Nchi Takatifu:Sadaka ya Jumapili 30 Mei kwa ajili ya jumuiya za Gaza
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Patriaki wa Yerusalemu, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa ameomba Parokia zote na makanisa ya majimbo kutoa mchao wao wakati wa sadaka ya Jumapili tarehe 30 Mei ambapo Mama Kanisa anaadhimisha Siku Kuu ya Utatu Mtakatifu, kwa ajili ya Jumuiya za Gaza na mahitaji yao yaliyojitokeza katika ghasia za hivi karibuni
Katika barua yake iliyochapishwa kwenye Wavuti wa Upatriaki, Askofu Mkuu Pizzaballa amewaalika waamini wote kuwa na moyo mwema na mtazamo kwa ajili ya watu wenye kuhitaji zaidi hasa kwa ajili ya Gaza mahalia mbapo wao wamepata madhara makubwa ya mabomu kwa siku za hivi karibuni.
Mateso ya Gaza yamezidi kuongezeka katika ghasia na mashambilizi hayo kwa wakazi wa Gaza, wakati huo huo wakiendelea na mapambano dhidi ya Covid- 19 amesisitiza Patriaki. Kwa maana hiyo kiongozo huyo wa Upatriaki ameomba kwa moyo wote waweze kuchangia ili kutoa faraja katika mateso ya ndugu hao waamini wakristo. Na Mpango huo unataka kuwa ishara ya mshikamano kutoka majimbo yote ya upatriaki wa kilatino.