2021.01.12 Mtakatifu Yosefu 2021.01.12 Mtakatifu Yosefu 

Uzinduzi wa mfuko wa kusaidia Taasisi za Mtakatifu Yosefu

Kuanzia na tafakari iliyo kwenye barua na mwaliko wa kuiga Baba mwenye ujasiri wa ubunifu,Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACS) limezindua mfuko kwa ajili ya mchango wa kusaidia mipango mbali mbali ya mashirikia yanayoitwa jina la Mtaatifu Yosefu na kujikita katika shughuli za upendo Barani Amerika ya Kusini,Afrika,Nchi ya Mashariki, Ulaya Mashariki na Asia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji(ACS) limezindua mfuko wa kusaidia Taasisi zote ulimwenguni ambazo zinatumia jina la Mtakatifu Yosefu kama Msimamizi wao. Fursa hiyo imetokana na Barua ya Kitume ya Patris Corde iliyochapishwa mnamo Desemba iliyopita, ambayo Baba Mtakatifu Francisko alitangaza Mwaka maalum wa Mtakatifu Josefu wakati wa maadhimisho ya miaka 150 ya kutangazwa kwa mtakatifu huyo huyo kuwa msimamizi wa Kanisa zima. Kuanzia tafakari iliyo kwenye barua na mwaliko wa kuiga Baba mwenye ujasiri wa ubunifu, Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACS) limezindua mfuko huo wa fedha kusaidia mipango mbali mbali ambayo inatumia sura ya Mtakatifu huyo mlezi  katika Bara la Amerika ya Kusini, Afrika, Nchi ya Mashariki ya Kati, Ulaya Mashariki na Asia.

Mmoja ya mchango  huo utakuwa ni kwa Kanisa la Mtakatifu Joseph huko Beirut, linalosimamiwa na mapadre wa Kijesuit, ambalo lilipata uharibifu mkubwa kufuatia na mlipuko uliotokea katika bandari ya mji mkuu wa Lebanon mapema Agosti 2020. Mbali na milango na madirisha paa, iliyotengenezwa  karne ya 19, inahitaji hatua za haraka kukarabati. Kwa mujibu wa Padre Gabriel Khayrallah, anayekuhudumia kanisa hilo amesisitiza uhusiano wa kina wa jumuiya  yake na Mtakatifu: “Kama makuhani wa Kijesuit, tunazingatia Mtakatifu Yosefu, mtu wa huruma na upendo”. Katika kisiwa cha Madagascar mpango huo  wa ACS unakusudia kufadhili ujenzi wa nyumba ya parokia huko Betatao, kusaidia makuhani wa parokia inayojumuisha eneo la vijiji vingi. Huko Uruguay, Amerika Kusini, mfukoi huo unakusudia kukusanya pesa kwa ununuzi wa gari la parokia ya Mtakatifu Yosefu huko Lavelleja, wilaya iliyoko kaskazini mwa nchi. Parokia hiyo inahitaji gari kutekeleza mipango ya kijamii na misaada ya katekesi, ambayo mingine iko katika mikoa ya mbali sana.

Shirika la Kipapa la  Kanisa Hitaji (ACS) pia inakusudia kusaidia watawa  56 katika Jimbo la Mtakatifu Joseph nchini Urusi.  Jimbo hili lipo  katika mashariki mwa Siberia, ambalo limetanda juu ya eneo kubwa kama vile Canada. Watawa hao, ambao ni wako katika jumuiya nzima  wamejitolea zaidi kwa watoto wa mitaani na yatima, hasa katika miji mikubwa. “Kwangu mimi ni mfano wa kazi ya kimya na amani. Hajawahi kulalamika katika nyakati ngumu. Hawazungumzu Injili, bali ni matendo tu katika maisha ya wengine ambayo yamejaa shida, kama yetu” ameelezea mmoja wa watawa. Huko Ukraine, Misaada kwa Kanisa la Haja unakusudia kufadhili ukarabati wa nyumba ya watawa yashirika la Wagiriki-Katoliki wa Mtakatifu Joseph huko Potelych. Watawa wanaendesha kituo cha watoto yatima katika jengo lililoharibiwa. “Mtakatifu Joseph ndiye mtakatifu mlinzi wa utume wetu. Kufuata mfano wake mwema, tunafanya kazi yetu kwa unyenyekevu, bila kutarajia thawabu yoyote, na kwa furaha kwa utukufu wa Mungu na kwa faida ya Kanisa ”walisema.

17 February 2021, 14:46