Bendera ya Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya  

Afghanistan,Jumuiya ya Papa Yohane XXIII:Ulaya isigeuze kisogo ikaribishe wakimbizi

Jumuiya ya Umoja wa Ulaya isigeuze kisogo chake kuwasahau wakimbizi wa Afghanistan.Katika familia zetu nchini Italia na nchi za nje tunaendelea kupokea vijana wengi,hata wadogo ambao wanakuja kutokea Afghanistan,ambao walifikia kupitia njia za mikondo ya kibinadamu kwenye makambi ya wakimbizi huko Ugiriki.Ni uthibitisho wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Papa Yohane XXIII akiomba msaada wa Tasisi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tunaungana na sala ya Papa Francisko ili milio ya silaha isitishwe na kushinda meza ya mazungumzo. Ndivyo anathibitisha Giovanni Paolo Ramonda, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Papa  Yohane XXIII akigusia juu ya hali haisi ya kipeo cha kibinadamu kinachoendelea huko Afghanistan.” Katika familia zetu nchini Italia na nchi za nje tunaendelea kupokea vijana wengi, hata wadogo ambao wanakuja kutokea Afghanistan, ambao walifikia kupitia njia za mikondo ya kibinadamu kwenye makambi ya wakimbizi huko Ugiriki. Katika nyumba zetu wanapata ulinzi, msimamo, faraja kwa ajili ya majeraha yasiyelezeza na wanasimulia uchungu mkubwa kwa ajili ya familia zao zilizobaki nchini Afghanistan”. Bwana Ramonda anendelea kuelezea kuwa “ wazo na mamombi yanawaendea wale wote ambao wanaendelea kupata vurugu pasipo haki na kufanywa watumwa kwa namna ya pekee wanawake, watoto kike na kiume na makabila madogo. Hatuwezi kuwageuzia mabega yetu, kwani ni dharura ambayo taasisi za Ulaya ziweze kuelekeza suluhisho na mapokezi, wakipinga kuwarudisha kwa nguvu, na kutenda kwa ngazi ya kisiasa na mapendekezo ambayo yanapinga mantiki za vurugu.”

Umati  mkubwa ukitafuta namna ya kukimbia nchi
Umati mkubwa ukitafuta namna ya kukimbia nchi

Mshikamano wa Kituo cha Astalli kwa wakimbizi wa Afghanistan nchini Italia

Katika Kituo cha Astelli cha Wajesuit, kinaelezea mshikamano kwa wakimbizi wa Afghanistan ambao wanaishi Italia. "Katika wiki hizi za vurugu na masaa haya ya mwisho tuko karibu na vijana wengi wakimbizi ambao kwa miaka sasa tumewapokea na kuwasindikiza. Tunaamini ulazima wa kushirikishana na wasiwasi wao ambao unazidi kukua wakati wanatazama na nchi yao isiyo na ulinzi na wanatuomba wafanyeje ili kuwaweka wapendwa wao katika hali ya usalama.

Padre Camillo Ripamonti, Mwenyekiti wa kituo cha Astalli amesema “tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, taasisi za Ulaya na za mataifa ili waweke kipaumbele cha usalama na kulinda raia". Watafute njia zinazowezakana na za usalama wa kuingia Ulaya kwa yule ambaye anatafuta kuacha nchi ya Afghanistan. Ni lazima kwa watu ambao kwa makumi ya miaka wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa na vita katika Nchi ambayo tumehushwa moja kwa moja na ambayo tunayo wajibu huo kwao.

17 August 2021, 15:17