Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake  duniani Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake duniani 

Afrika:Kuanzia ufahamu hadi hatua za dhati ni mpango wa kudhibiti nyanyaso kwa wanawake

Umezinduliwa mpango wa Baraza la Makanisa ya Afrika (Aacc),pamoja na mihimili mingine kadhaa ya kidini,tarehe 27 Novemba 2020 Siku kumi na sita za kuhamasisha bara la Afrika juu ya suala la unyanyasaji wa kijinsia na kukuza shughuli mbali mbali za ulinzi wa wanawake na watoto.Mpango huo unaongozwa na mada“Kutoka ufahamu hadi hatua za matendo ya dhati”,uliozinduliwa jijini Nairobi,Kenya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku kumi na sita za kuhamasisha bara la Afrika juu ya suala la unyanyasaji wa kijinsia na kukuza shughuli mbali mbali za ulinzi wa wanawake na watoto. Huu ndio mpango, uliozinduliwa tarehe 27 Novemba na Baraza la Makanisa Afrika yote (Aacc), pamoja na mihimili mingine kadhaa ya kidini. Mpango huo umepewa jina la “Kutoka ufahamu hadi hatua za matendo ya dhati”, umekuwa wa haraka zaidi kwa sababu, wahamasishaji wamebainisha kuwa, kutokana na kufungwa au kuwekwa karantini kwa sababu ya ugonjwa wa virusi vya corona au Covid-19 kumeongeza sana visa vya udhalilishaji wa wanawake na watoto, ambao hawawezi kutoroka dhidhi ya watekelezaji  hao wabaya kwa sababu ya vizuizi vya kuzuia kuambukiza.

Ni mpango uliowasilishwa wakati wa mkutano kwa njia ya  video uliofanyika katika Kituo cha “Desmond Tutu”, cha (Aacc) kilichoko jijini Nairobi, Kenya, ambapo mpango huo sasa utaweza kutamkwa  na kila shirika la kidini linalofuata mwongozo wake muhimu. Lengo, hata hivyo, ni moja tu, kwa mujibu wa maanadhi ya Baraza la Makanisa Afrika (Aacc), ambayo ni “kuondoa aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto wakati na baada ya janga la Covid-19”, kwa sababu ni ukiukaji wa heshima ya binadamu na sura ya Mungu ambayo kila mtu hujumuisha nayo. Siyo hivyo tu lakini pia unyanyasaji wa kijinsia ni tishio katika  uhusiano wa kijamii na jukumu lao msingi kwa ajili ya  utulivu na ustawi wa wanadamu wote” wamesisitiza.

Wakati huo huo, waanzilishi  wa mpango huo wanashutumu ukweli kwamba wazo la ukosefu wa usawa wa kijinsia sasa limeonekana kwa kiwango cha kuwa tabia ya kawaida ya binadamu, na kuunda maono yake ya ulimwengu. Kwa kuongezea, ukosefu huu wa usawa unaoendelea kudumishwa na miundo na mazingira ya mizizi ya utawala wa mfumo dume na kuchochewa na ukawaida wa ubaguzi”. Hata hivyo viongozi wa dini wanasema wana matumaini juu ya kufanikiwa kwa mpango huo kwani ulimwenguni, ​​zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu wanajitambulisha na dini, hasa katika bara la Afrika, wana nguvu ya kuleta mabadiliko ya kijamii na kitamaduni” wanasisitiza na , hasa kwa kuzingatia kulinda maadili ya kawaida ya wanadamu, kama vile heshima ya asili ya kila mmoja”.

Hatimaye Baraza la Makanisa barani Afrika (Aacc) linasisitizia umuhimu wa ushirikiano na roho ya mshikamano ambayo inahuisha mpango huo, kwa sababu kwa njia hii itawezekana kuratibu juhudi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia barani kote. Mpango huo unashirikiana na mashirika mengine kama vile  Msaada wa Kikristo, Ushirikiano  wa Mabaraza ya Kikristo na Makanisa katika Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika na Mtandao wa  Imani katika matendo.

28 November 2020, 14:44