Vatican News
Kwa mujibu wa Caritas nchini Venezuela ni kwamba mshikamano umeongezeka zaidi katika kipindi hiki cha janga la virus vya corona Kwa mujibu wa Caritas nchini Venezuela ni kwamba mshikamano umeongezeka zaidi katika kipindi hiki cha janga la virus vya corona 

Venezuela #coronavirus.Caritas:janga limeongeza mshikamano zaidi!

Caritas nchini Venezuela linabainisha juu ya kuongezeka kwa mshikamano zaidi katika kipindi hiki kigumu cha virusi vya corona.Mara baada ya watu kulazimika kukaa karantini,wamejigawa mara moja kuwafikia msaada watu wenye kuhitaji zaidi walioko mbali na wazee.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika nyakati za kukosa mahitaji kama vile yaletwayo na janga la virusi vya corona, mshikamano umeongezeka mara dufu na kuwezesha nguvu kubwa ya huduma ya upendo kutendeka. Amethibitisha hayo Bi Janeth Márquez, Mkurugenzi wa Caritas nchini Venezuela, akifafanua kwa kinaga ubaga juu ya matendo ya dhati yaliyochukuliwa mara moja katika hatua  za haraka kwenye sekta ya Kichungaji kijamii ya Baraza la Maaskofu nchini Venezuela(Cev), mbele ya tishio la Codvid-19.

Awali ya yote Kanisa limeweza kugundua njia mpya Mkurugenzi huyo abainisha na  kwa sababu matatizo zaidi yanayo sikika zaidi hasa kwa watu yanayotazama chakula, kutokana na  ulazima wa kubaki karantini, na wakati huo mahitaji muhimu ya lazima hayapo. Pamoja na hayo Caritsanchini Venezuela wamejikita kwa haraka kuanza kutembelea wenye kuhitaji kuanza nyumba kwa nyumba hasa katika maeneo yaliyo mbali na mahali walipo wazee. Na wakati huo huo wanaendelea kuwapa lishe watoto wenye utapiamlo na  kuwakabidhi katika nyumba zao hata madawa ya lazima. Hata hivyo matatizo hayakosekani anasema mkurugenzi hiyo kwa mfano ukosefu wa mafuta ya gari kwa ajili ya kuzungukia watu kama hao.

Kwa bahati nzuri amethibitisha mshikamano haukosekani kwa maana watu wengi wameweza kuwapelekea chakula, ameibinisha katika Tovuti ya Baraza la Maaskofu nchini Venezuela. Aidha amesema, katika kipindi hiki cha janga, wanazidi kuona ongezeko la zawadi nyingi na ubunifu na ambazo zimewawezesha wao kuweza kuwasaidia watu  ambao wanahitaji zaidi ikiwa pamoja na kuwapatia  taarifa zilizo wazi na rasmi kuhusu dharura ya kiafya.

Kwa hakika huduma zote zinaendelea na dharura mpya ambayo inatazamia kukutana moja kwa moja na watu anasema Mkurugenzi,  japokuwa kwa kuzuia maambukizi, kwa mfano katika vituo vya utoaji wa chakula, waandaaji kwa sasa wanaandaa chakula na kuweka kwenye mifuko  ili kuwapelekea moja kwa moja katika nyumba zao… Vile vile amebainisha kuwa ,Vituo vya msaada wa ushauri vinaendeshwa kwa njia ya kupiga simu moja kwa moja na wakati ofisi za Caritas zinafunguliwa kwa kupeana ratiba ya kufika watu ili wasiweze kuwa zaidi ya watu kumi mara moja katika viuo hivyo.

Hatimaye Bi  Janeth Márquez anasisitizia juu ya msaada mkubwa ambao umeweza kujionesha katika mitandao ya kijamii. Na hii amesisitiza ni katika kutoa semina mbalimbali mubashara ili kuwajuza watu juu ya kanuni za kuzingatia watu za usafi wa kujikinga na virusi hata kuwahamasisha kuwa na mshikamano kati ya familia ili wasiache yoyote nyuma.

20 April 2020, 12:00