Maaskofu wa IMBISA (Angola, Botswana, eSwatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, São Tomé na Principe, Afrika Kusini na Zimbabwe) Maaskofu wa IMBISA (Angola, Botswana, eSwatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, São Tomé na Principe, Afrika Kusini na Zimbabwe) 

Afrika Kusini:Mkutano wa maaskofu kuhusu mivutano kijamii

Kuanzia tarehe 2-7 Agosti 2021 unatarajiwa kufanyika mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Afrika Kusini (Sacbc)ambao utajikita katika masuala yanayohusi mivutano ya kijamii,maandalizi ya Sinodi 2023 na sheria kuhusu ndoa nchini humo.Hata hivyo Baraza hili hivi karibuni ililaani mauaji yaliyotokea yenye ubaguzi,kukamatwa,utekaji nyara na mateso yalitokea huko eSwatini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mivutano ya kisiasa na kijamii, huko Eswatini na nchini Afrika Kusini, mchakato wa safari ya Sinodi kuu ya maaskofu ambayo inatarajiwa kufanyika mnamo 2023 na kujadili mapendekezo ya sheria ya kitaifa kuhusu ndoa ndizo mada msingi wa mkutano mkuu wa Baraza la Maaskofu Afrika Kusini (Sacbc) utakaofanyika kuanzia tarehe 2-7 Agosti 2021. Kwa sababu ya janga la Uviko -19, mkutano huo utafanyika kwa njia ya mtandao tu kama ilivyotokea mwezi Januari mwaka huu.  Katika hatua ya kwanza, maaskofu katika mkutano wao watatafakari juu ya hali halisi ambayo watu wa Eswatini wanaishi, kwa sababu ni kipindi sasa katika Nchi kumeibuka na maandamano ya nguvu dhidi ya mfalme Mswati III, aliyeko madarakani kwa zaidi ya miaka 30. Kipindi cha kuchochea kilikuwa ni mauaji ya mwanafunzi mmoja mnamo mwezi Mei, ambapo polisi wanawajibika. Maandamano yalikandamizwa na ngumi ya chuma na kupelekwa walipeleka jeshi na kusababisha vifo na majeruhi, Polisi ni wahusika.

Katika jambo hili, kupitia Shirikisho la Baraza la Maaskofu wa Afrika kusini (Imbisa) ambalo linajumuisha viongozi wa Angola, Botswana, eSwatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, São Tomé na Principe, Afrika Kusini na Zimbabwe), lililaani mauaji hayo ambayo hayana sheria, yenye ubaguzi, kukamatwa, utekaji nyara na mateso yalitokea eSwatini, huku wakizindua wito wa mazungumzo, maridhiano na suluhisho la amani. Mtazamo mwingine wa maaskofu pia utakwenda Afrika Kusini yenyewe, ambayo pia ni mahali pa mapigano ya hivi majuzi, vurugu na uporaji ambao umesababisha vifo zaidi ya watu 70 na kukamatwa kwa wengine 1,200. Kwa asili ya mvutano huo, maandamano hayo yalitokea kufuatia kukamatwa kwa Mkuu wa Nchi wa zamani, Jacob Zuma, aliyehukumiwa kifungo cha miezi 15 gerezani kwa kudharau Mahakama, katika hali ya kesi ya ufisadi. Hata katika kesi hii, kwa mara nyingine tena maaskofu walichukia sana hali hiyo, wakiwaalika wale wote wanaohusika na vitendo vya uharibifu na uhuni kutafakari juu ya uharibifu uliosababishwa kwa nchi nzima.

Kwa maana hiyo, Baraza la maaskofu (Sacbc) litaangalia juu ya Mkutano Mkuu wa XVI wa Maaskofu au Sinodi iliyopangwa kufanyika jijini Vatican katika miaka miwili, ijayo kwa kuongozwa na kaulimbiu “Kwa ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume”. Kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko, ambapo tukio hili litatanguliwa na machakato wa maandalzili ya miaka miatatu ambayo imegawanywa katika awamu tatu: Kijimbo, bara na ulimwengu mzima, inayotajatia kuanza tarehe 17 Oktoba ijayo, ambapo kila Askofu atazindua mchakato huo. Na hatimaye, maaskofu wa Afrika Kusini watazingatia pendekezo la sheria ya kitaifa juu ya ndoa kuhusu Pepuda, yaani mswada wa sheria juu ya Uhamasishaji wa Usawa na Kuzuia Ubaguzi (Sheria ya Kukuza Usawa na Kuzuia Ubaguzi ya tarehe 17 Juni 2021). Kuhusiana na mpango wa kwanza wa sheria, ni lazima izingatiwe kuwa tawala tofauti za ndoa zilizozomo Afrika Kusini: kwa upande mmoja kuna ndoa ya kiraia, kwa upande mwingine kuna ndoa nyingine za kitamaduni, ambazo zinatofautiana kulingana na jumuiya za kikabila na ambazo zinawakilisha asilimia 3 ya jumla ya harusi zilizoadhimishwa nchini humo. Wakati ndoa ya wenyewe kwa wenyewe ni ya watu wawili tu, ndoa za kiutamaduni ya jamii nyingine zinatambua uwezekano wa mitala. Kwa sasa, muswada husika, ambao kura yake katika Bunge inatarajiwa kufanyika mnamo 2024, pia inakusudia kuanzisha polyandry yaani mitala.

Sio hivyo tu: serikali iliendelea kuandaa pendekezo la sheria kupitia kile kinachoitwa “Green Paper” yaani kitabu cha kijani. Iliyochapishwa mnamo mwezi Mei, ambayo ilikusanya uchunguzi na maoni ya vikundi kadhaa vya raia, viongozi wa jadi na wa dini, ambacho kilitokeza kwamba ndoa ni taasisi ambayo inapaswa kupatikana kwa wote, bila kujali jinsia, kwa maana hiyo ni juu ya hoja hizi maalum ambazo maaskofu watakaa na kukabiliana nazo katika mkutano mkuu. Kwa upande wa Pepuda, maaskofu hao wanataja kile ambacho tayari kimesemwa na ForSa, Uhuru wa Dini nchini Afrika Kusini, shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi kwa kuunga mkono uhuru wa kidini. Chombo hiki kilichukia ukweli kwamba, ikiwa itaidhinishwa, Pepuda italazimisha mashirika ya kidini, kwa jina la usawa, kukubali wanachama au viongozi au wafanyakazi ambao imani zao ni kinyume na zile za shirika lenyewe. Mwishowe, ajenda ya Baraza la Maaskofu inatoa fursa ya uchaguzi wa urais mpya, ambaye muda wake utaanza Januari 2022.

31 July 2021, 15:30