Vatican News
Lazima kutunza sayari tetu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Lazima kutunza sayari tetu tuliyopewa na Mwenyezi Mungu 

Viongozi wa Makanisa ya Ulaya wanatoa wito wa kuishi kipindi cha uumbaji kwa roho ya kiekumene!

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi wa Makanisa Ulaya na Baraza la Maaskofu Ulaya wanawaalika waamini wote na wenye mpenzi kubadilisha kipindi kilicho chaguliwa na Papa Francisko ili kurudisha pamoja kati ya uhusiano na kazi ya uumbaji kwa ajili ya kuwa na furaha ya nchi na kuishi kwa muungano na sala.Kipinidi hiki kinaanza tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba katika siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Inakaribia maadhimisho ya kila mwaka katika kujikita kwa hakika katika matendo ya kutunza  Nyumba yetu ya pamoja ambapo ni mwaliko  wakuweza wa kuishi “kipindi cha uumbaji ambacho kinaadhimishwa ulimwenguni tangu tarehe Mosi Septemba ijayo kama “Siku ya Kuombea kazi ya uumbaji” na ambacho kitaendelea kwa mwezi mzima hadi tarehe 4 Oktoba sambamba na siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Mwaliko wa Papa Francisko kwa wakristo katika kipindi hicho maalum ni kuwa na tabia ya kusali, kutafakari na kujikita katika matendo ya kweli  ili kuweza kukarabati  mahusiano na mwingine na Muumba wa mbingu na dunia.

Lazima kijenga wakati ulio bora wa sayari yetu

Kufuatia na tukio hilo, hata mwaka huu kama ilivyo miaka mingine iliyopita, Baraza la makanisa ya Ulaya na Baraza la Maaskofu katoliki Ulaya, wanatumia fursa hii kuwatia moyo wajumbe wote wa Makanisa barani Ulaya kutambua kiukweli siku hizo kama fursa nyeti ya kusheherekea utajiri wa imani yetu. Kwa kuangazwa na  mawazo la Papa Francisko kutoka Waraka  wa “Laudato Si”, yaani sifa iwe kwako , maraisi wa mabaraza haya wanakumbusha juu ya wasiwasi wa kuunganisha familia ya kibinadamu katika kutafuta maendeleo endelevu na kupyaishwa kwa  wito wa majadiliano na kukabiliana kati ya watu wote kwa  namna ya kujenga sayari ya wakati ujao lakini kuanzia hata sasa.

Adui wa kitaalimungu ni mpinga mazoezi ya kuwa na uhusiano na maumbile

Mantiki kama hiyo  wanaandika viongozi hawa  kuwa mmoja wa wataalimungu wa kisasa kama vile  Juergen Moltmann, alithibitisha kuwa “leo hii adui wa kitaalimungu ni mpinga mazoezi katika mahusiano yetu na maumbile” na kwamba alitoa ushauri wa kufanya mazungumzo  juu ya Mungu ambaye yupo katika kazi zote za  uumbaji kwa njia ya Roho Mtakatifu wake  na pia kufanya mang’amuzi ambayo yanaweza kupelekea wanaume na wanawake kufanya maridhiano na amani ya maumbile ya asili. Katika taarifa yao vile vile inaweka bayana na kuelezea kwa namna hiyo jinsi ya ukuu wa kieumeni inaleta pamoja maana katika kuadhimisha “Siku ya Kuombea kazi ya uumbaji na katika Kipindi  chote cha uumbaji na ni ishara ya kushukuru hata pendekezo la marehemu Patriaki wa kiekumene Dimitrios I kunako mwaka  19892 na Mikuntano tofauti ya kiekumene ya Ulaya  iliyoandaliwa kwa pamoja na Baraza la Makanisa na la Maaskofu wa Ulaya kuanzia Basilea (1989) kupitia  Graz (1997) hadi  Sibiu (2007).

Mantiki ya Yubilei ni mzizi wa kibiblia

Mwaka huu kutokana na janga ambalo limelata madhara makubwa ya kibinadamu na kuonekana katika mwanga, udhaifu wa mwanadamu  tukio linalazimisha kuchukua tahadhali sana kwa hali  halisi ya maisha endelevu katika sayari hii. Kwa njia hiyo mwaka huu bado unakuwa ni fursa ya kufikiria uharibifu mkubwa wa mazingira na hatari itokanayo na mabadiliko ya tabianchi. Kwa njia hiyo ni mwaliko kutoka kwa maraisiwa mihimili hii ya kidini Ulaya kuadhimisha mwaka huu Kipindi   cha kazi ya Uumbaji chini ya kauli mbiu ya Yubilei ya ardhi. Mantiki ya Yubilei ina mzizi wake Kibiblia na kusisitiza kuwa lazima pawepo usawa wa haki na endelevu kati ya hali halisi kijamii, kiuchumi na kiikolojia. Aidha somo la Yubilei kibiblia inaelekeza ulazima wa kuweka usawa wa mifumo ya maisha; inathibitisha ulazima wa kuwa na haki na uendelevu;  inatibitisha ulazima wa kuwa na sauti ya kinabii katika kulinda nyumba ya binadamu. Viongozi hawa wanawaalika Wachungaji wote na wakristo wote wa Ulaya, Maparokia, jumuyia za kikanisa na kila mtu mwenye mapenzi mema kuwa makini katika “Kipindi cha uumbaji na kuishi kwa roho ya kiekumene, kuungana katika sala na katika matendo ya dhati!

26 August 2020, 14:10