2021.03.05 Hija y Papa Francisko nchi Iraq 2021.03.05 Hija y Papa Francisko nchi Iraq 

Hija ya Papa Fracisko nchini Iraq:Furaha ya watawa na Papa

Uwepo wa dini nchini Iraq ni muhimu sana na zaidi ni uwepo hai wa Kristo ambao kila mmoja wao amemtambua tangu kuzaliwa na baadaye kumtambua katika mateso na vita ambavyo wamepitia.Kristo aliyependa kama mfariji na uwepo wake kwa uhakika kuwa karibu nao.Niushuhuda wa mtawa,mzaliwa wa Iraq akishuhudia ukristo katika nchi yake kwenye muktadha wa ziara ya Kitume ya Papa Franciska nchini humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kufika kwa Papa Jijini Baghdad ni pamoja na kukutana na maaskofu,  watawa na makatekista wa Kanisa Kuu la ‘Sayidat al-Nejat’ yaani Mama yetu wa Mwokozi mahali ambapo bado panaonesha ishara za mateso ya wanairaq kutokana na uwanja wa mashambulizi mawili ya kigaidi. Shambulio la kwanza lilitokea mnamo tarehe 31 oktoba 2010, ambapo walipoteza maisha yao watu 48 mingoni mwake wakiwemo mapadre wawili na majeruhi karibia 70 hivi. Jengo hili lilizinduliwa kunamo Machi 1968 lililojenga juu ya Kanisa dogo la mwaka 1952 ili kukaribisa wakatoliki Siria ambao daima ndiyo wengi. Vatican news, ikizungumza na Sr. Narjis Henti wa Iraq katika mkesha kabla ya Papa, ameelezea mantiki mbali mbali zinazowakilisha wakristo na dini katika Nchi ambayo Papa Francisko anatembelea ili kuimarisha imani na kuwatia moyo kwa ajili ya maelewano kijamii.

ZIARA YA PAPA NCHINI IRAQ
ZIARA YA PAPA NCHINI IRAQ

Uwepo wa dini nchini Iraq ni muhimu

Sr. Henti amesema kuwa uwepo wa dini nchini Iraq ni muhimu sana na zaidi ni uwepo wa Kristo, ambao kila mmoja wao amemtambua Mungu tangu kuzaliwa na baadaye kumtambua katika mateso na vita ambavyo wamepitia. Kristo aliyependa kama mfariji na uwepo wake kwa uhakika karibu nao. Sista Anashuudia kuwa tangu  akiwa mgogo alihisi uwepo wa Kristo katika maisha yake na katika familia yake na hivyo aliamua kujibu wito wake. Kuwa mtawa nchini Iraq pia ni muhimu hata kwa muktadha huo, katika nchi iliyo na Waislamu wengi ambapo uhuru siyo mtimilifu  kama  nchi za Magharibi. Kwa upande wao kuwa hapo kunamaanisha kuwa ndani ya tumbo la Kanisa la Iraq ambalo liko hai na linastawi! Misa, katekisimu, Dominika, jumuiya  inajionesha kuwa hai na kwa kila mmoja wa watawa hao wanawakilisha dhamana ya uhusiano  na Mungu, ambaye ndiye pekee anayetoa furaha na nguvu. 

PAPA AKIWA NA RAIS WA IRAQ
PAPA AKIWA NA RAIS WA IRAQ

Uzoefu wa wakati mgumu wa vita 

Sr. Henti akieleza juu ya wakati mgumu wa vita  na maana ya uwepo wa wakristo nchini humo amesema kuwa nchini Iraq, uwepo wa kidini wa Wakristo umekuwa muhimu kila wakati, hasa katika uhusiano uliojengwa na Waislamu wengi. Uhusiano nao  ni kutokana na kuaminiana. Mkristo machoni mwao ni mtu mwaminifu, mtu anayemjua Mungu, hata ikiwa Mungu ni tofauti na wao. Kwa ajili ya Kanisa kwa ujumla, uwepo wa Kikristo kwa miaka yote umekuwa awali ya yote kuwa ushuhuda na tangu 2003 na kuendelea, lakini pia hapo awali, shuhuda wa kumwaga damu. Na ndivyo ilivyokuwa kwa sisita mwenzake aliyeuawa mnamo 2002, lakini pia huko Mosul kwa baba wao  wa kiroho au kwa askofu . Wote  hao wamekuwa mashuhuda  wa furaha na ujasiri, mashuhuda wa uwepo wa Yesu. Na ushuhuda huu haukuwa muhimu tu kwa Wakristo, lakini pia kwa Wairaq woteameisitiza Sr. Henti.

MAANDALIZI YA NYIMBO
MAANDALIZI YA NYIMBO

Misa itaayofanyika huko Erbil ya kuhitimisha ziara ya Papa

Na katika Misa itakayofanyika katika Uwanja wa Erbil Jumapili ikiwa ni siku ya mwisho ya Ziara ya Papa ambayo itaongozwa na nyimbo kwa lugha mbali mbali, Sr Henti amesema kuwa, Muziki ni moyo wa ubinadamu na tangu mwanzo umechukua nafasi msingi hata nchini Iraq. Ilikuwa ni mila  na desturi ya kurithishana kwa sauti ambayo imewafanya kubaki wameungana na Kristo. “Muziki ni moyo unaotuunganisha sisi sote. Kwa maana hiyo, ikiwa mtu anasikia wimbo au sala kwa Kiaramu au Kiarabu au kwa lugha nyingine za hapa mahalia, sisi sote tunajisikia tumeunganishwa na urithi ambao ni wetu, na muziki unaofikia mioyo, ishara inayokumbusha ujumbe wa Papa katika udugu”, amesema Sr Henti.

MISA JUMAPILI ITAADHIMISHWA ERBIL KATIKA UWANJA WA MICHEZO
MISA JUMAPILI ITAADHIMISHWA ERBIL KATIKA UWANJA WA MICHEZO

Na hatimaye amesema “Kiukweli, udugu unaweza kuoneshwa na urafiki, lakini pia kwa kuhimiza mioyo nakusema:tuko hapa na nchi yetu itaendelea, na hiyo  ndiyo inafanya muziki. Zaidi ya yote, Kanisa daima limeshuhudia uwepo wa Bwana ambao hunaibuka na nyimbo na  maombi ya waamini, ambao wanaweza kuweka kumbu kumbu ya urithi wa kiutamaduni tangu utoto!.

05 March 2021, 13:30