Kardinali Vincent Nichols, Kiongozi wa Kanisa la Uingereza na Walles. Kardinali Vincent Nichols, Kiongozi wa Kanisa la Uingereza na Walles. 

Kwaresima 2021:Kard.Nichols awaalika waamini kuadhimisha Jumatano ya majivu nyumbani

Kuungana tena kama familia,kusali pamoja na kupeana baraka ya pamoja na ishara ya msalaba kwenye paji la uso la kila mmoja na kanuni za kiutamaduni za liturujia ya Jumatano ya majivu:“Kumbuka kuwa wewe ni mavumbi na kwa mavumbi utarudi au “ongoka na kuiamini Injili”,ndiyo ushauri uliotolewa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Walles.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kubaki ndani ya familia na kuomba kwa namna ya pekee huruma ya Mungu dhidi ya virusi vya corona ndiyo ushauri ameutoa Kardinali Vincent Nichols, rais wa Bwaraza la Maaskofu Uingereza na Walles (Cbcew), kwa waamini, watu Mungu katika kuadhimisha Siku ya Jumatano ya majivu bila kukusanyika katika kuweza kuzuia maambukizi zaidi. "Mwaka huu kupakwa majivu Kanisani itakuwa ngumu" anaandika Askofu Mkuu wa Westminster katika barua yake ya kichungaji iliyochapishwa tarehe 15 Februari 2021 ambapo anaeleza kuwa "hata kama baadhi ya makanisa yatabaki yamefunguliwa kwa ajili ya maadhimisho ya ibaada za misa, maparokia wamepewa maelekezo ya kutofanya ibada ya kiutamaduni ya upakaji wa majivu".

Hata hivyo amebainisha kwamba kuna uwezekano wa kuadhimisha mwanzo wa Kwaresima kwa namna tofauti inayojikita juu ya ukuu wa kiroho wa  ibada ambayo inawakilisha ishara ya nje ya hatua ya kina katika harakati ya moyo kuelekea kwa Bwana tunayempenda.  Pendekezo kwa njia hiyo ni kuungana kama familia, kusali pamoja na kupeana baraka ya pamoja na ishara ya msalaba kwenye paji la uso la kila mmoja na kanuni za kiutamaduni ya liturujia ya Jumatano ya majivu: “Kumbuka kuwa wewe ni mavumbi na kwa mavumbi utarudi au “ongoka na kuiamini Injili”.

Kwa kuongezea kusoma maandishi ya sala yaliyopendekezwa na, Kardinali Nichols anawaalika waamini waombe binafsi, huruma ya Mungu hasa katika nyakati hizi ngumu za janga. Barua hiyo inahitimisha na mwaliko mpya kwa waamini kufungua mioyo yao kwa zawadi ya uwepo wa Mungu ili iweze kuwasaidia, kuwafariji na kuwaimarisha. Kanisa la Uingereza pia limejiandaa kuadhimisha Kwaresima na mawazo yanayowahusi waathiriwa wa Covid-19. Katika kipindi chote cha Kwaresima, kuanzia Jumatano ya Majivu hadi tarehe 4 Aprili ambayo ni Jumapili ya Pasaka, Kanisa la Uiingereza linapendekeza mpango wa wa Kwaresima, ukiwa na mlolongo wa maombi ya kila siku na tafakari juu ya vifungu kadhaa vya Biblia na mada inayoongoza kwa kila wiki.

Waamini nchini Uingereza wataweza kupata tafakari kupitia programu inayoweza kupakuliwa kwenye simu zao za mkono au kwa barua pepe. Tafakari hiyo inatolewa katika muundo tofauti, kutoka kitabu hadi video pia inapatikana kwenye YouTube. Kutoka katika tovuti ya Kanisa la Uingereza ambapo waathiriwa zaidi 100 elfu wa Covid-19 nchini Uingereza pia wanakumbukwa kwa sala, inawezekana pia kupakua kalenda na shughuli kadhaa za kufanya kama familia kila moja ya siku za Kwaresima.

17 February 2021, 14:36