Kardinali Bassetti,Rasi wa Baraza la Maaskofu Italia Kardinali Bassetti,Rasi wa Baraza la Maaskofu Italia 

Kard.Basetti:Safari za kisinodi zitapyaisha Kanisa la Italia

Umehitimishwa mkutano wa 74 wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI).Rais wake akizingumza na waandishi wa habari amesema maaskofu wamejadili na kujiuliza juu ya ajira.Inahitajika mazungumzo ya utulivu na heshima ya dhamiri ya kila mtu hasa kuhusu suala la kiwango cha kuzaliwa na kwamba lazima kuhakikishia watu haki zao ili kushinda hofu za wakati ujao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Mkutano mkuu wa 74 wa Baraza la Maaskofu Italia, umemalizika huku ukifungua safari nyingine za kuanza kwa upya  hasa kwa kutazama wakati ujao wa Kanisa na jamii inayozunguka. Hii ina maana ya changamoto zake za Italia iliyojaribiwa kutokana na janga na matatizo ya ulimwengu wa ajira ulimwenguni. Kwa maana hiyo maaskofu wamzungumzia juu ya ukosefu wa ajira, vile vile hata na majanga ya sasa ya ulimwengu na pia hata ya vifo vya kazini na vya ghafla, vile vile changamoto za Kanisa, huku wakitafari namna ya kuanza safari mpya ya kisinodi kwa utashi wa Papa Francisko. Katika kikao hicho hawakukosa pia kuzungumzia juu ya kupungua kwa kiwango cha kuzaliwa kwa watoto chini suala ambalo limekabiliwa hivi karibuni hata na Papa Mwenyewe na Waziri Mkuu wa Nchi Bwana Mario Draghi, ambapo kwa ujumla ni lazima kukabiliana nalo kwa uwazi na utulivu huku kwa kuheshimu dhimiri ya wote.

Katika kazi ya kikundi cha wachungaji 200 wa Kanisa la Kaskazini, Kusini na katikati mwa Italia, pamoja na maaskofu 13 wastaafu, wameweka bayana juu ya dharura na jinsi gani Kanisa la Italia linapaswa kuanza kwa upya sinodi yake ambapo Kardinali Gualtiero Bassetti, Rais wa Cei,  katika  mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano huo amese mkutano huo haukuwa yakujikita na mazungumzo ya kichungaji kwa nyuzi 360 , yaliyojikita juu ya Injili na hali halisi za watu wa leo hii. Hiyo ni furaha, matumaini lakini pia majanga ya leo, ambayo ni furaha, matumaini na majanga ya Kanisa pia. Awali ya yote Rais metoa shukrani kwa niaba ya maaskofu wa Italia kwa Papa ambaye, katika hotuba yake ya utangulizi wa Mkutano, alitoa maoni mapya ya safari ya sinodi, akielekeza Mkutano wa Firenze wa mnamo 2015 kama rejeo na hatua ambazo zilijitokeza hapo. Kwa maana ya kutoka kwenda nje, kutangaza, kuishi, kuelimisha, kulipatia Kanisa sura ya mama anayewasindikiza na kubembeleza watoto wake. Watu wanahitaji leo hii, hasa katika wakati kama huu wa sasa, kwa sababu ya dharura ya kiafya na athari zake za kijamii na kiuchumi.

Sinodi inataka kuwa bembelezo kwa watu katika mateso makali amesema Kardinali Bassetti. Papa alisisitiza kwamba njia ya sinodi lazima iwe ya kutoka chini kwenda juu na kutoka juu kwenda chini.  Tunaanza na parokia, jimbo na pia kufikia katika shida mbalimbali. Baadaye kunzia kwa maaskofu, mahakama, lakini sio kutoka juu, bali kutoka chini, kwa wote pamoja, kwa sababu hata watu wa Mungu ni wasio shindwa katika kuamini, hakuna tofauti la jukumu kati ya waliobatizwa. Lengo ni sawa kila wakati, dhamira ya kutembea pamoja. Nina hakika kwamba umoja huu utaweza kufanya upya. Utume daima unafafana wa kutembea kwa pamoja. Ninuhakika kuwa umoja huo utaweza kupaushwa Kanisa kuanza ndani na si katika kudanganywa na matatizo ya watu”.

