Salvatore Martines, Rais wa kitaifa wa Chama cha Wakarismatiki,Italia Salvatore Martines, Rais wa kitaifa wa Chama cha Wakarismatiki,Italia  

Italia:14-26 Mei Semina ya Karismatiki:Njoo Roho Mtakatifu

Katika mambo ambayo yameukumba ubinadamu hasa Covid-19 kuna ile shauku kubwa ya kujiweka chini ya mabawa ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu.Ni makosa sana kwa yule anayefikiria kuwa Roho Mtakatifu anapokelewa mara moja tu.Utume wake katika maisha ya hauna kikomo na kila anapokuja daima kuna uvuvio mpya wa upendo,wa zawadi,wa karama na wa mshangao

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 26 Mei 2021 semina ya kitaifa ya Maisha ya Roho inaendelea. Ni katika kufanya Novena ya siku kuu ya Pentekoste ambayo ni kwa mwaka huu ni muhimu katika maandalizi ya kuungana wote wanachama cha Wakarismatiki Wakatoliki, kwa ajili ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 29 na Dominika tarehe 30 Mei 2021 katika fursa ya Mkusanyiko wao wa 43 Kitaifa wa Makundi na Jumuiya ya Wakarismatiki Wakatoliki Italia. Kwa njia hiyo semina imeanza Ijumaa usiki ya kitaifa ya Maisha Mapya katika Roho inaendelea kwa njia ya Mtandao, ikiongozwa na kauli Mbiu: “Njoo Roho Mtakatifu”, kupitia  kwenye Jukwaa la Roho Mtakatifu (RNS,) ukurasa wa Facebook na YouTube saa 2.30 usiku.

Semina hiyo imefunguliwa kwa wote kuanzia na wale wote ambao tayari wana uzoefu wa Ubatizo katika Roho kwa njia hiyo ili kuweza kupyaisha kwa umoja na ndugu, kaka na dada kwenye makundi na ndani ya jumuiya. Wakati huo huo semina hii inawaelekea wote ambao hawajawahi kufanya uzoefu wa Semina kwa ajili ya uvuvio wa roho na wanataka kujifungulia uhusiano mpya na Roho Mtakatifu. Kwa mujibu wa Bwana Salvatore Martines, Rais wa kitaifa wa Chama cha Wakarismatiki, Italia kabla ya kuanza semina hiyo amesema,  kuna shauku ya mapya katika Nchi, ya maisha mapya, ya kuzaliwa kwa upya, lakini kwa kufikiria pamoja yote hayo hasa zawadi ya Roho Mtakatifu ambayo inatoka katika Roho wa Mungu.

Katika mambo ambayo yameukumba ubinadamu hasa Covid-19, kuna ile shauku kubwa ya kujiweka chini ya mabawa ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Ni makosa sana kwa yule anayefikiria kuwa Roho Mtakatifu anapokelewa mara moja tu.  Utume wake katika maisha hauna kikomo na kila anapokuja daima kuna uvuvio mpya wa upendo, wa zawadi, wa karama na wa mshangao. Na ndiyo maana Kanisa halichoki kamwe kurudia kusema “Njoo Roho Mtakatifu. Linataka kuwa hata kilio chetu, katika siku hizi za kungojea sikukuu ya Pentecoste, amesisitiza. Katika Chama cha wakarismatiki na Papa Francisko wanaendelea kuhamasisha na kusaidia, kwani wamegundua neema ya upyaisho wa uvuvio wa Roho ambaye anauisha, anaamsha, analeta kwa nguvu uhai wote kama uhuisho wa kihistoria wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu na ambaye alikuja kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo.

Bwana Martinez aidha amesema katika karisimatiki kwa hakika ni neena ya kikanisa ya kuamshwa kwa uvuvio wa Roho, safari ya kujigundua binafsi kwa njia ya uzoefu wa Roho. Ni mambo mangapi mapya, uongofu, uponywaji, utume wa kikarama unaofanyiwa uzoefu na unaendelea kuiishi shukrani kwa uzoefu wa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Kwa maana hii, ni uamuzi, kuwa wajumbe wote wa chama cha wakarismatiki kwa kila ngazi, kutaka kuishi kwa pamoja “semina ya maisha mapya katika Roho ambayo yanafanya kazaliwa upya katika safari moja ya kijumuiya baada ya kipindi cha janga la kiafya.

Kwa pamoja ni kuomba Roho Mtakatifu. Kwa pamoja ni kupokea kwa mara nyingine tena Roho. Kwa pamoja ni kuomba upyaisho wa kiroho, uamsho wa sala kwa ajili ya kupata roho Mtakatifu ili kuweza kwa pamoja kukutana katika umoja na ambayo ni fursa maalum ya kurudia kwa pamoja kuomba nguvu ya Roho Mtakatifu ndani mwetu. Ni kutaka kutoa kipaumbele cha kwanza cha Roho Mtakatifu ikiwa Nchi zinataka kurudia kuishi na kutokana na mgogoro mkubwa wa kiafya ambao unaendelea, amesisitiza Bwana Martinez. Kwa kuhitimisha ametoa shukrani na shuku ambayo inawaunganisha marafiki wote wa ndani ya hali halisi ya Wakarismatiki, na wale wote ambao wanahisi haja ya kuzaliwa kwa mara nyingine tena katika kipindi hiki cha majaribu na udhaifu mkubwa na kutaka kufanya uzoefu wa uhusho wa Roho Mtakatifu.

16 May 2021, 13:23