Sudan:Wcc amesema mkataba wa amani nchini Sudan ni tumaini jipya kwa raia!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Makanisa ya Kikristo (Wcc)nchini Sudan wanatazama kwa mapya ya amani ya kudumu katika makubaliano yaliyotiwa saini mnamo Oktoba 3 huko Juba na wawakilishi wa serikali ya mpito na vikundi vikuu vya waasi wa nchi hiyo na upatanishi wa Sudan Kusini. Kwa mujibu wa Mchungaji William Deng Mian,Katibu mkuu wa Baraza la Mkanisa nchini Sudan (Nccs) ameelezea furaha yake na kwamba watu kweli wamechoka na vita na wanataka amani. Kila jitihada ambayo inasaidia kusimamzisha silaha na kuruhusu watu waishi kwa amani inakaribishwa kwa moyo mweupe, kwa mujibu wa nchungaji huyo wa Wcc.
Makubaliano hayo yanafuta mkataba wa kwanza wa pamoja uliotiwa saini mnamo tarehe 31 Agosti mwaka huu na ulisainiwa na Chama cha Mapinduzi cha Sudan(SRF), kinachojumuisha waasi kutoka Darfur, kusini mwa Kordofan na Blue Nile, mikoa mitatu ambayo waasi wa Sudan wamepambana kwa umwagaji damu dhidi ya ubaguzi uliofanywa na Khartoum wakati wa urais wa mkuu wa zamani wa nchi, Omar al-Bashir. Makubaliano hayo yanashughulikia masuala kadhaa muhimu: usalama; kugawana madaraka, fidia, kurudi kwa wakimbizi wa ndani na wakimbizi, udhibiti wa ardhi ambazo kiutamaduni zinatumiwa na jumuiya za kikabila na ujumuishaji wa wanamgambo waasi katika jeshi la kawaida la Sudan.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Sudan Kusini na Sudan Scbc) Padre Musa Timothy ameonesha furaha yake ya kufikia hitimsho hili lilioanza mwaka mmoja uliopita “ Makubaliano ya amani yanapokelewa na kupongezwa na watu wote wa Sudan kwa ujumla lakini pia hasa kwa watu wa Darfur, kwa sababu ni kuhitmishwa kwa vita na mateso yaliyoanza tangu mwaka 2003 amesisitiza Padre huyo.