Vatican News
Mwaliko wa kweli wa kuendelea na  mshikamano na kushirikisha furaha ya Injili ndiyo uliotolewa na Maaskofu wa Ubelgiji katika mtazamo wa baada ya janga la virusi vya corona Mwaliko wa kweli wa kuendelea na mshikamano na kushirikisha furaha ya Injili ndiyo uliotolewa na Maaskofu wa Ubelgiji katika mtazamo wa baada ya janga la virusi vya corona  (©paul - stock.adobe.com)

Ubelgiji#Coronavirus:tumaini linatakiwa katika ulimwengu baada ya janga!

Maaskofu nchini Ubelgiji wanawaalika watu wa Mungu kujikita zaidi katika mshikamano na kushirikishana furaha ya Injili.Tutoe matumaini ili kushinda changamoto zinazokabiliwa na ulimwengu baada ya janga.Katika chagamoto hizi,hakuna majibu yaliyo tayari lakini,inawezakana kabisa kuchota kutoka katika rasilimali ya imani yetu na kushirikishana katika jamii ili kuweza kung’amua na kutenda kwa ajili ya wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika barua ya kichungaji iliyoandikwa na maaskofu wa Ubelgiji wanatoa mwito wa kuendelea kutoa mshikamano na kushirikishana furaha ya Injili. Ni lazima kutoa matumaini ili kushinda changamoto zinazokabiliwa na ulimwengu baada ya janga la virusi. Katika barua yao  ya kichungaji inaongozwa na kauli mbiu “Tumaini la kutolewa” katika changamoto baada ya janga la virusi vya corona. Ni mwaliko wa kweli wa kuendelea na  mshikamano na kushirikisha furaha ya Injili. Hati hiyo, inaambatana na video, ambapo inaangazia takwimu za miezi hii migumu ya ugonjwa ambao umeleta shida kubwa kwa watu wengi, familia na jamii zilizoathiriwa na huzuni, magonjwa, upotezaji wa kazi na kutengwa. Kwa upande wao, wazo lao la kwanza linaendelea  na kukumbusha hata mateso ya wakristo waliozuiwa kwa miezi hii kutoweza kupokea Sakramenti na kukutana kwao katika jumuiya za kikanisa. “Kuwa mbali na ndugu na dada zetu imekuwa gharama kwetu sisi” wanasema, huku wakiwashukuru waamini kwa kuheshimu vizuizi vizito vilivyowekwa dhidi ya maambukizi.

Maaskofu wanasema lakini miezi hii haijaonyesha mateso na shida tu, kutengwa huko  "kulituruhusu sisi sote kuona ishara nyingi za mshikamano” wanabainisha maaskofu wa Ubelgiji. “Watu wengi wamejitolea wakati wao na talanta zao kwa wengine. Majirani au hata wageni kamili wasiojulikana wamekuwa wa karibu na wa msaada. Na hii ni ambao ulionyesha kuwa katika nyakati hizi za giza Mungu alikuwapo na kwamba, Pasaka yake ni nguvu kuliko giza. Aidha maaskofu wa Ubelgiji wameongeza kusema, "karantini pia iliruhusu Kanisa kuonyesha ubunifu mpya wa kichungaji na gundua tena viwango vya imani ambavyo ukawaida huweka hatari ya kutufanya tusahau, kama vile kusikiliza Neno, sala ya binafsi au ya familia, tafakari na mazungumzo".

Maaskofu wa Ubelgiji wanawatia moyo watu wa Mungu kuendelea kwenye njia hiyo kwa pamoja, ili kuifanya jamii zao ziwe  nzuri zaidi kwa sababu iwe ya kidugu, nyeti zaidi na yenye kujali majeraha ya kila mtu na kiu ya ulimwengu huu na zaidi watoa ushauri wao baada ya covid -19, kuhifadhi na kushehereke maadhimisho vema  ili viwe vyanzo vya mambo ya undani na jitihada za maisha yao.  Janga la virusi kwa hakika limewezesha kutambua changamoto kuu za wakati wetu ambazo ni za kijamii, mazingira na kiuchumi. Katika chagamoto hizi, hakuna majibu yaliyo tayari  lakini, inawezakana kabisa kuchota kutoka katika rasilimali ya  imani yetu na kushirikishana katika jamii ili kuweza kung’amua na kutenda pamoja na watu wengine na vikundi katika  jamii zetu.

Kanisa la Ubelgiji linatoa ujumbe kwa namna ya pekee kwa  kwa jamuiya za Wakristo wakiwasihi hasa kujitoa, kwa shauku ile ile, kwa moyo wa Mungu na moyo wa ulimwengu, kama jinsi ubatizo wetu unavyotutaka: Mbele ya janga hili, ulimwengu huu, wenye uwezo wa ukarimu mkubwa, uko pia kwenye mtego wa mashaka. Basi tujitahidi kutoa mshikamano wetu, tumaini na furaha ya Injili”, inashauri  barua  na kuhitimisha kwa matumaini kwamba majira ya joto yaweza kuwa wakati muafaka wa kuunganisha na umuhimu na wakati huo huo, fursa kwa ajili  ya kutafuta kikamilifu kile ambacho Mungu anataka kwa kila mmoja wetu, kwa Kanisa lake na kwa ulimwengu wetu”.

01 July 2020, 13:23