2020.05.15Askofu Joachim NTAHONDEREYE, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini BURUNDI 2020.05.15Askofu Joachim NTAHONDEREYE, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini BURUNDI 

Burundi:Ukuu wa kimisionari kiini cha mafunzo ya kikuhani Bujumbura!

Ilifanyika semina ambayo iliongozwa na mada “tangazo,sakramenti na huduma ya kikuhani katika utume wa Kanisa” katika kituo cha mafunzo ya kikuhani huko Gitega nchini Burundi. Askofu Joachim Ntahondereye, wa Jimbo Muyinga na rais wa Baraza la Maasofu amezungunzia kuwa wameitwa kujiandaa kwa ukomavu kulingana na asili na upekee wa kimisionari wa Kanisa katika changamoto wanazokabiliana nazo Burundi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kuanzia tarehe 28 hadi 30 Desemba 2020, imefanyika Seminana ya mafunzo ya kimisionari kwa ajili ya makuhani, iliyofanyaka  katika Taasisi ya Kikanisa na Elimu katika Seminari Kuu ya Majimbo ya Mtakatifu Yohane Paulo II huko  Gitega nchini Burundi. Semina ya mafunzo imefanyika katika mantiki za shughuli zinazohusiana na Jubilei ya shaba ambayo iliadhimishwa mwezi Mei 2019, katika Seminari muhimu ya Kitaalimungu. Mada iliyoongoza mkutano huo na mijadala kadhaa ilikuwa ni “Tangazo, sakramenti na huduma ya kikuhani katika utume wa Kanisa”. Kati watoa mada tano kwa  siku hizo za tafakari na kukabiliana kati ya makuhani hao ya kwanza iliongozwa na Monsinyo Nestor Niyokindi, makamu Askofu Mkuu wa Gitega isemayo “Mafudisho ya kimisionari ya kipapa: mfuko na ufunguzi ulio wazi.  Kwa kukumbusha Mtakatifu Yohane Paulo II”, amewaalikwa washriki kuwa na  utambuzi huu na kuwaomba wote watambue kuondoa  zile mantiki za kuhifadhi kichungaji na kuiga mtindo mpya wa  kutoka nje kwa ajili ya uinjilishaji.

Aliyekuwa akiongoza mkutano huo alikuwa ni Ndugu Emmanuel Ntakarutimana wa Shirika la Wahubiri) ambaye  alijaribu kukabiliana na mada Roho na jitihada za kimisionari za Kanisa la Burundi, hali halisi, wadau msingi na matarajio ya baadaye. Akidadavua alibainisha lengo la kimisionari ni kuwataka  watu wote  waweze kumjua Kristo yaani kwamba wakristo wasitazame nje tu,  badala wote wanaalikwa kuongokea daima Kristo kuanzia ndani mwao, na kwa maana hiyo amesisitizia juu ya  vigenzo viwili vya kimisionari, kwa maana ya ndani na ya nje. Hata hivyo mwongoza mkutano huo amependekeza michato ya tafakari tofauti katika uhusiano na mantiki hizi mbili.

Naye Askofu Joachim Ntahondereye, wa Jimbo katoliki la  Muyinga na rais wa Baraza la Maasofu nchini Burundi,amezungunzia juu ya  sanduku la vifaa vya utunzaji bora wa kichungaji wa Kanisa la Burundi, yaani Sanduku ambalo amesema kuwa wameitwa kuchukua na kujiandaa kwa ukomavu kulingana na asili na upekee wa kimisionari wa Kanisa katika changamoto wanazokabiliana nazo za ukweli wao wa Burundi. Wakati Askofu Bonaventure Nahimana, wa jimbo katoliki la Rutana, amebainisha kuwa Seminari kuu imekuwapo kama nafasi moja na katika wakati wa mafunzo ya roho ya kimisionari. Na kwa upande wa mchango wa Askofu Mkuu Simon Ntamwana, wa jimbo Kuu  Gitega, yeye alirudi kutazama kwa kina juu ya  hitaji la kutafakari juu ya vipimo vya hali ya kiroho ya ukuhani, kwa maana ya  Padre wa dunia ya leo  na juu ya njia ya kuweza kuendelea ili kukabiliana na changamoto ambazo zinazinduliwa kila mara na kelele nyingi za mtandao na hatari za kujazwa na vitu vya ulimwengu. Semina ya mafunzo ilimalizika na uundaji wa mapendekezo kwa vitengo mbalimbali vya mashirika yanayohusiana moja kwa moja na lengo la utume,na pia ahadi kadhaa za kufanya kwa washiriki wote ili kuamsha na kuimarisha roho ya kimisionari ya Kanisa la Mungu na ambalo ni Burundi.

06 January 2021, 15:22