2020.11.24 Siku ya kukabidhiana isara za Siku ya Vijana 2023 2020.11.24 Siku ya kukabidhiana isara za Siku ya Vijana 2023  

Umeanza mwaka wa kichungaji katika miaka mitatu ya maadalizi ya Siku ya Vijana 2023,Ureno

Katika Madhabahu ya Mama Maria huko Fatima nchini Ureno umenzinduliwa mpango wa kichungaji kwa ajili ya maandalizi ya Siku ya Vijana 2023.Msimamizi wa Madhabahu ya Mama Maria anasema lengo ni kuongeza nguvu katika mapendekezo ya ujumbe wa Fatima na wito wa uongofu na kuwafanya mahujaji waweze kufanya uzoefu wa kweli wa habari nema ya Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika madhabahu ya Fatima wameanza mwaka wa Kwanza wa Kichungaji katika ya mitatu ambao umejikita juu ya Bikira katika maandalizi ya Siku ya XXVIII ya Vijana duniani inayotarajiwa kuadhimishwa mwaka 2023 huko Lisbon nchini Ureno ikiongozwa na Kaulimbiu “Maria aliamka na kwenda haraka”. Matendo ya kichungaji katika Madhabahu hayo yatafuata kujibu changamoto zilizowekwa na janga la covid na mada ya mwaka wa kwanza wa kichungaji ni “Sifa kwa Bwana anayewasimamisha wadhaifu”. Shughuli hizi za kichungaji zinataka kuwakilisha ujumbe wa Fatima kama kielelezao cha wasiwasi wa Mungu kwa ajili ya binadamu anayeteseka. Haya yameeleza na Padre Carlos Cabecinhas, msimamizi wa Madhabahu

Katika kufafanua zaidi amesema Janga la Covid-19, limeweka kwa kina changamoto katika madhabahu.  Lakini hata hivyo kwa kufikiria ujumbe wa Fatima ndiyo unaweka uzoefu wa kukutana na Mungu na ulazima wa kushuhudia kikristo na kuwa na uwezekano wa kitume. Lengo ni kuongeza nguvu katika mapendekezo ya ujumbe wa Fatima na wito wa uongofu na kuwafanya mahujaji waweze kufanya uzoefu wa kweli katika  kuwakilisha ujumbe wa Fatima kama habari njema ya Mungu na kufanya kuwa madhabahu ni sehemu ya ukarimu hasa mahujai wenye hali ya udhaifu na mateso. Kwa wastani Fatima inataka kuonesha bado kama mahali pa matumaini na kutoa maana ya uzoefu wa udhaifu na mateso ya binadamu.

Padre Cabecinhas  amesema kuwa  ndiyo hiyo Kumbukumbu ambayo Sr. Lucia anabainisha katika Ujumbe wa Matumaini ya Fatima. Tarehe 13 Juni 1917, Mama Maria alimuuliza Lucia Dos Santos Je unateseka sana?  Usikate tamaa. Sitokuacha kamwe. Moyo wangu usio na doa utakuwa ndio kimbilio lako”. Mazungumzo hayo kwa mujibu wa Msimamaizi wa Madhabahu ya Maria, unataangaza mwaka wa kichungaji ili kuonesha jinsi ambavyo ujumbe wa Fatima badao unakuwa  ndiyo mwamko ambao ndani ya utashi wa kutaka kujua na kuunganisha mateso ya mwingine na  kutafuta kumjua na kumpatia uwezekano wa kujieleza.

Padre Cabecinhas aidha amefafanua zaidi kuwa ujumbe wa Fatima ni neno ambalo linatia nguvu na kutia moyo kwa sababu linatoa uwezekano wa kupata maana ya kushinda kukata tamaa. Na kipinidi cha  mafunzo na tafakari pia vitaandaliwa, kama jinsi ambavyo hakutakuwa na ukosefu wa mipango ya kitamaduni. Wamezindua Maonyesho ya nyuso za Fatima picha amazo ni muhimili wa  mandhari ya kiroho ambayo tayari ikionyesha vipande muhimu zaidi vya usanii wa kudumu wa mahali  patakatifu.  Kwa kuhitimisha amesema “Sote tunafahamu kuwa hata mwaka ujao bado unajulikana sana kuwa na  hali ya janga na kwamba tutalazimika kukabiliwa na shida nyingi, katika viwango tofauti na kwamba tunaamini kuwa ujumbe wa Fatima ni ujumbe wa matumaini na kutia moyo”.

10 December 2020, 15:28