Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu Ouagadougou, Burkina Faso na Rais wa SECAM Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu Ouagadougou, Burkina Faso na Rais wa SECAM 

Ujumbe kwa ajili ya Siku ya Secam:kufanya kazi kwa umoja na muungano

Siku ya Secam inatukumbusha umoja wetu na Mungu na kati yetu katika Kristo ambaye anashinda tofauti zetu zote na kuziweka katika mtazamo sahihi”.Amesema hayo katika ujumbe uliosainiwa na Kardinali Philippe Ouédraogo,Askofu Mkuu wa Ouagadougou na rais wa SECAM katika fursa ya Siku ya Secam inayoadhimishwa kila tarehe 29 Julai ya kila mwaka.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

“Kupuka kutoka kila kitu kinachogawanya na badala yake kufyonza na kudumisha kila kitu kinachomweka Mungu katika nafasi ya kwanza maishani mwetu na kulisha udugu wa kweli na udugu katika bara hili”. Huu ndiyo wito wenye shauku kubwa kwa waamini uliotolewa na maaskofu wa Kiafrika katika Ujumbe wao wa Siku ya Secam ambayo inaadhimishwa kila tarehe 29 Julai hadi tarehe 1Agosti. Tukio hili lilianzishwa mnamo mwaka 2013 katika kufanya kumbukumbu ya kuanzishwa rasmi kwa Kongamano la Maaskofu wa Shirkisho la Mabaraza ya Afrika na Madagascar (SECAM), ambalo lilifanyika mnamo tarehe 29 Julai 1969, mbele ya Papa Paulo VI wakati wa hija yake ya kitume ya Uganda.

“Siku ya Secam inatukumbusha umoja wetu na Mungu na kati yetu katika Kristo ambaye anashinda tofauti zetu zote na kuziweka katika mtazamo sahihi”. Amesema hayo katika ujumbe uliosainiwa na Kardinali Philippe Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou na rais wa SECAM. “Katika wakati ambao ni wenye migogoro, migawanyiko na vurugu barani Afrika, mwaliko huu ni kukuza utamaduni na maono ya ulimwengu ambayo yanajumuisha na mizizi katika Kristo ambapo hakuna Myahudi wala Mgiriki, hakuna Bwana wala mtumwa. Kwa kuongezea, hii ni roho ambayo imekuwa ikihuisha Secam, ambayo maaskofu wote wa bara hili hushiriki majukumu, na pia ni maana ya Siku ambayo inakusudia kuwapa Wakatoliki wa Kiafrika fursa ya kusaidia kuunga ujumbe wake. Masilahi yetu ya pamoja na kujitolea kwa Shirikisho ni muhimu kufanikisha malengo yake”, ameasisitiza Kardinali Ouedraogo katika ujumbe huo.

Kwa upande wa Kardinali, anawahimiza maaskofu hasa kuhamasisha ushirika na kuingiliana ili kutekeleza kile kinachoitwa Hati ya Kampala katika Makanisa yao ya karibu, ambao ni Waraka wa kichungaji wa SECAM uliochapishwa mwezi Januari iliyopita wa kujitolea katika umisionari kwa bidii zaidi katika bara zima. Katika suala hili, Secam inatoa shukrani kwa ndugu Maaskofu, makleri wote, watawa na washiriki wote wa Kanisa, familia ya Mungu barani Afrika na Visiwani kwa kujitolea kwao kwa uinjilishaji, licha ya ugumu wa sasa katika pande mbali mbali za ulimwengu. Ujumbe pia unazungumzia juu ya chungu na za kuumiza zinazoikabili Afrika hivi sasa: kwa mfano janga la Uviko -19, ukosefu wa usalama, vurugu, ugaidi, vita ambavyo vimesababisha upotezaji wa maisha ya watu wengi na mali na ambayo inalazimisha watu wote kuishi bila ubinadamu, hali na hofu ya kila wakati. Katika kushiriki maumivu waliyonayo watu wa Kiafrika, SECAM inahimiza upyaisho na ujasiri mpya na uaminifu kwa Mwenyezi, Mungu mwenye upendo na huruma. Kwa waamini pia wamealikwa kurejea katika siku hizi tatu kwa Mungu Baba ili kumshukuru kwa baraka tele na ulinzi wake endelevu, kwa zawadi ambayo kila mmoja anawakilisha kwa mwenzake na kwa zawadi ya Mama Afrika na imani ya Kikatoliki.

Kutoka kwa maaskofu wa Afrika kwa maana hiyo ni maombi ya kumalizika kwa janga la Uviko-19, vurugu, mateso na utekaji nyara na kuthamini juhudi zinazofanywa na serikali za bara ili kudhibiti kuenea kwa virusi katika nchi zao na kitia moyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kulinda afya za watu wetu”. Hatimaye ni asanta kwa watu wote, wakiwemo makuhani na watawa, ambao wamefanya bidii yao katika miezi ya hivi karibuni kuleta afueni kwa wagonjwa. Maadhimisho kiutamaduni tarehe 29 Julai, ya Siku ya Secam huhamishiwa Jumapili inayaofuata ikiwa tarehe yenyewe inaangukia katika siku za wiki, kama ilivyo kwa mwaka huu, kwa maana hiyo maadhimisho ni siku ya Jumapili tarehe 1 Agosti. Katika tukio hilo, Kardinali Philippe Ouédraogo taongoza sherehe kuu ya Ekaristi, japokuwa Misa nyingine zimepangwa kufanyika katika makanisa na parokia zote za bara.

31 July 2021, 15:22