Wachungaji wakishiriki maisha ya furaha ya utume na wazalendo wa Papua Guinea Mpya Wachungaji wakishiriki maisha ya furaha ya utume na wazalendo wa Papua Guinea Mpya 

Papua Guinea mpya:Mambo ya maisha,heshima na hadhi ya maisha

Vijana wa shule na kutoka maparokia ya mji wa Boroko nchini Papua Guine Mpya wameshiriki mkutano uliongozwa na mada"Mambo ya Maisha:Heshima na hadhi ya maisha kwa kuwasaidia kujua namna ya kutetea maisa tangu kutungwa kwake hadi kifo chake.Askofu Mkuu wa Port Moresby,Kardinali John Ribat,amefafanua maendeleo ya mipango ya kiroho na sakramenti kwa vijana katika Madhabahu ya Jimbo Kuu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Vipindi vya sala, kushirikishana, uwakilishi, maswali na mijadala ni mambo yaliyokuwa uameandaliwa kwenye mkutano ulioongozwa na mada “Mpango wa Mambo ya Maisha” kwa mtazamo wa kuheshimu hadhi ya maisha, ambao ulilenga vijana kutoka shule tofauti na baadhi ya maparokia ya mji wa Boroko huko Papua Guinea Mpya.Tukio hilo lililiratibiwa na Tume ya SOCOM ya Baraza la  Maaskofu Katoliki na msaada wa Caritas (PNG),  tume ya Maisha ya Familia, Vijana na Tume nyingine, ambapo walisisitizia kuhusu heshima hiyo hasa wakati wa kutunga mimba mkutano ulifanyika hivi karibuni, tarehe 13 Machi Machi 2021 katika Madhabahu ya  Bikira Maria Msaada wa Wakristo huko Boroko ya Jimbo Kuu. Akiwahutubia vijana washiriki, mratibu wa mpango huo, Padre Ambrose Pereira (sdb), alisema kwamba ni muhimu kushirikisha na kile ambacho wanajifunza katika shule zao   na parokia zao. Vijana ni miongoni mwa watumiaji wakuu wa mitandao ya kijamii  na mpango huo ulilenga kuwapa jukwaa la mafunzo  ambalo wataweza kushirikishana imani yao na kukua kiroho. Pongezi  la mpango huo pia zilitoka kwa Askofu Mkuu wa Port Moresby, Kardinali John Ribat, ambaye amefafanua maendeleo ya mipango ya kiroho na sakramenti kwa vijana katika Madhabahu ya Bikira Maria Msaada wa wakristo.

Naye  kiongozi mwenginem Sr. Alice Fulgencio, FMA) kwa vajana amefafanua kwa wanafunzi hao juu ya  tofauti kati ya 'pro-life' na 'pro-choice' kwa maana ya muktadha wa utetezi wa maisha kuanzisha mwanzo wa kutungwa hadi kifo chake na muktadha mwingine wa kisasa ambao unakuwa na upendelea wa kuchagua kuondoa maisha. Na ili kuweza kuwakilisha vema, ushuhuda kwa njia ya video kuhusu  mtetezi wa maisha ulioneshwa, kwa lengo la kuwasaidia vijana  hawa ili kufanya maamuzi kulingana na maadili na thamani kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa Katoliki, na si katika mantiki ya ulimwengu. Waandaaji wa mpango huo walitegemea  zaidi ya washiriki 300, lakini idadi ilikuwa ndogo kutokana na hali halisi ya janga la sasa la virusi vya corona

Tukirudi katika suala la neno Pro -life na pro -choice, tulitazame kwa umakini. Pro-choice: ni neno linalojieleza kuhuu uchaguzi, kwa maana ya yule ambaye anakubaliana  au kuchagua na kuhalishwa utoaji wa mimba, kwa maana nyingine kuchagua kutoa. Utoaji mimba leo hii unawakilisha moja ya masuala makubwa ambayo yanauhusu ulimwengu wote, wakati huo huo husababisha majadiliano na kugawanya maoni ya umma kati ya wale wanaokubali (pro- choce) na wale ambao wanapinga na kwa maana  hiyo kutetea maisha ( Pro -lfe). Kukatisha mimba kinyume na sheria (wakati mwingine huitwa “utoaji mimba”. Kwa hali hali isiyokuwa wazi sana, mjadala unatofautisha nafasi mbili kuu: (Pro-life), wale ambao wanapenda maisha, na wangependelea kuona utoaji mimba unakuwa haramu. Wafuasi wa nadharia hizi wanachukulia kiini kuwa mwanadamu katika mambo yote ambayo kwa sababu hii kinapaswa kufurahia haki sawa ya kuishi kama mwanadamu baada ya kuzaliwa.

