Kipindi cha kwaresima Kipindi cha kwaresima 

Kenya:Maaskofu wahimiza ulazima wa kujenga taifa na kuwajibika

Katika wiki tano za Kwaresima 2021 nchini Kenya kila mmoja itakuwa na mada yake maalum:Ulinzi wa utakatifu wa familia,mafunzo ya kimaadili kwa vijana,kupambana dhidi ya ufisadi,usalama,hatimaye kufuata ustawi wa pamoja.Mada hizo zinaangazia pendekezo la barua ya kichungaji ya Kwaresima 2020 ambapo waamni walitakiwa kuwa waaminifu,wawajibikaji wa wema wa pamoja na kazi ya uumbaji.

Na Sr. Angela Rweaula – Vatican.

Maaskofu chini Kenya wametoa mwaliko katika fursa ya kiutamaduni ya kampeni ya kwaresima iliyozinduliwa Jumamosi tarehe 13 Februari 2021, ikiwa inaongozwa na kali mbiu “kulijenga taifa kwa njia ya utawala jumuishi na aminifu”. Katika msisitizo huo maaskofu wanasema kulijenga taifa lao ni lazima na uwajibikaji wa kila mkenya. Wiki tano za Kwaresima zitakuwa kila mmoja na mada yake maalum: Ulinzi wa utakatifu wa familia; mafunzo ya kimaadili kwa vijana; kupambana dhidi ya ufisadi; usalama; na hatimaye kufuata wema wa pamoja. Mada hizo zitatafakariwa kwa kina katika mwanga wa mapendekezo ya maaskofu ya barua yao ya kichungaji ya Kwaresima mwaka  jana  2020 ambapo walikuwa wamewaalika wakatoliki kuwa waaminifu, wawajibikaji na wakuaminika katika kuratibu wema wa pamoja na kazi ya uumbaji

Katika ujumbe wao kwa mwaka 2021, maaskofu wanaadika kuwa bila mafunzo ya kutosha ya kimaadili ni ngumu kufikia utawala unaojumuisha na uwajibikaji. Katika utangulizi, wa maelekezo hayo, Askofu John Oballa Owaa, wa jimbo la Ngong na rais wa Tume ya Haki na Amani, anasisitiza kwamba malezi mazuri ni msingi wa njia ya utakatifu ambayo Wakristo wote na watu wenye mapenzi mema wameitwa kutekeleza katika sakramenti, kusaidia wengine na kusimamia kwa njia ya uwajibikaji zawadi ambazo Mungu ametupatia”. Kwa mujibu wa maaskofu, nchi hiyo inaonekana kuwa imepoteza leo hii dira ya uadilifu ambayo inaweka huduma ya kujitoa kwa jirani hasa kwa kumweka katikati mtu na mwenendo mzuri wake na kazi zake, kama Yesu alivyofundisha. Mara kadhaa maaskofu wa Kenya walikuwa tayari wamezindua wito huu kutokana na kuongezeka kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Hivi karibuni Askofu wa Ngong alikuwa amethibitisha kuwa Familia ni moja ya maadili ya thamani sana ambayo Kanisa linashikilia na kuhamasisha. Ikiwa mambo yanakwenda vizuri katika familia, jamii inastawi. Ikiwa mambo yanaanza kuharibika, jamii itaathiriwa. Mungu alipendelea kama umoja wa kwanza wa jamii, familia iwe mahali pa utakatifu, umoja na upendo. Ikiwa. Ikiwa familia zote zingeelewa huduma ya Kanisa, unyanyasaji wa kijinsia haungekuwa na nafasi katika jamii”.

Katika maelekezo katika kampeni ya Kwaresima, maaskofu hususan wanaoneesha vitisho vinavyoongezeka katika familia nchini, kuongezeka kwa wasiwasi mimba za utotoni, uchochezi wa vurugu za kisiasa kati ya vijana, ufisadi uliokithiri, ukosefu wa usalama katika baadhi ya mikoa na migawanyiko ambayo ni tishio la umoja wa kitaifa. Mada ambazo Kanisa Katoliki nchini Kenya limeingilia kati mara kwa mara mwaka jana, pamoja na viongozi wengine wa dini wakiwa na wasiwasi juu ya kuanza tena kwa mivutano ya kisiasa nchini na kashfa mpya ya ufisadi zilizoibuka kipindi cha kiangazi iliyopita juu ya usimamizi wa fedha za Covid-19, ambapo pia ziliongezwa mivutano isiyopungua ya kikabila na kijamii inayohusisha vizazi vipya.

Ni katika suala hili ambao kwa dhati maaskofu wanakuwa umakini zaidi na kuthibitisha: “Tuna wasiwasi juu ya mahangaiko na kukata tamaa tunayoona kwenye nyuso za vijana wengi ambao, baada ya kusoma na kupata diploma au digrii, wanalazimika kuondoka nchini au kuishi kwa wanaofanya kazi. Kwa mujibu wa maaskofu hao kutoridhika kwao kunaweza kuwa bomu la wakati na kwa maana hiyo ni jukumu la maadili kuwapa tumaini, na mchango wa taasisi zilizoalikwa kuzingatia vizazi vipya kwa kukuza mipango na shughuli katika mwelekeo huo. Maaskofu wanaongeza: “Kama wajumbe waaminifu wa Kanisa, kama wazalendo lazima tuchukue hatua katika matendo ya dhati ambayo yanasindikiaza na kuwezesha vijana wenye talanta na uwezo, ili kupata kazi au maisha yenye tija pia kupitia upatikanaji wa mikopo na kuwezeshwa mikopo hiyo”.

16 February 2021, 13:33