2020.04.18 Matumizi ya vyombo vya habari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa, Livingstone, Zambia 2020.04.18 Matumizi ya vyombo vya habari katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa, Livingstone, Zambia 

Zambia#coronavirus:Kanisa bila mpaka:waamini wanapata neno kupitia mitandao!

Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa la Jimbo Kuu la Livingston nchini Zambia anaelezea ni kwa namna gani katika janga la virusi vya corona wanaendelea kukabiliana nalo hasa kuwezesha waamini watu wa Mungu kushiriki kiroho maadhimisho ya liturujia za kipindi hiki cha Pasaka kwa njia ya zana walizonazo za mitandao yote ya kijamii.Pd.Mulasikwanda,anathibitisha kukutwa bila maandalizi ya teknolojia ya mitandao.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika parokia moja ya Livingstone nchini Zambia, kufuatana na dharura ya kiafya imeweza mara moja kuchukua hatua za kweli ili kukabiliana na hali halisi hasa kwa ajili ya kuwasaidia wanaparokia wake waweze kushiriki kiroho maadhimisho ya misa za moja kwa moja, sala  na misa nyingine kupitia ukurasa wa facebook. Kwa kufanya hivyo pia kwa ubunifu pamoja na zana dhaifu walizo nazo wameweza kuzidisha matangazo hayo katika majakwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii ambayo yamewezesha watu kushiriki maadhimisho yote ya liturujia za Pasaka na nyingine. Ni kwa mujibu wa Maelezo ya Padre Clifford Mulasikwanda, ambaye ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa huko Livingstone, nchini  Zambia, katika harakati za kukabiliana na janga hili la “Covid-19”.

Akifafanua anasema: “Kwa sasa Makanisa yote nchini Zambia yamefungwa na serikali inaendelea kutoa ushauri kwa watu wabaki ndani”, kwa mujibu wa Padre Mulasikwanda, anabainisha kuwa  katika parokia yao matumizi ya mitandao ya kijamii kwa upande wa waamini imepokelewa vema na imekuwa kama "manna" mkate" kutoka mbinguni. Aidha amesema  kwa hakika janga hili limeleta athari hasi, kwani virusi vya corona ni ugonjwa wa hatari ambao ni lazima kutoa mzizi wake. Pamoja na mgogoro huo, umepelekea kuingilia kwa haraka nyanja mpya za kisasa ambazo hakuna aliyekuwa anafikiria au kutarajia kkwa wiki chache zilizopita.

Kwa upande mwingine amethibitisha, mahitaji ndiyo mama wa ubunifu. Hii kiukweli Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresa, lilikuwa halikujiandaa katika kukabiliana na njia ya matangazo ya mubashara na matumizi ya wakati  huu kupitia  mitandao ya kijamii. Hii ilikuwa inatokana pia na ukosefu wa zana muhimu. Kwa sasa wanatumia simu yake ya smart phone, kipaza sauti kidogo na kifaa kingine walicho kiazima kutoka parokia nyingine. Lakini hadi sasa vimewasaidia, pamoja na kazi ngumu na kwamba ikiwa fedha itaruhusu watapendelea kununua kamera ya video na maikrofoni inayofaa zaidi kwa utangazaji wa moja kwa moja. Kwa sababu ya vikwazo vya bajeti, kwa wakati huu, parokia hiyo imepakua programu ya bure inayopatikana kwenye mtandao na ambayo inaruhusu ujumuishwaji wa video na sauti, kwa sababu mara nyingi ile inayotolewa na majukwaa kama vile Facebook na whatsap haifanyi kazi vizuri kwa sababu inasababisha utendaji wa kazi usiwe mzuri.

Vile vile akifafanua anasema duniani leo hii,  watu wanahitaji kuona kile ambacho wanasikia. Kwa sababu hii, wanajaribu polepole kuboresha yaliyomo na teknolojia ambayo wanawapatia. Siyo tu hilo bali kwa utambuzi ya kwamba utangazaji wa moja kwa moja wa matukio ya kiroho unagharimu kwa maana hiyo waamini wema wameweza kutoa hata michango yao midogo ya kununua GB nyingine na kwamba  kuna watu wema katika parokia yao.

Akifafanua juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa waamini, amebainisha ni kwa jinsi gani watu wa parokia yao wanasifu na kutumia sana facebook na WhatsApp. Ndiyo njia mbili ambazo ni rahisi kufikiwa kwa kila aina ya watu kijamii kama vile wanawaume na wanawake, vijana wa kila rika na wazee na kwa wote wanaonesha kupenda, kutokana na kuanzisha suala  kupitia katika majukwaa yao ya kijamii ambayo tayari wanatumia na ili kuwasaidia kupata habari halisi zinazo endelea kwa mujibu wa Padre Mulasikwanda.

Hata hivyo kuhusu maoni ya makuhani wengine na wahudumu wa Kanisa kuu mbele ya changamoto ya kutumia vyombo vya habari vya kijamii ili kuinjilisha, Paroko amesema maoni ya waamini wao yamewafanya watambue kwamba wameunda Kanisa lisilo  na mipaka na bila vizingiti.  “Watu wa Mungu wana njaa ya Neno la Mungu katika nyakati hizi ngumu. Kila mhudumu wa dini anayetumia vema mitandao ya kijamii ana watazamaji wengi". Kwa kuhitimisha Padre Mulasikwanda anabainisha:"Hata kupitia vyombo vya habari vya kijamii, wanaparokia wanainjilishwa, wanahubiriwa na kutakaswa kwa sababu hakuna mtu anayejua Roho inavuma kutoka wapi na kwenda wapi”.

20 April 2020, 12:59