wa Angola, Botswana, eSwatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, São Tomé na Principe, Afrika Kusini na Zimbabwe), lililaani mauaji hayo na mapo walisema kuna ubaguzi, utekaji nyara na mateso yalitokea eSwatini, huku wakizindua wito wa mazungumzo, maridhiano na suluhisho la amani katika eneo hilo.

Mtazamo mwingine wa maaskofu pia umekwenda Afrika Kusini yenyewe, ambayo pia ni mahali pa mapigano ya hivi karibuni,  kwa vurugu na uporaji ambao umesababisha vifo zaidi ya watu 70 na kukamatwa kwa wengine 1,200. Kwa asili ya mvutano huo, maandamano hayo yalitokea kufuatia kukamatwa kwa Mkuu wa Nchi wa zamani, Jacob Zuma, aliyehukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kudharau Mahakama, katika hali ya kesi ya ufisadi. Katika mantiki chanya, ambayo inaweza kuonekana katika maandamano hayo Askofu Sipuka amesema wanaonekana kuwa na hatua isiyoweza kurekebishwa kusuluhisha ukosefu wa demokrasia katika eneo hilo. Ni matumauni ya Sacbc kufanukiwa bila kupoteza zaidi maisha yenye thamani. Wakati huo huo, rais wa maaskofu amesisitiza tofauti kati ya mizozo iliyoibuka katika nchi hizo mbili kwanza “huko eSwatini ​​watu wanapigana dhidi ya mfalme ambaye analichukulia taifa kama mali yake ya kibinafsi, wakati huko Kusini Afrika wale ambao wanachochea vurugu wanapigania adhabu ya mtu ambaye alifanya kitu kama hicho na  aliwezesha uporaji wa nchi na wakati alipkuwa awajibike kwa matendo yake, hakuheshimu sheria za kitaifa”. Kimsingi, amesema Askofu  Sipuka, huko eSwatini watu wamechoka na mtu asiyeguswa, wakati huko Afrika Kusini wanapigania kurudi kwa mtu kama huyo madarakani. Lakini ugonjwa mkubwa wa mtu ambaye mtu ameidhinishwa kufanya kile anachotaka, ni mbaya kwa nchi”, ameonya askofu, “kwa sababu hii inamaanisha kuwa wale walio madarakaniwanaweza kujitoa kwa faida ya wote kwa ajili ya faida yao wenyewe”.

Ugonjwa huu mkuu pia umeathiri Kanisa wakazi wa zamani aliongeza kusema  rais wa Baraza la maaskofu,  lakini shurani kwa  Mungu, sasa Kanisa limeamka.  Kwa njia hiyo, ametia moyo kwa kujitoa kikamilifu katika uamsho wa Afrika Kusini, akiunganisha sauti ya Kanisa na ile ya wale ambao wanawajibika juu ya wale ambao wamefanya vurugu na uporaji na wale ambao wanataka maendeleo makubwa ya uchumi ya idadi ya watu, badala ya misaada ya muda tu.  Kwa upande mwingine amekumbusha takwimu zinaonesha kuwa, kila mwaka, nchini Afrika Kusini watoto milioni 1.1 wanazaliwa. Kati ya hawa, ni wahitimu 150,000 tu, ambayo inaruhusu mjanja yeyote kuwatumia vijana kwa malengo yake ya ubinafsi”. Lakini ni katika uwanja wa elimu na ajira, kwa mfano katika sekta ya vijijini, kwamba Kanisa linaweza kufanya sehemu yake, alimkumbuka rais wa Sacbc: “Tuna shule na tuna ardhi kubwa ambazo wamisionari wameturithi. Kwa hivyo tunaweza kutafuta suluhisho”. Hali mbaya katika eSwatini na Afrika Kusini, kwa hivyo, lazima ichukuliwe kama fursa ili Kanisa liweze kuwasilisha kwa watu kanuni za kidemokrasia zinazofaa zaidi kwa upatanisho wa kitaifa.

Mkazo wa kiongozi huyo mwingine ukageukia juu ya janga la Uviko-19 ambapo, Afrika Kusini, limesababisha maambukizi milioni 2.47 na vifo zaidi ya 72,000 hadi sasa. Askofu Sipuka amewashukuru wale wote ambao wameweka imani katika nyakati hizi ngumu, na vile vile "makuhani na wafanyakazi wa kichungaji ambao wameendelea kuwa wabunifu katika muktadha huu muhimu. Wazo la kushukuru lilienda kwa wagonjwa wote na waliokufa kutokana na janga hili. Pamoja na hayo, tunaweza kusema salama kwamba imani ya Kikatoliki bado iko hai kusini mwa Afrika”, aliongeza kiongozi huyo, na baadaye kuwakumbusha waamini wote kwamba makanisa yako wazi na yanaweza kutembelewa, kwa kufuata kabisa itifaki zote za afya.

Wakati huo huo, rais wa Sacbc ameonesha uchungu na jinsi Wakatoliki na Wakristo wote kwa jumla wametumia wakati wao kidogo kupunguza mateso ya kijamii yanayotokana na UVIKO-19 na vurugu za hivi karibuni. Wakristo ni asilimia 80 ya idadi ya watu wa Afrika Kusini alibainisha na kwamba “Ikiwa tungekuwa na umoja zaidi, tunaweza kutoa zaidi kwa watu wanaohitaji, badala ya kutawanya michango ya mtu binafsi kati ya madhehebu tofauti. Kwa maana hiyo ametia wito wa ulazima kwa kufanya kazi kwa umoja na mazungumzo ya kidini hasa katika ngazi ya chini. Hatimaye Askofu  Sipuka ameonesha imani na kampeni ya chanjo dhidi ya Covid ambayo inaonekana kuwa hatimaye ina afueni kwa sasa, dozi milioni 7.57 zimetumiwa nchini, na kufikia asilimia 5 ya idadi ya watu. Miongoni mwa mada zingine zilizo kwenye ajenda ya Mkutano huo ni safari ya kuelekea Sinodi Kuu ya Maaskofu, iliyopangwa huko Vatican mnamo 2023 juu ya kaulimbiu “Kwa Kanisa la Sinodi: muungano, ushiriki na utume” na pendekezo la sheria ya kitaifa juu ya ndoa ambayo inakusudia kuanzisha mitala.

05 August 2021, 10:03