Kardinali Maurice Piat  wa Jimbo Kuu la  Port-Louis, nchini Mauritius Kardinali Maurice Piat wa Jimbo Kuu la Port-Louis, nchini Mauritius  

Mauritius:Maeneo Ibada katika kipindi cha Pasaka yamefungwa kutokana na janga

Maadhimisho ya sherehe za Pasaka kwa waamini katika maeneo ya ibada hayakufanyika kutokana na janga la covid hata ibada za ndoa nchini Mauritius.Kwa mujibu wa Kardinali Maurice Piat ameadhimisha Misa ikitangazwa moja kwa moja na televisheni.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Makanisa yamefungwa ya Port-Louis nchini Mauritius kwa sababu ya janga la Covid-19 ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo katika sherehe zote za Pasaka. Hii ni tangu tarehe Mosi Aprili 2021, ambapo mamlaka ya serikali, iliamua kufunga maeneo yote ya ibada ili kuzuia maambuki zaidi ya virusi vya Corona au  Covid-19. Kwa njia ya  maombi ya Jimbo la Port-Louis, hata hivyo   wamewezesha kutangaza moja kwa moja liturujia za Juma Kuu zilizoongozwa na Kardinali Maurice Piat, katika Kanisa Kuu la Saint-Louis na Jumapili  tarehe 4 Aprili, Kardinali ametangaza ujumbe wa kiutamaduni wa Pasaka mbele ya vyombo vya habari kwa maana ya Runinga kuwaelekea waamini wote.

Kwa mujibu wa taarifa ya  Tovuti ya Jimbo Kuu la Port-Louis, upo uwezekano lakini wa kupelekea komunio kwa wagonjwa na kutoa sakramenti ya mpako wa wagonjwa au kuomba kukutana na kuhani kwa ajili ya kuungana au kusindikizwa kiroho lakini wakihifadhi kanuni na sheria za kiafya zilizowekwa ili kuzuia maambukizi zaidi ya corona. Kardinali Piat amesisitiza haya hata ni masuala ya kuwa na busara katika kufuata kanuni na ambayo wao pia wanatakiwa kutoa mfano. Na kwa maana hiyo haiwezekani kufanya ibada pia za ndoa za kidini hadi itakapotangwazwa tena.

04 April 2021, 15:13