Maofisa kutoka Utume wa India nchini  Afghanistan wakiondoka kurudi kwao kwa sababu ya hofu Maofisa kutoka Utume wa India nchini Afghanistan wakiondoka kurudi kwao kwa sababu ya hofu 

Jumuiya ya Mt.Egidio&Makanisa ya Kiinjili waomba mkondo wa dharura kwa wakimbizi!

Kufuatia na kile kinachoendelea nchini Afghanistan,Jumuiya ya Mtakatifu Egidio na Makanisa ya Kiinjili wanaomba mikondo ya kibinadamu ya dharura ili kuwapokea wakimbizi.Katika ombi lao lililosainiwa na wenyeviti wa shirikisho la kiinjili Italia na Mratibu wa Wavaldese:"Tunaomba kujitoa kwa Italia, ambayo ilikuwa ya kwanza kufanikisha mikondo ya kibinadamu,ili kupitisha uhamishaji wa wakimbizi wa Afghanistan.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ulaya lazima itende kwa dharura kwa ajili ya ulinzi wa wale ambao wanakimbia nchini Afghanistan iliyochukuliwa na Watalebani.  Kwa masaa haya wanaume, wanawake na watoto wako hatari ya maisha kiurahi kwa sababu ya kuamini katika thamani ya demokrasia, uhuru wa kujieleza na kusoma. Tunaomba pia kujitoa kwa Italia, ambayo ilikuwa ya kwanza kufanikiwa kwa mikondo ya kibinadamu, kupitisha zana hii kuwezesha uhamishaji wa wakimbizi wa Afghanistan.

Kwa zaidi ya miaka sita sisi, Wakatoliki na Waprotestanti, tumekuwa tukifanya kazi pamoja kujenga mikondo za kibinadamu kutoka Lebanon na kutokana na itifaki mpya na Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Mambo ya nje, tulizindua “mkondo wa kibinadamu wa kwanza kwa wakimbizi 200 kutoka vituo vya kizuizini vya Libya na, wakati huo huo, kuruhusu uokoaji wa wengine 300. Kulingana na uzoefu huu tuko tayari kutekeleza mpango kama huo kwa niaba ya wakimbizi wa Afghanistan, ambao tayari wanashirikiana na taasisi, tawala za mitaa na maneno mengine ya raia wa jamii ambao wanataka kushiriki mpango huu wa haraka wa kibinadamu.

Tunaweza basi kuwasaidia wale Waafghanistan ambao, tayari wako Ulaya, wanaishi katika hali mbaya. Tunaomba serikali zote za Ulaya zisimamishe vitendo vya uhamisho ambavyo tayari vimekwishaamuliwa kwa mamia ya waombaji hifadhi na wakawakataa Waafghanistan, na pia wachunguze tena maombi yaliyokataliwa kutokana hali hii ya kutisha. Tunathibitisha kwamba nguvu ya kimaadili na kisiasa ya Ulaya pia imejengwa kwa kuhakikisha haki za kibinadamu na ulinzi kwa wale wanaoteswa na ambao tayari wamepata mateso ya janga hili la vita. Ombi hili limesania na Marco Impagliazzo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio; Luca M. Negro, Mwenyekiti wa Shirikisho la Makanisa ya Kiinjili nchini Italia na Alessandra Trotta, mratibu wa Meza ya Wavaldese.

17 August 2021, 14:38