Sudan Kusini baada ya kutangaza kesi za kwanza za virusi vya corona askofu Hiiboro anasema makanisa yanabakia wazi katika mioyo na matendo lakini ni wakati sasa wa kusitisha vita duniani kote Sudan Kusini baada ya kutangaza kesi za kwanza za virusi vya corona askofu Hiiboro anasema makanisa yanabakia wazi katika mioyo na matendo lakini ni wakati sasa wa kusitisha vita duniani kote 

Sudan Kusini#coronavirus:makanisa yanabakia wazi mioyoni!

Kwa mujibu wa Askofu Eduardo Hiiboro wa jimbo la Tombura Yambio nchini Sudan Kusini amesema makanisa yanabakia wazi katika mioyo,matendo na katika utakatifu wa kuishi kila siku.Anaomba Bwana aweze kusaidia katika janga hili maana anasema hakuna uwezo na wala nguvu maana watu ni wadhaifu pia hawana nyumba.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hatuna uwezo wa kukabiliana na vita vingine, hatuna nguvu, watu wamekuwa wadhaifu pia  hawana nyumba. Ninaomba kwa Mungu atafute suluhisho la haraka ili kukomesha virusi ulimwenguni kote, alete amani katika Nchi yetu na katika maeneo yote yenye mzozo wa kivita, ili tuweze kutambea wote pamoja kuelekea katika ulimwengu wa amani. Leo hii pamoja na mateso ya umbali, makanisa yanabaki wazi katika mioyo yetu, katika matendo na katika utakatifu wa kuishi kila siku. Miimili ya majengo halisi imefungwa lakini mioyo imefunguliwa na maisha yetu ya kiroho yanaendelea.

Ndivyo ujumbe ulivyo wafikia katika shirika la habari za kimisionari kutoka kwa Askofu Eduardo Hiiboro wa jimbo katoliki Tambura-Yambio nchini Sudan Kusini ambaye katika kipindi hiki kigumu anataka kutoa wito wake ili kusitisha vita katika mataifa duniani na ujumbe ambao umekuwa kila mara ukienezwa kila kona ya dunia kutoka kwa Papa Francisko kwa matumaini ya kupokelewa hata katika nchi ya Suda Kusini. Askofu Hiiboro amesema, “jitihada za kichungaji ambazo Papa Fracisko anapeleka mbele kwa ajili ya ubinadamu wote, bado unaendelea kutoa chachu ya kina.

Kwa mujibu wa Askofu Hiiboro anasema Papa yupo kila wakati katika mateso ambayo yanamkumba binadamu wote. Aidha ameongeza kusema “Ninauzoefu huo binafsi na watu wote wa Sudan Kusini”. Askofu Hiiboro amemfananisha Papa Francisko kama msamaria wa kweli ambaye daima yuko karibu wenye kuhitaji. Anahatarisha hata maisha yake, hajibakizi nguvu zake na jitihada zake ili kuweza kuhisi uwezo wake katika kila jumuiya.

Papa Francisko daima amekuwa mstari wa mbele katika shughuli za kichungji na kwa na umakini wa Dunia; daima akiwa mstari wa mbele wa kuwa karibu na mateso ya ubinadamu. Kwa mujbu wa  Askofu Hiiboro anamshukuru Papa kwa kazi hiyo ya uwajibikaji wa haraka katika mapambano ya Covid-19. Amekuwa wa hai tangu mwanzo na katika wito wake wa mara kwa mara ulimwenguni kuhusu mapambano dhidi ya janga hili na ni moja ya ishara ambazo amezionesha upendo wake, umakini wake, wasiwasi wake na ukaribu kwa ulimwengu unaoteseka.

Kwa mtazamo wa janga la covid-19 Askofu anatoa wito kwa watu wote wa Sudan Kusini ili waweze kweli kufuata na kuheshimu maelekezo yaliyotolewa na serikali, kwa namna ya pekee wa kulinda afya ya wote na zaidi walio maskini. Uwepo wa virusi vya corona ni janga kubwa kwa wale walio maskini zaidi na ambao wanakosa tayari miundo mbinu ya nyumba, kwa maana hiyo “tuombe Bwana aendelee kuwalinda na kubaki karibu nao”. Amehitimisha Askofu  Hiiboro.

10 April 2020, 16:26