Tangu nchi ya Sudan Kusini kupata uhuru 2011 hadi leo haijawa na msimamo wa amani. Tangu nchi ya Sudan Kusini kupata uhuru 2011 hadi leo haijawa na msimamo wa amani. 

Sudan Kusini:Ni muhimu kujenga Taifa kwa upya lenye amani!

Damu ya mashihidi wetu ni mbegu ya amani,ndiyo ujumbe uliotolewa na Askofu Mstaafu Paride Taban wa Torit,katika fursa ya Siku ya Kitaifa kwa ajili ya mashahidi nchini Sudan Kusini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kujenga kwa upya nchi, yenye tabia ya amani na maendeleo, ndiyo wito kutoka kwa Askofu Mstaafu Paride Taban wa Torit nchini Sudan Kusini katika fursa ya Kitaifa kwa ajili ya mashahidi iliyoadhimishwa tarehe 30 Julai 2020. Katika fursa hiyo Askofu Mstaafu Paride Taban, ametangaza ujumbe wake alioupatia jina “damu ya mashihidi wetu ni mbegu ya amani”.

Tutazame mambo muhimu ya Kristo

“Tushinde tofauti na kuhamaisha maelewano ya amani ili kuifanya nchi yetu kama Ufalme wa Mungu hapa duniani” ameandika Askofu Taban na kuwaalika waamini kuiga mfano wa Mtakatifu Paulo ambaye alikazia umakini kwa kile kilicho muhimu hasa Kristo na kuacha mambo mengine yasiyo ya muhimu.

Viongozi wa nchi wapambanie ustawi wa wote

Kwa mujibu wa Askofu  Taban, aliyetajwa katika Tovuti ya Amecea, anasema hii kwa namna ya pekee ndiyo mafundisho ambayo yanapaswa kufuatiliwa na viongozi wa nchi kupambania hasa ustawi wa wote. Nchi ambayo ni kijana sana iko mbioni katika kutafuta msimamo. Nchini Sudan Kusini ilipata uhuru wake kunako tarehe 9 Julai 2011, na  baada ya miaka 9 hadi sasa haijawa na msimamo wowote. Inatosha kutaja hata ripoti ya Caritas ya Italia iliyopewa jina “amani inayoyumba”.

Ni watu ambao wamekumbwa na vita vya kutisha vya wao kwa wao katika bara lenye njaa ya majanga. Katika hati ya Caritas, inakumbusha kuwa “ vita vya wao kwa wao vimesababisha mamia elfu ya vivo : watu wengi kukimbia na mamilioni kulundikana kwa ndani, na waliokimbilia nje wanasababisha udhaifu mkubwa katika nchi walimokimbilia; maeeneo kukosa majengo muhimu: mchakato wa amani ulitiwa sahini ya makubaliano na kusitisha vita bado hayazingatiwi na wala kuheshimiwa: mara nyingi yameahirishwa na daima migongano ya hapa na pale na matokeo yake ni njaa na umaskini.

Kanisa mahalia katika harakati za kuwa karibu na watu wa Mungu

Kwa bahati Kanisa mahalia kama Papa Francisko , havijakosa kamwe kusikia sauti na ukaribu wake kwa watu hao huku wakitoa msaada uwe nyenzo za kiroho na kimwili na zaidi katika kipindi hiki kigumu cha virusi vya corona. Kwa maana hiyo wanatoa wito wa kuomba msamaha,na mazungumzo ili kushinda kinzani za migawanyiko ya kikabiliana na maslahi ya wachache kwa jina la umoja wa kitaifa.

01 August 2020, 12:27