Maaskofu wa Kenya watoa Wito kwa Serikali ili kuchukua hatua za ulinzi wa madreva wa malori ambao wanayo nafasi kubwa ya uchumi wa nchi hiyo pia na watu wengine katika mazingira magumu. Maaskofu wa Kenya watoa Wito kwa Serikali ili kuchukua hatua za ulinzi wa madreva wa malori ambao wanayo nafasi kubwa ya uchumi wa nchi hiyo pia na watu wengine katika mazingira magumu. 

Kenya#coronavirus:Ulinzi wa watu katika mazingira magumu unahitajika zaidi!

Wito kutoka kwa Rais wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Wakimbizi,Wahamiaji na Mabaharia nchini Kenya anasema lazima kulinda watu walio hatarini.Hawa ni watu wanaoishi barabarani na wagonjwa wa akili.Wito pia kwa Serikali ili kuchukua hatua za ulinzi wa madreva wa malori ambao wanayo nafasi kubwa ya uchumi wa nchi hiyo.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Askofu Virgilio Pante, wa Jimbo Katoliki la Maralal na Rais wa Tume kwa ajili ya wahamiaji, wakimbizi na mabaharia wa Baraza la Maaskofu nchini Kenya, wakati wa maadhimisho ya Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu, Jumapili tarehe 14 Juni 2020, amesema kuwa “Watu wanaoishi barabarani na wale wanaosumbuliwa na ugonjwa wa akili wanajikuta katika hali mbaya na hatari ni kubwa kuambukizwa na virusi vya corona au COVID-19”.  

Askofu Pante ameonesha wasiwasi mkubwa wa Maaskofu wa Kenya kuhusu madhara ya COVID-19 na kuomba hatua za kuzuia maambukizi zaidi ambayo yanajionesha kwa watu walio katika mazingira magumu katika jamii, kwa mfano wakimbizi, waliorundikana ndani, wafanyakazi ambao wanalazimika kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama madreva wa malori, wachungaji, watu wasio na makazi na wale ambao ni wagonjwa wa akili.

Askofu wa Maralal amekumbuka kwa namna ya pekee hali halisi ya madreva wa malori ambao wanayo nafasi msingi katika uchumi wa kitaifa. “Madreva wa malori wanatoa mchango mkubwa katika  ustawi wa uchumi kwa nchi yetu. Kuongezeka kwa idadi ya madreva wa malori walioambukizwa na virusi vya corona au COVID-19 ni ishara ya pengo kubwa katika utunzaji wa usalama na afya zao katika changamoto ambazo madereva wa malori wanakumbana nazo". Aidha Askofu amesema zaidi ni suala la kutia wasiwasi mkubwa kwa wote. Tunatoa wito kwa serikali ili likabiliane kwa haraka changamoto hizo za madreva wanazokumbana nazo ili kupunguza kuenea kwa virusi".

Rais wa Tume ya Wakimbizi, Wahamiaji na mabaharia amepongeza  juhudi za wafadhili wanaowaunga mkono familia za barabarani ambao sehemu kubwa ndiyo walio athirika sana na COVID-19, na kusisitiza kwamba juhudi zinahitaji kuongezeka ili kukabiliana na shida ya watu waliorundikana wa ndani na wakimbizi wanaoishi katika maeneo yenye msongamano bila vifaa vya kutosha kukabiliana na wimbi la maambukizi.

“Wakimbizi na mlundikano wa ndani wanaoishi katika kambi zilizo na watu wengi wana hatari ya kupata ugonjwa wa virusi vya corona. Tunatoa wito ili hatua za kutosha zichukuliwe kwa haraka katika kulinda vikundi hivi vilivyo katika mazingira magumu”. Hatimaye Askofu  Pante amekumbuka “hali ya jamuiya  za hamahama ambazo zinajikuta katika uchungaji na katika kesi zilizoripotiwa za COVID-19 ni za chini,japokuwa ameongeza kusema- lazima zifundishwe juu ya hatari za ugonjwa wa virusi vya corona na hatua za kuzuia zichukuliwe”.

16 June 2020, 12:02