2020.01.11 Askofu Mkuu  Paolo Borgia, Balozi wa Kitume nchini Ivory Coast  2020.01.11 Askofu Mkuu Paolo Borgia, Balozi wa Kitume nchini Ivory Coast  

Ask.Mkuu Borgia:Kanisa la Ivory Coast,litoke nje bila kuwa na hofu!

Askofu Mkuu Borgia,Balozi wa Kitume nchini Ivory Coast amekumbusha umuhimu wa kumbu kumbu ya miaka 125 ya Unjilishiji nchini humo na kuwashauri maaskofu wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema na upendo wake,katika safari ya miaka hiyo na kumuomba msamaha wa makosa yaliyotendeka huku wakitathimini shughuli za Kanisa na tafakari ya matendo ya kichungaji ya wakati ujao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Mkutano wa mwaka wa 117 wa Baraza la Maaskofu nchini Avory Cost uliofanyika huko Bonua, jimboni Grand Bassam, Balozi wa Kitume amewashauri jumuiya ya kikanisa iwe na jitihada bila kuogopa na Kanisa linalo toka nje.  Mkutano huo unahitimishwa Jumapili tarehe 24 Januari 2021 kwa maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatufu ikiwa ni hitimisho la Maadhimisho ya Jubilei ya miaka 125 ya Unjilishaji nchini humo.

Ni katika muktadha huo ambapo Askofu Mkuu Paolo Borgia Balozi wa Kitume nchi humo amekumbusha kwa dhati juu ya umuhimu wa kumbu kumbu hiyo na kuwashauri maaskofu wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema mengi ya upendo wake, katika mchakato mzima wa miaka hiyo, na kumuomba kwa unyenyekevu msamaha kwa yale ambayo labda ni makosa yaliyotendeka na zaidi tena kutathimini juu ya shughuli za Kanisa na kutafakari juu ya matendo yote ya kichungaji ya wakati ujao.

Balozi wa kitume amethibitisha kuwa Kanisa lazima liwe jumuiya ya kikanisa ambalo linatambua kuthubutu katika jitihada zake bila kuogopa, na ambao kwa uthabiti wake, bila kuchelea, kwenda hadi mwisho kwa wale wote ambao wako pembezoni mwa jamii na kuwainamia, kugusa ubinadamu wa Kristo ambao unateseka kwa kukosa mahitaji zaidi. Akitazama kwa dhati mada iliyongoza mkutano wa maaskofu hao isemayo: “Elimu nchini Ivory Coast katika huduma yamaendeleo fungamani ya binadamu”, Askofu Mkuu Borgia amehimiza Kanisa kuchangia shughuli zake katika nyanja ya aelimu, kuhamasish utu mpya wa kibinadamu ambao unapendelea mkutano na mazungumzo, na ambayo yanaruhusu maendeleo ya kweli katika ujenzi wa mchakato wa kweli wa njia ya amani”.

Kabla ya kuanza mkutano huo Askofu Mkuu  Ignace Bessi Dogbo, rais wa Baraza la  Maaskofu wa Ivory Coast na askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Korhogo, alisema kuwa “elimu, bila shaka ni chombo kinachofaa zaidi kwa ajili ya  huduma fya maendeleo fungamani ya kibinadamu, kwani inasaidia mtu huyo kufikia kimo chake cha  Kristo kwa kuondoa ukali, mikunyato  na zaidi  kwa kupata fadhila ambazo Injili na dhamiri zinapendekeza.Askofu Mkuu wa Korhogo, katika mantiki hiyo elimu, amesema wahusika wote, wadau wote na washiriki  wa Kanisa, wazazi, walimu na waandishi wa habari lazima wachukue jukumu lao la uwajibikaji tosha.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, amesisitiza  zaidi ya hayo kuwa elimu itamsaidia mtu mzima kwa kiwango ambacho ukuaji wa kisaikolojia unatokana na njia ambazo ni pamoja na mafunzo, marekebisho, ufahamu, na ushirikiano. Wakati wa Misa ya ufunguzi wa mkutano, katika parokia ya Mtakatifu Pietro Claver huko Bonoua, Askofu Bessi Dogbo, aliwaalika  familia ya Mungu kufuata mfano wa Familia Takatifu ya Nazareti ya kujitoa kusomesha watoto wao kwa uchaji. Kwa njia hiyo kiongozi huyo alisema, watoto wataingia katika mpango wa wazazi wao kama Yesu alivyofanya kwa Yosefu na Maria, kupitia utii na ambao ndio wa kwanza kumtii Mungu!

23 January 2021, 13:02