Hakuna adhabu ya hukumu ya kifo haisadii bali wenye hatia kushukuliwa hatua za kisheria zilizo kali. Hakuna adhabu ya hukumu ya kifo haisadii bali wenye hatia kushukuliwa hatua za kisheria zilizo kali. 

Liberia-Kanisa Katoliki:Hakuna adhabu ya kifo bali kuongeza nguvu kulinda waathiriwa!

Hakuna kutoa adhabu ya kifo kwa wale wanaofanya ubakaji,bali lazima kuimarisha sheria zilizopo na kuwalinda waathiriwa.Amesema hayo Paroko wa Mtakatifu Kizito nchini Liberia wakati nchini huom kuna mjadala mkubwa wa kitaasisi juu ya uwezekano wa kuanzisha hukumu ya adhabu ya kifo kwa wenye hatia ya ubakaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumapili tarehe 16 Agosti 2020 wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu, kwenye Parokia ya Mtakatifu Kizito huko Paynesville, nchini  Liberia, Padre Ambrose Kromah amesema adhabu ya kifo siyo suluhisho la dhuluma badala yake kwani anasema : “Watakuwa wakilinganisha na juhudi zinazofanywa za kuvunja 'utamaduni wa kimya' unaozungukia ubakaji”. Amethibitisha hayo wakati katika nchi hiyo kuna mjadala mkubwa wa kitaasisi juu ya uwezekano wa kuanzisha hukumu ya kifo kwa wale wenye hatia ya ubakaji. Kwa mujibu wa Paroko ya Mtakatifu Kizito, Padre Ambrose Kromah  amewaalika kuzingatia hasa sababu za vurugu kama hizi  na kwamba “kwa namna yoyote ile na dhidi ya mtu yeyote aliyetenda, ni vitendo vibaya sana ambavyo lazima kila wakati lazima vilipotiwe kwa masharti madhubuti, wakati wale waliowajibika na hilo lazima wafikishwe mbele ya sheria, bila kujali asili yao, hali yao au msimamo wao wa kijamii”.  

Tafakari ya kina na msaada wa kiadili kwa ajili ya uponyaji wa waathiriwa

Ni kwa njia ya tafakari ya kina juu ya suala hili  tu  inaweze kubadili hali halisi ya sasa, amesisitiza Padre Kromah, lakini pia ameongeza kusema kuwa “ni kelelezo cha tafakari ya kujumuisha msaada wa kiadili unaohitajika katika  uponyaji wa waathiriwa pia kulipwa fidia kwa uharibifu uliosababishwa”. Kufuatia na hiyo ndipo Paroko ametoa mwaliko kwa wazalendo wa Liberia ili kuharakisha michakato ya kisheria juu ya kesi za ubakaji na kuongeza nguvu za vyombo husika vilivyokabidhiwa ili kutoa haki kwa waathiriwa. Kwa kuhitimisha amesema: “Kuamua kuadhibiti kwa njia ya adhabu ya kifo dhidi ya wimbi hili la ubaya,  sio suluhisho  kwa sababu itakuwa sawa na kuainisha ubaya zaidi na utamaduni wa kifo”, ”.

Mwaka wa mwisho nchini Liberia vitendo vya ubakaji vimeongezeka

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, visa vya ukatili wa kingono na kijinsia nchini Liberia vimeongezeka sana hasa  katika mwaka wa mwisho huu kutokana na janga la virusi vya corona  ambalo limeweka watu wengi katika mazingira magumu, hasa wale ambao tayari wamekwisha athirika. Katika takwimu kutoka Wizara ya Sheria zinaonyesha kuwa kati ya Januari na Juni 2020, zaidi ya kesi 600 za kushambuliwa vibaya kwa sababu ya ubakaji zimerekodiwa. Kesi 107 kati yao wamefikishwa mahakamani na watu  44 wamehukumiwa  na watu 42 wamepata dhamana. Hata kama nchi hiyo iko kati ya nchi 177 kati ya 188 kwenye orodha ya kila mwaka ya ukosefu wa usawa wa kijinsia, lakini inaonesha  kuongezeka kwa kasi na  kiwango hicho kunachotarajiwa kutokana na  matokeo ya dharura ya kiafya. Hata hivyo pia  taarifa inasema kuwa  katika wiki mbili zilizopita, ubakaji kadhaa wa watoto na wasichana umeripotiwa. Katika muktadha huo, maombi ya adhabu kali zaidi kwa wenye hatia yameongezeka, pamoja na hukumu ya kifo, iliyoandaliwa kati ya mengine na Makamu wa Rais, Bwana Jewel Howard Taylor, na Mkuu wa nchi huyo Bwana  Prince C. Johnson.

21 August 2020, 13:49