KILIMO NCHINI BENIN-NIGER KILIMO NCHINI BENIN-NIGER 

Secam na washirika wake:Ulaya ikuze ushirikiano na Afrika wa haki&uwajibikaji!

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagacar(SECAM) na washirika wake wanaandika waraka wa pamoja kwa Jumuiya ya UA na Ulaya kutokana na matarajio ya mkutano wao wa Jumuiya hizo mbili utakaofanyika mwaka huu.Katika barua wanasema barani Afrika,chakula ni haki msingi ya kibinadamu,sio bidhaa mikononi mwa watu wachache waliochaguliwa ambao huamua bei kupitia tasnia zao za chakula.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ushirikiano mpya wa Ulaya na sekta za kilimo na chakula za Afrika, ndiyo itakuwa mada ya mkutano muhimu ujao kati ya Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Afrika (UA). Mkutano huo hapo awali ulitarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 2020, lakini iliahirishwa hadi 2021 kutokana na  mgogoro wa Covid-19. Mkutano huo unakusudia kufafanua ushirikiano wa muda mrefu kati ya pwani mbili za Mediterania ndani ya mfumo wa mpya na shauku ya Ushirikiano wa Afrika na Ulaya, ambapo Umoja wa Ulaya (EU)  umekuwa ukifanya kazi tangu 2018, hasa kupitia Kikosi Maalum cha "Afrika Vijijini", kikifuatilia ahadi zilizotolewa mnamo 2017. Lengo ni kuzindua uwekezaji wa umma na wa kibinafsi katika kilimo endelevu barani Afrika, kuongeza ubadilishanaji wa kibiashara kati ya mabara haya mawili, kushiriki maarifa na kujua na kuunda ajira na shughuli zinazoingiza mapato katika maeneo ya vijijini barani Afrika.

Kwa kuzingatia mkutano ujao, ambao utalazimika kukamilisha ushirikiano huu ulioimarishwa kati ya uchumi wa mabara haya mawili, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM), na mashirika mengine kadhaa ya Kanisa la Afrika, pamoja na mashirika ya kijamii (CSO) ), wametoa waraka wao wa  pamoja ukirudia kuonesha wasiwasi kadhaa juu ya nyayo za mkakati  mpya wa pamoja wa Ulaya na Afrika. Kwa mujibu wa Kanisa la Kiafrika, kiukweli mtu aliyekosa kisomo ni shida kubwa ambazo zinapaswa  kukabiliwa nazo, kuanzia na ukiritimba wa sekta ya chakula na wafanyabiashara wa tasnia ya kilimo, na uharibifu wanaosababisha mazingira, ardhi, rasilimali maji, bioanuai na lishe na afya ya watu wa Kiafrika. Ingawa lengo lililotangazwa ni kujenga maisha ya baadaye yenye mafanikio zaidi, yenye amani zaidi na endelevu kwa wote hata hivyo majumu matano yaliyopendekezwa katika uwanja wa nishati, utaftaji wa habari, uwekezaji wa ndani, amani na uhamiaji sio dogo juu ya mahitaji ya asilimai 60% ya familia za Kiafrika ambazo hutegemea kilimo cha familia na uzalishaji mdogo wa chakula kwa maisha yao.

Ingawa wakulima wadogo, wachungaji, wavuvi na jumuiya za misitu ndio sehemu kuu ya Afrika ya vijijini, watendaji wanaotawala eneo hili ni wa nje: wafadhili, wafanyabiashara, mashirika ya misaada ya kimataifa na ya nchi mbili. Sera za kiuchumi barani zinaendelea kuamriwa na kaskazini mwa ulimwengu ambazo zinapendelea uwekezaji wa kibinafsi na ushirikiano wa umma na kibinafsi, kilimo, kinacholenga kuuza nje na uuzaji wa ardhi kwa unyonyaji wa mali asili bila kutathmini, au licha ya athari ya mazingira ya shughuli hizi, wataka huo unabainisha. Katika suala hili, Kanisa la Afrika linatofautisha njia hii na maono mengine kwamba "Kwa asilimia 60 ya Waafrika ambao wanategemea kilimo kwa maisha yao  ardhi sio bidhaa wala faida ya mtu binafsi. Ni zawadi ya Mungu na ya mababu zetu ambayo huamua utambulisho wetu kama wanadamu, heshima yetu, hisia zetu za kuwa watu”.

Zaidi ya hayo barani Afrika, chakula ni haki msingi ya kibinadamu, sio bidhaa mikononi mwa watu wachache waliochaguliwa ambao huamua bei kupitia tasnia zao za chakula”. Taarifa hiyo inasisitiza tena kwamba sekta ya kilimo ndio nguzo ya uchumi wa Afrika, kama ilivyo kwa nchi nyingi ulimwenguni: sio tu inahakikishia usalama bora wa chakula na lishe, faida za mazingira na uthabiti zaidi kwa mabadiliko ya hali ya hewa, lakini pia inachukua jukumu n anafasi msingi katika mshikamano na utamaduni za jumuiya”. Kwa maana nyingine chaguzi za sera ya uchumi kwa zina muktadha wa nguvu kubwa pia  kwa mambo haya. Tamko lililotiwa saini na SECAM kwa  maana hiyo linatoa mfululizo wa mapendekezo ambayo yanalenga kuunda upya uhusiano wa kisiasa na uchumi wa bara ili kuanzisha ushirikiano ambao ni wa haki na uwajibikaji. Kati ya hizi, ya kwamnza ni ile ya uwekezaji mkubwa katika kilimo-ekolojia ili kuimarisha, kwa njia endelevu, usalama wa chakula na enzi kuu, na kwa maana hiyo kupunguza umaskini na njaa, kuhifadhi bioanuwai na kuheshimu maarifa ya mababu ya wakazi wa eneo hilo.

Hili ni suala  la  kutafakari tena mtindo wa sasa wa maendeleo ya kilimo barani Afrika na kutambua jukumu muhimu la biashara za familia, ushirika na wakulima wadogo. Kwa maana hiyo pia kuna pendekezo la kuhakikisha kuwa ununuzi wote mkubwa wa ardhi unatanguliwa na tathmini ya uwazi ya athari za mazingira, kijamii na kitamaduni na idhini inayofahamishwa ya jamii za asili na za wakulima. SECAM inaomba kusitisha kupunguzwa kwa maliasili ya bara hili kama bidhaa zinazowindwa na mashirika ya kimataifa. Hatimaye hoja nyingine za waraka huo zinahusu haki za binadamu, ambazo Kanisa la Afrika linataka sheria. Sheriaza mataifa na ya kimataifa, kwa ajili ya  amani na usalama, hali muhimu kwa maendeleo barani Afrika.

01 March 2021, 17:43