Kuna haja ya kusafisha na kutunza mazingira kila sehemu Kuna haja ya kusafisha na kutunza mazingira kila sehemu 

Ufilippini#Kipindi cha kazi ya uumbaji:wakristo na waislam wajitolea kusafisha pwani.

Ofisi ya Kitume ya Puerto Princesa nchini Uffilippino kwa kujibu mwaliko wa Papa Francisko wa kuishi pamoja kipindi cha kazi ya uumbaji ambacho kimeanza tarehe Mosi Septemba katika Siku ya kuombea Kazi ya Uumbaji,wameandaa shughuli ya pamoja ya wakristo na waislam kusafisha pwani ya Barangay Bancao-Bancao .

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kikundi cha Wakristo na waislam wa kujitolea wamekutana pamoja tarehe 3 Septemba 2020 wakiwa na zana kwa ajili ya kusafisha pwani yao nchini Ufillipini. Kwa mujibu wa taarifa zilizo tolewa kwenye Tovuti ya Baraza linasema shughuli hii ilifanyika katika eneo la Barangay Bancao-Bancao kwa kuandaliwa na Ofisi ya Kitume ya Puerto Princesa kwa kujibu mwaliko wa Papa Francisko wa kuishi pamoja kipindi cha kazi ya uumbaji ambayo imeanza tarehe Mosi Septemba katika Siku ya kuombea Kazi ya Uumbaji.

Msimamizi wa  kitume Askofu Socrates Mesiona, katika siku hiyo ameitumia kwa kuwaasa waachane na tabia za utamaduni wa kutumia na kutupa katika jamii ya kisasa na kusema “Tunazo dini tofauti, tunazo imani tofauti, lakini tunishi katika dunia hiyo hiyo” , kwa maana hiyo ni matumaini yake ya kwamba  watu wanaweza kuonesha wote ‘tasaufi’ yaani roho za ulinzi wa mazingira. Katika muktadha huo huo hata kiongozi wa kiislam mahalia,  Hadji Arturo 'Abdulaziz' Suiz wametoa umuhimu wa sababu za kulinda mazingira kwamba “Tulinde mazingira kwa ajili ya kizazi kijacho”.

Kipindi cha kazi ya uumbaji ambacho ni kwa matashi makubwa ya Papa Francisko kitahitimishwa tarehe 4 Oktoba 2020 sambamba na siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi mtawa mdogo na mtetezi mkuu wa mazingira, mfano wa kuigwa na usiyosahaulika. Kwa upande wa Kanisa la Uffilippini watakirefusha hadi hadi tarehe 11 Oktoba inayoangukia siku ya  Dominika ya Siku ya Watu asilia. Kati ya mambo yaliyoanzishwa wanatarajia tarehe 30 Septemba 2020 kuanzia upandaji wa miti juu ya mlima wa Irawan kwa jili ya manufaa ya Jumuiya ya kidini ya Palawan.  Kunako mwaka 2019 Usimamizi wa Kitume wa Puerto Princesa uliweza kupanda hata miti mipya 10,000 katika eneo la ulinzi wa Mlima wa Mantalingahan huko Brooke nchini Ufilippino.

05 September 2020, 13:08