Na kusema hasa juu ya shida, kati ya zile mbaya zaidi ambazo wasiwasi mkubwa wa maaskofu ulielezewa, ni mikasa ya kazi: ukosefu wa ajira lakini pia vifo vibaya hivi majuzi mahali pa kazi. Shughuli za kibinadamu zinalingana na hadhi ya mtu huyo, kwa sababu wakati mtu ananyimwa kazi ni kana kwamba nilimnyima utu, Kardinali Bassetti aliwaambia waandishi wa habari pembeni mwa mkutano huo. Vijana ambao wakati wa miaka 30 wanasema: Sijui nifanye nini na maisha, kwa sababu sina kazi. Ningependa kuanzisha familia, lakini nitafanyaje?    , Kweli, katika hali hizo mtu hunyimwa utu wake”.

Rais wa CEI amewanyanyapaa vifo kazini kama dhuluma kubwa”: “Katika kipindi hiki, pia kwa sababu ya kufungwa, idadi ya ajira na ajali zimeongezeka. Hii inamaanisha kuwa, mahali pengine, kutakuwa na majukumu ikiwa maisha ya watu hayatahakikishiwa, “alisema. Rejea inahusu msiba wa hivi karibuni wa Mottarone, ambao ulisababisha vifo vya watu 14, wanaofafanuliwa na wachunguzi kama ‘janga la kutaka faida’. Ikiwa kuna majukumu ya wazi, jambo hilo linakuwa uhalifu na vile vile ajali, kwa sababu huwezi kucheza juu ya usalama wa watu’ ameshangaa Kardinali Bassetti. “Mtu huyo, akienda likizo, na akiingia kwenye kibanda lazima awe salama kama nyumba yake. Na kwa kuwa leo kuna njia za kuhakikisha usalama, mtu angefikiria kuwa hazitumiwi kuhakikisha maisha. Tunaona kile kilichowapata maskini 14. Tunatumahi kuwa mtoto huyo ataokolewa, na sisi maaskofu tumemwombea sana”.

Kuhusiana na kiwango cha kuzaliwa, kwa upande wa Kardinali Bassetti aanabainisha kuwa jambo hili ni dalili ya hofu. Hofu, ambayo ni, ya siku za usoni ambazo zipo kati ya watu. Huondoa matumaini katika maisha na katika maisha ya mtoto anayezaliwa. Kuwahakikishia watu haki zao inamaanisha kuwasaidia kuwa watulivu zaidi katika kupanga maisha yao ya baadaye. Nina uhakika katika siku zijazo za familia, hakuwezi kuwa na watoto, kwa sababu familia isiyo na watoto ni ndogo sana. Watoto ni matunda ya thamani ya ndoa. Sisi maaskofu tulizungumza juu yake na Waziri Mkuu Draghi, tukisisitiza kwamba lazima tuunde mazingira yote kwa watu kuishi katika mazingira mazuri ya kupata watoto”.

Kwa maana hiyo na maaskofu wote walikubaliana juu ya jambo hilo, la kutoa hundi moja inaweza kuwa  suluhisho zuri. Walakini, ameonya kardinali Bassetti, “lazima tuendelee kwenye njia hii kwa sababu kwa bahati mbaya Italia ni kana kwamba inaanza mwanzo. Ulaya iko mbele zaidi kwa kuzingatia familia. Ikiwa umakini mkubwa unakosekana kwa waajiri (siwezi kukutuma kwa sababu unatarajia mtoto, ni dhuluma!) Na pia kwa upande wa Serikali ambao unapendelea wale ambao wana watoto na wanataka kuwa nao, ikiwa hali hizi zinakosekana, huenda kidogo sana. Kwa hivyo, angalau Italia lazima iendane na kile kinachotokea mahali pengine, kwa mfano huko Ufaransa”.

28 May 2021, 15:24