Na Pro choice yaani (kwa niaba ya chaguo), ambayo ni pamoja na wale ambao hukabidhi chaguo kwa suala hili kwa tathmini binafsi ya mwanamke, na kwa yeye tu. Hawa licha ya kutokanusha dhamana ya maisha ya mwanadamu, wanathibitisha kwamba mwanamke mjamzito lazima awe na uwezo wa kuchagua katika hali nyingine na ndani kesi ya mipaka iliyowekwa na sheria, haki ya kukatisha ujauzito. Kwa bahati mbaya, katika jamii ya sasa utoaji mimba mara nyingi huonekana kama njia ya uzazi wa mpango na kwamba sababu zinazosababisha uchaguzi huu ni matokeo ya ubinafsi na ukosefu wa uwajibikaji. Shida ni kwamba ngono inachukuliwa kama mwiko na mimba nyingi ambazo hawazitaki zisingekuwapo ikiwa kungekuwapo na elimu zaidi ya ngono na elimu ya uzazi wa mpango, hasa kwa vijana kuanzia walio katika shule za kati.

Matatizo ya ukosefu wa msimamo, mimba za utoto, ajira, anasa wakati mwingine na vikwazo halisi vya kijamii vimepeleka msukumo wa wanawake wangi kujikuta wanafanya maamuzi kinyume na sheria hasa tendo la  kukubali kutoa mimba. Utoaji mimba siyo jambo bora, hata katika  suala la uchaguzi, badala yake ni lazima  kujikita katika kujenga utamaduni ambao unafundisha, kuheshimu na kupenda maisha kwa pamoja. Katika nyakati za karne ya sasa ni kazi ngumu hasa kukabiliana na mivutano ya baadhi ya mashirika mengine ya kijamii ambayo yanatoa msukumo wa kutengua hata sheria ya utoaji mimba na kugusa dhamiri na hisia za kujitegemea kwa mwanamke. Vilevile utoaji wa mimba kwa upande wa wakatoliki ni suala lisilo la haki, kukosa kuheshimu maisha na haki za maisha ya wanawake. Baadhi ya mataifa kama Marekani, Ulaya, na kwingineko yamekuwa na mapendekezo mapya kuhusu sheria inayotaka kuruhusu utoaji mimba, ambayo kwa bahati mbaya wanapata washabiki wake katika  nchi nyingi ambazo zimeonekana kuhalisha mfano nchini Ireland.

Suala la utoaji mimba limeibua kwa wastani mjadala mkubwa. Kwa wakatoliki tunajua wazi thamaini ya maisha. Lakini je ni watu wangapi wasio na huruma hata kati ya familia, jamii kazini na sehemu nyingine nyingi, wanakuwa mstari wa mbele kushauri na kupendelea utoaji mimba huo?. Na zaidi wengine wengi  wanapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Yatosha kutazama katika luninga au kusikiliza katika radio utaona au  kusikiliza majadiliano ambayo yanahusu anasa, bila uwepo wa hali ya  hewa ya Mungu. Hayo yote na mengine yamempelekea mwanadamu kufikia hatua ya kutojali uhai wa mtu, kwa maana utafikiri anaua mbu kutoka tumboni mwa mwanamke au kama  ni uchafu, hiki ni kilio hata cha Mungu ambaye ameumba binadamu kwa mfano na sura yake. Binadamu hata amesahau kabisa hasira aliyokuwa  nayo juu ya dhambi  ya Sodoma na Gomora, na maombi ya mtetezi mkuu, Baba wa Imani Ibrahimu kutoangamiza maisha, hata mmoja.

Kanisa litaendelea na wote wenye mapenzi mema kutetea uhai wa binadamu tangu kutungwa hadi kifo chake; kama Baba Mtakatifu Francisko ambaye hachoki kuhimiza utetezi wa kila mtu kuanzia kiinitete, mtoto, mtu mzima hadi mzee. Ni uwajibu wa kila jamii na jumuiya nzima ya Kanisa kuelimisha watoto wetu, ndani ya familia, bila kuogopa, awe baba au mama. Tatizo kubwa la akina baba ni kushindwa kuelekeza watoto wao, kwa sababu nao wanawapa mimba vijana wengine nje ya ndoa. Kumrudia Mungu na kujua wajibu wetu wa kulinda uhai ni muhimu kuanzia kutungwa kwake hadi kifo cha kawaida cha mtu.

17 March 2021, 16:45