LAZIMA KUPAMBANA DHIDI YA TABIA ZA KIBAGUZI KWA WALIO NA VVU NA UKIMWI LAZIMA KUPAMBANA DHIDI YA TABIA ZA KIBAGUZI KWA WALIO NA VVU NA UKIMWI 

Malawi:Tabia za ubaguzi dhidi ya wenye VVU zikome

Onyo kali dhidi ya ubaguzi kwa watu wenye ugonjwa wa virusi vya ukimwi limetolewa na Mratibu wa Kitaifa wa Afya Katoliki wa Baraza la Maaskofu nchini Malawi."Sisi sote ni sawa,lazima tusaidiane na kutiana moyo ili watu wenye virusi vya ukimwi(VVU) pia washiriki katika shughuli za Kanisa na katika kazi ya maendeleo ya nchi".

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Sisi sote ni sawa, lazima tusaidiane na kutiana moyo, ili watu wenye virusi vya ukimwi(VVU) pia washiriki katika shughuli za Kanisa na katika kazi ya maendeleo ya nchi. Ni Onyo lililozinduliwa na mratibu wa kitaifa wa afya Katoliki wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Malawi (ECM), Bertha Magomero, akiwalenga wale wote ambao wana tabia ya kibaguzi kwa watu wenye VVU.

Wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa usimamizi uliofanyika katika Wilaya ya Machinga, Liwonde, na watu wa kujitolea kusaidia waathiriwa wa virusi kutoka Baraza la maskofu, viongozi wa dini na wasambazaji wa vifaa vya kupima VVU wanaofanya kazi chini ya mpango wa Imani na shughuli za kijumuiya (FCI), Bi Magomero alisisitiza kuwa ni  kwa njia ya kutokuwa na ubaguzi tu, nchi itaweza kuwa mahali pazuri pa kuishi.

Aidha amesema kuwa inasikitisha kutambua kwamba hata jamaa na ndugu  ndio wanakuwa wa  kwanza kubagua watu wanaoishi na VVU na UKIMWI. Watu hawa wanaishi maisha yenye afya kuliko wale ambao hawajajaribiwa. Bi Magomero ameongeza kuwa mitazamo hii inasababisha watu wengi wenye VVU kutokubali matokeo ya vipimo  na kuacha kuendelea kupata msaada wa antiretrovirals (ARVs), kwa kuchochea kuenea zaidi kwa virusi. “Kuna maisha zaidi katika kujua hali yako kuliko kuishi kwa kukataa”, alisisitiza mratibu huyo.

Kuna wengi ambao huficha hali zao au huepuka matibabu ili kuepuka kubaguliwa, kutelekezwa au kutendwa vibaya na marafiki na jamaa. Na ni kwa sababu hii kwamba kwa sasa Baraza la Maaskofu Malawi (ECM), kupitia Tume za Afya na Mawasiliano, imetaka kuhusika zaidi katika upimaji wa VVU, matibabu na uzingatiaji wa matibabu katika vita dhidi ya janga hilo katika wilaya za Machinga na Mangochi, kama sehemu ya Mpango wa Imani na shughuli za kijumuiya (FCI) ya Baraza la Maaskfu nchini Malawi.

Miongoni mwa ushuhuda uliojitokeza wakati wa mkutano, ni ule wa VVU anayepata matibabu na ambaye alisema alipimwa akiwa na ugonjwa huo mnamo 1983 na akaanza kutumia tiba ya ARV mwaka huo huo. “Ilikuwa ngumu kukubali kwamba nitaitumia kwa maisha yangu yote ingawa nilikubali baadaye, lakini kutokana na unyanyapaa katika familia niliacha kwa sababu nilikuwa na hakika kuwa ni bora kufa kuliko kuishi na VVU / UKIMWI . Baada ya mikutano kadhaa na watu wa wajitolea, nilikuwa na hakika kwamba nilitaka kuendelea kuishi kwa furaha na VVU, na niliamua kuanza kutumia ARVs tena, uamuzi ambao sitajuta kamwe.” Mmoja wa viongozi wa kidini wa Mtakatifu Patrick wa parokia ya Mofolo Woyera amesema wataendelea na kazi yao ya kusindikiza, kuzuia na kueneza ujumbe wa matumaini kwa wote. Tangu mpango wa FCI uanze, wengi wameitikia.

19 March 2021, 13:40