2020.01.21 Sala ya Kuombea Umoja wa Kikristo 18-25 Januari 2020.01.21 Sala ya Kuombea Umoja wa Kikristo 18-25 Januari  

Ufilipino:Umoja ni zawadi na uwajibikaji wa wakristo kwa ajili ya umoja

Umoja na wakati huo huo ni zawadi na uwajibikaji wa wakristo wote ambao wanaalikwa kuuhamasisha katika ubinadamu wote.Ndivyo wanabainisha Tume ya masuala ya kiekumene ya Baraza la Maaskofu nchini Ufilipino katika fursa ya Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo 18-25 Januari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Umoja na wakati huo huo ni zawadi na uwajibikaji kwa wakristo wote ambao wanaalikwa kuuhamasisha katika ubinadamu wote. Ndiyo maelezo ya mwakilishi wa maaskofu ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya shughuli za kiekumene ya Baraza la Maaskofu nchini Ufilipino(Cbcp), Askofu Mkuu Angelito Lampon, katika ujumbe  kwa njia ya video kwenye fursa ya Wiki ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo inayoendelea hadi tarehe 25 Januari 2021 kwa kuongozwa na mada “Kaeni katika pendo langu: mtazaa matunda mengi” (Gv 15, 5-9). Katika ujumbe huo amesema ikiwa umoja ni zawadi ya Mungu ndani mwake pia ni zoezi ambalo wote wanaalikwa kijibidisha kwa uhai wote ili kuufikia; na hiyo inawezekana tu kwa kuheshimu imani ya kila mmoja na kufurahia tofauti zetu.

Umuhimu wa maombi ya wakristo

Askofu Mkuu huyo wa jimbo la Coatabato, amesisitiza kuwa umuhimu wa ushuhuda wa umoja katika tofauti, kati ya wakristo kwa ajili jumuiya ya kibinadamu ndiyo maana ya kusema jambo kubwa sana la ulimwengu, ambalo umoja wa kweli unawezekana tu kati ya wakristo, lakini pia kwa ubinadamu wote. Umuhimu wa siku nane za sala kwa njia hiyo pia umesisitizwa na Balozi wa Kitume wa Ufilipino, Askofu Mkuu Charles John Brown, ambaye kama ilivyoripotiwa na shirika la habari za maaskofu (Cbcp) amepongeza juhudi zilizofanywa nchini humo kusherehekea mwaka huu pia tukio la kila mwaka la kiekumene, licha ya shida zilizosababishwa na janga la corona. "Uekumene ni zawadi kutoka kwa Mungu, zawadi ambayo inawezekana kupitia maombi", amesisitiza balozi huyo.

Hatoshi kuomba tu lakini usaidizi wa maskini zaidi

Katika fursa ya Wiki, ya Maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo shirika la habari Katoliki la Ufilipino (Licas) linaripoti kuwa msimamizi wa kitume wa Manila, Monsinyo Broderick Pabillo amesisitiza, kwa upande wake, kwamba haitoshi kuombea umoja tu bali ni muhimu kuwa na juhudi za kusaidia maskini na walio hatarini zaidi, hasa katika nyakati hizi za janga. Lazima wote wawe na sauti ya pamoja ili kufanya chanjo ipatikana lakini pia kuzuia unyanyasaji kutoka kwa mamlaka.

21 January 2021, 15:27