MISA YA MKESHA WA PASAKA KATIKA KANISA KUU LA KABURI TAKATIFU YERUSALEMU MISA YA MKESHA WA PASAKA KATIKA KANISA KUU LA KABURI TAKATIFU YERUSALEMU 

Nchi Takatifu,Patriaki Pizzaballa:Jifunze kwa wanawake waliokwenda Kaburi la Yesu

Ni kujifunza kutoka kwa wanawake waliokwenda katika Kaburi la Yesu kwa ajili ya kutangaza ufufuko na matumaini.Amesema hayoPatriaki wa Kilatini Pizzaballa wakati wa mkesho wa Pasaka katika Kaburi Takatifu huko Yerusalemu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mkesha wa Pasaka ya Bwana, Patriaki wa Yerusalemu, Pierbatista Pizzaballa ametoa mahubiri yake kuhusu masomo ya liturujia hiyo akiwaalika waamini awali ya yote kujifunza kutoka kwa wanawake ambao alfajiri mapema ya Pasaka walikwenda katika Kaburi la Yesu ili kupaka mafuta na manukato mwili wake.  Wanawake wanao uwezo wa kuvumilia uchungu, wa kwenda mbali zaidi ya kushindwa na hawaachi kutumia fedha zao ili kununua mahitaji kwa ajili ya kutoa heshima kwa Yesu, siyo wa kushindwa bali aliyependwa, amesisitiza Patriaki Pizzaballa.

Upendo wa wanawake hao kwa Yesu haukuzimika kwa sababu ya kifo chake. Uhusiano na Mwalimu wao, ulikwenda zaidi ya ndoto za binadamu wa ufalme mpya. Upendo wa kweli ni wa bure, hautegemei mambo yoyote na wala kujua kifo. Patriaki ameeleza kuwa wanawake wanaoelezwa katika Injili walinunua mahitaji ya lazima tayari kabla ya kuingia usiku wa Jumamosi, na hawakusubiri siku nyingine baadaye, walitafuta hata mafuta kwa sababu ya maziko yenye hadhi. Walitumia fedha zao ili kutaka kuupaka mwili wa mpendwa mwalimu wa Galilaya na katika wao kuna haja ya kutambua namna ya kuishi kwa kupoteza, yaani kutumia kwa dhati maisha yetu kwa ajili ya upendo wa Kristo, kuutazama msalaba kama kipimo cha upendo ule ambao unatukomba na kaburi hilo wazi kama tangazo la maisha ya milele kwetu sisi sote.”

MAANDAMANO KUANZA IBADA YA MKESHA YERUSALEMU
MAANDAMANO KUANZA IBADA YA MKESHA YERUSALEMU

Akizungumzia juu ya ufufuko, Patriaki Pizzaballa amesema kuwa hakuna nadharia inayoweza kushawishi na kuondoa ukweli kuwa ufufuo unaweza kupatikana kwa kufanya uzoefu, lakini hata hivyo leo hii kuna haja ya shuhudia hasa ishara zioneshwe za Mfufuka kati yetu ambaye anatuangazia kwa kushangaza na uaminifu  kwamba ulimwengu hauko tena katika nguvu ya kifo. Mashuhuda wa leo hii ni wale ambao licha ya matatizo, uchungu, upweke, magonjwa na ukosefu wa haki, wanatumia maisha yao kuunda fursa za haki, za upendo na ukarimu, amesisitiza Patriaki wa Yerusalemu.

BARAKA YA PATRIAKI PIERBATISTA PIZZABALLA
BARAKA YA PATRIAKI PIERBATISTA PIZZABALLA

Ni wale ambao wanatambua kusamehe, kwa sababu wanahisi tayari kusamehewa. Ni wale ambao katika ukimya wa kila siku wanatoa maisha yao kwa ajili ya watoto wao na watoto wa wengine, na ambao wanawafikiria kuwa kila mtu ni sehemu ya hatima yake, na wanajikita kuhudumia kwa upendo na shauku kubwa wakijisahau wao binafsi. Patriaki Pizzaballa amesema kuwa shuhuda wa kwanza ni Kanisa mahali ambamo Mfufuka anazungumza nasi, kwa njia ya Sakramenti na tangazo la Neno. Kanisa ambalo linapaswa kuwa jasiri na siyo kuogopa upweke, kutoeleweka na lazima kuonesha mfufuka kwa utulivu ulimwenguni na Neno lililo wazi na uhakika kwa ushuhuda wa uhuru, uamuzi na shauku.

MAJI YA BARAKA WAKATI WA MKESHA WA PASAKA YERUSALEMU
MAJI YA BARAKA WAKATI WA MKESHA WA PASAKA YERUSALEMU

Hatimaye Patriaki Pizzaballa amesisitiza kwamba “hautakutana na mfufuka ikiwa hautaenda Kaburini na ukabaki umefungwa kwenye karamu kuu binafsi”, kwamba “ikiwa utaona na kukutana na yule Mfufuka, huwezi kubaki bila kusonga mbele na kwamba leo hii ni zaidi awali , umuhimu wa matumaini. Kristo aliyefufuka ndiye tumaini letu na hii ndiyo tunayoitwa kushuhudia, tukienda kila mahali, bila kusìmama . Na zaidi amesisitiza kuwa “Tusirudi nyuma au kujifungia kwa hofu zetu. Tusiruhusu kifo na watawala wake kututishia (...) Ufufuko ni tangazo la furaha mpya ambayo hupasua ulimwengu ambao hauwezi kubaki umefungwa katika mahali hapa, lakini ambao lazima bado ufikie kila mtu kutoka hapa leo”. Amehitimisha.

04 April 2021, 15:19